Vitu gani vya kuzingatia hasa unapofanya biashara ya uuzaj wa mayai ya kisasa?

Vitu gani vya kuzingatia hasa unapofanya biashara ya uuzaj wa mayai ya kisasa?

Nakushauri uende Muvek wako Mikocheni karibu na kwa nyerere, Njia inayoenda FEZA School... Ukiuliza utaonyeshwa... Watakusaidia kila unachotaka kujua pamoja na kupata vifaranga...Wana kitabu kidogo kinachoelezea kila kitu kuhusu ufugaji wa kuku wanakiuza elf 5 (5,000). Nipm nikupe namba ya Muhusika kama utapotea akuelekeze.
 
Jamani wana jf kuna mwenye idea na ufugaji na utunzaji wa kuku wa mayai?naweza kupata wapi kuku wa wiki kumi na kwa bei gani?nahitaji kuku 500.nitawafugia shinyanga mjini.Je ni miezi gani mizuri ya kuwafuga,namaanisha miezi ambayo haina magonjwa.
 
jamani wana jf kuna mtu yeyote anaweza kunisaidia kunipa idea juu ya ufugaji na utunzaji wa kuku wa mayai wa kisasa}layers}.Nataka kujua wapi naeza kuwanunua kuku wa wiki kumi,na je wanauzwa kiasi gani kwa kuku 500.
 
Wadau nina wazo la kufanya biashara ya kufuga kuku wa mayai kwa lengo la kuuza mayai(ya kisasa). Nimejaribu kufanya utafiti kidogo kuhusu breed nzuri ila napata mawazo mchanganyiko, wengine wanasema interchick, wengine breed za malawi au zambia, wengine za arusha ambazo hutolewa kenya. Mbali na breed nimefanya pia utafiti wa chakula na hapo sina shida sana nimepewa formula ya kutengeneza chakula mwenyewe kwa stage tofautitofauti ya ukuaji wa kuku. Kwa upande wa magonjwa ndo sehemu hasa ninayopata shida kwani katika utafiti wangu kila mtu anakiri kuwa changamoto kuu ni magonjwa ambayo huweza kuuwa kuku wengi kwa mda mfupi sana. Nahitaji mdau mwenye uzoefu na biashara hii anipanue mawazo zaidi kuhusu changamoto hii ya magonjwa, breed nzuri, ni njia gani zipo za kuzuia au kukinga magonjwa hayo, soko la mayai kwa sasa likoje,mayai feki toka kenya yameharibu soko au la? Na taarifa zozote muhimu kabla sijaanza utekelezaji wa biashara hii.
Natanguliza shukrani wakuu
 
Umejianda anda aje? Biashara inayousisha vitu vya uhai ni nomaaaaaa.
 
Umejianda anda aje? Biashara inayousisha vitu vya uhai ni nomaaaaaa.
Kujiandaa kwa namna gani unaulizia? Kutafuta hizi taarifa ni moja wapo ya maandalizi hasa kwa upande wa kupunguza business risk. Nikipata mawazo ya mtu mwenye experience ya biashara hii itanisaidia from practical perspective. Aidha kwa upande wa facilities na resources nipo okey!
 
Kama upo kwenye centre za miji/wilaya au jiji waweza kuwaona wataalamu wa mifugo. Kuhusu soko hili ni jambo la mwanzo ambalo unatakiwa kufanya utafiti kwenye eneo ulilopo kwani hakuna biashara bila soko. Unapaswa kuanzia hapo ndio utajua kuna haja au hakuna ya kuanzisha biashara unayoikusudia.
 
Maelezo mbona kama hayakujitosheleza mkuu akina sisi hatukuambulia chchote
 
Wakuu heshima nyingi! Mi niko Manyara hata road ya kwenda DSM siijui. Nielimisheni msinibanie ivo-hata hilo jina la kitabu nijaribu kutafuta huku! Shukrani mapema
 
Wadau wa naomba mwenye uzoefu wa biashara ya mayai ya kuku wa kisasa anisaidie ushauri juu ya mambo yafuatayo:
1) Je, biashara hii inalipa?
2) Je, ni muda gani mayai huaribika endapo sijauza?
3) Je, wapi naweza kupata mayai kwa bei nzuri na trei ni shilingi ngapi?
4) Trei tupu zinauzwa wapi?

