Mkulima wa Kuku
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,270
- 534
hii iko vizuri! Actually mimi nafuga wa kienyeji na nina mayai kiasi cha trei 1 kwa siku sina wateja. Bei yangu ni 12,000/- kwa trei. Bado suala la packaging ni issue kwangu kwani sijui nitapata wapi hizo trei ndogondogo
nitakuuzia 5800 kwa traynikitaka kununua mayai yako yote.....utaniuzia bei gan kwa tray? we ucpate tabu ya ku supply?
hongera sana
ni kweli sasa tunahitaji umoja ili kuweza kushika soko, kama uko bunju basi we nenda bagamoyo ulizia wakala wa mayai ya jumla huwa anachukua hata tray 300 na kulipa cash hapohapo ila nenda kaunge biashara kwanza usiende nayo, Tray zako unarudi nazo.
Hizi tray ndogo zipo tayari ulizia tu, ukipata nenda supermarkets siku hizi nyingi tu watajie kiasi cha kuanzia tray 200 - 300 mfano kwa kila wiki nk kisha ulizia bei zao ila kwa hawa jiandae kuacha tray hapohapo.
Waweza kwenda interchick pale ni mwezi uliopita walikutana wafugaji ila mie sikwenda nilibanwa kazini ukiomba kuonana na meneja kwa tip kidogo anaweza kukupa idea mbalimbali. Bei ninazojua ni 5500 hadi 5800 kwa jumla na 6000 rejareja kwa tray.
MKUU HONGERA SANA KWA JITIHADA ZAKO, MUNGU AKUSAIDIE ZAIDI NA ZAIDI.
- KUHUSU BIASHARA YA MAYAI, NI KWELI KABISA KUNA DEMAND NA KUNA COMPETITION KUBWA SANA MKUU, WAZALISHAJI NI WENGI SANA NA MASOKO NAYO NI KAMA HIVYO NI MENGI.
- MKUU UFANYE NINI SASA? NAKUSHAURI UFANYE JAMBO MOJA LA MSINGI SANA NA JARIBU KUJIBU HAYA MASWALI,
1. JE KUNA KITU CHA ZIADA KATIKA HAYO MAYAI YAKO YAANI UMEYAONGEZEA THAMANI?
2. JE WANUNUZI WAKO NI WA KUAMNIKIKA? MMENGIA NAO CONTACT NA KUSAINI MOU?
3. JE KWA NINI WATU WANUNUE MAYAI YAKO NA SI MAYI YA WATU WENGINE?
4. UKIPATA SOKO NA KUKAWA NA SUPPLY WENGI WA MAYAI YA KIENYEJI UTAWEZAJI KU KOMPITI NA HAO WENGINE?
- MKUU JARIBU KUTAFUTA NJIA YA KUYAONGEZEA THAMANI HAYO MAYAI YAKO HASWA KWENYE PAKING. USIISHIE KUWEKA KWENYE TRY NA KWENDA KUTAFUTA MTEJA.
- TAFUTA VIFAA VYA KISASA VYA KUPAKI MAYAI KIASI KWAMBA MTU ANAWEZA BEBA BILA KUHOFIA KUPASUKA KWA MAYAI.
- UKISHA PATA PATA HIYO PACKING NZURI YA KUWEZA KUPAKI HATA MAYAI MATANO MATANO, JARIBU KUTAFUTA SOKO KWA KUZUNGUKIA SUPERMARKET MBALAMBALI NA MIN SUPRTPARKET PAMOJA NA MADUKA YA REJAREJA, MKUU NINA UHAKIKA ASILIMIA 100% UTAPATA SOKO ZURI SANA ENDAPO UTAKUJA NA AINA MPYA YA KUPAKI MAYAI,
- WOTE TUSIISHIE KUPAKI KWENYE TRY YA MAYAI 30, TUJE NA AINA MPYA AMBAZO HATA HUKU KWETU SI NGENI SANA KWA SUPERMAKET KUBWA KAMA SHOPRITE,
- MKUU JARIBU KUPAKI IDADI NDOGO NDOGO KAMA HII MAKE KUNA WATEJA HAWAHITAJI KUNUNUA MAYAI 30 TREI NZIMA KUTOKANA NA MAISHA YAO.
- SI KWAMBA HAYA MADUKA MAKUBWA YA MAKUBURU HAYATAKI KUNUNUA PRODUCT ZA WABONGO ILA NI AINA YA PACKEGING ZOTE NDO TATATIZO.
- TUNAISHIA KULALAMIKA KWAMBA WANAAGIZA MCHICHA TOKA SOUTH AFRICA, TUKIZANI TUNAWEZA WAPEKEKEA MCHICHA UKIWA UMEFUNGWA MAFUNGU MAFUNGU NA KAMBA ZA MIGOMBA WANUNUE.
INATAKIWA TUBADILIKE HASA KWENYE PACKEGING ZETU, TUSIISHIE KULALAMIKA NYAMA INAAGIZWA TOKA SOUTH AFRICA, HAYA MADUKA YANA MAINTAI QUALITY HAYA WEZI ENDA BUCHANI PALE KARIAKOO NA KUNUNUA TU NYAMA NA KUPELEKA MADUKANI MWAO,
MKUU HUO NDO MCHANGO WANGU,
asante mkuu nitakutumia info zangu kwa ajili ya Biashara na mimi nina biashara nataka kuitangaza
nashukuru sana kwa ushauri!.
Soko la ndani halitabiriki kwani nimejaribu kwenye hotels kubwa, wa mama wauza mayai, wauza chips na sehemu nyingine zinazohitaji mayai (kama 25 trays kwa siku), wameniambia wenyewe wanafuga kuku wao. Hapo nikaona inanishinda kwani soko na bei hazitabiriki.
Katika kuulizia, nikaambiwa kuna mzee mmoja ana-export mayai ila inabidi mtu awe na high and consistent production capacity.
Sasa ndio nikawa najaribu kuulizia hapa jamvin kwa aliyekwisha msikiai.
Sikumaanisha mimi nataka niwe-exporter, no!.nataka ku-damp kwake (+ kufunga hesabu) then yeye ataendelea na vibali and other logistical issues kwani ndiye mzoefu kwenye exportation ya mayai.
So, soko la ndani yawezekana kabisa haliko saturated kama unavyosema ila lina zengwe na other non-tariff barriers zisizotabirika.
Obonyo!.
Nimekupata Dio, Nashukuru.
Basi ntakutafuta mwanzoni wa 2012, Mungu akitujalia.
Obonyo!.
Pale sinza karibu na mwika kuna jamaa ana frame yake anauza mayai tu, anaiita Mayai centre... Anauza mayai mpaka wateja tunachanganyikiwa na yeye anayatoa mombasa kenya... Sasa pamoja na usafiri na kila gharama anazopata bado anauza bei sawa na hapa dar. Sasa jiulize huko anayanunua kiasi gani.
Mkuu tunapozungumzia soko la ndani haimaanishi tu dar es salaam. Mi nilienda masasi nikakuta mayai ni adimu sana na watu wanayanunua kwa kila nguvu... Sasa fanya utafiti mikoa gani haina wafugaji ukafungue duka/maduka yako ya mayai, ila hakikisha una minimum tray 1000 za kuanzia, na yasiwe yamekaa saaana...
Tatizo watanzania wa mjini tuko so Dar minded, tunawaza Dar tu, dar dar kama vile dar ndio world trade centre??? LoL, mikoani kuna opportunities sana, mkuu tutembee tuone...