Wadau natanguliza shukrani zangu, nikiamini kuwa mtanisaidia.
 
wewe unataka kuwa wakala? au mchuuzi kama ndio nenda kajifunzie kwa mawakala soko la Kinondoni au Ilala wanayanunua kwa wafugaji wengine wanauza hapa mengine zanzibar.
nadhani ungeanzia na soko kwanza maana mayai yapo tu kisha utajua faida itakuwa vipi
 
Wana JF,

Naomba mtu anaefahamu kuhusu wapi nitapata hiyo bidhaa kwa bei ya ushindani kwa jumla ili na mimi niweze kuuza na kupata faida, nataka kufungua hiyo biashara hapa mtaani kwa kuanzia nahitaji kama trey 100 hivi.

Niko Dar.

Nawasilisha.
 
Wana jf naomba mtu anaefahamu kuhusu wapi nitapata hiyo bidhaa kwa bei ya ushindani kwa jumla ili na mimi niweze kuuza na kupata faida, nataka kufungua hiyo biashara hapa mtaani kwa kuanzia nahitaji kama trey 100 hv.

Niko DAR

Nawasilisha.

Iliwahi kuletwa humu hii habari
Wakuu,

Kuna msiba mkubwa mno kwa hawa wafugaji wa kuku wa mayai ya kisasa, takribani mwezi sasa mayai yamefurika mji mzima - hakuna sokokabisa.

Imefikia hatua sasa mayai yanaanza kuharibika kwa kukaa muda mrefu bila soko, inasemekana mayai yametoka nje ya nchi - tetesi ni kwamba yametoka Kenya kwa njia za panya. kwani ushahidi unaonyesha kwamba mayai yanayozalishwa Tanzania hasa Dar - es - Salaam hayawezi kabisa kujaza soko la ndani.

Bei ya mayai haya imeteremka toka 7500 - 8000 kwa Tray moja hadi kufukia 4500 - 6000 Tshs. Lakini pia hayanunuliki hata kwa bei hiyo.

Tunaomba wahusika na wadau wote wa mifugo hasa Wizara ya mifugo waliangalie suala hili kwani linaua kabisa wafugaji wadogo wadogo.

Nawakilisha kwa niaba ya wafugaji wa kuku wa mayai

mleta habari alikuwa FUSO
 
Last edited by a moderator:
Wana jf naomba mtu anaefahamu kuhusu wapi nitapata hiyo bidhaa kwa bei ya ushindani kwa jumla ili na mimi niweze kuuza na kupata faida, nataka kufungua hiyo biashara hapa mtaani
kwa kuanzia nahitaji kama trey 100 hv.

Niko DAR

Nawasilisha.

Unahitaji mayai ya kuku wa kienyeji au ya kisasa
 
Mpigie +255713564785 atakupatia mayai kwa bei nzuri.

Ukihitaji vifaranga vya kuku au kware pia atakupatia.
 
Wanandugu kama ambavyo tumekuwa tukishirikiana kubadilishana mawazo kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai, hatimaye kumekucha.. Mimi nafuga kuku 1000, kati ya hayo 580 ambao ni awamu ya kwanza wanaanza kutaga. awamu ya pili wanaanza kutaga Januari. nina soko la mayai katika duka moja. ila ningependa kupata soko jingine pia.

uzalishaji unategemea kuwa kama tray kama 10 kwa siku au 70 kwa wiki. production itaongezeka kadri ziku zinavyoenda na pia wale wa awamu ya pili wakianza kutaga.

kama kuna mtu ahahitaji mayai au anaweza kunipa mawazo wapi naweza kuyauza haya mayai kwa ujumla tupeane ushauri.

mayai ni wa kuku wa kisasa. wale wa kienyeji nitaanza kuwafuga next year baada ya kukamilisha sehemu ya kuwaweka shambani.

Note: nafugia Dar, maeneo ya bunju.

mkuu bado unauza mayai? unauzaje kwa tray bei ya leo?
 
Back
Top Bottom