Najikuta nakosa cha kukuuliza
CONTROLA haki tena umemaliza kila kitu aiseh 😃
Lakini siwezi kubali nikaacha kukuuliza japo kidogo🤪unapenda kupika nini??na ukipika nani anaekula hicho chakula??maana unapenda kupika lkni huli😅😅
😄😄mkuu hakuna mtu kama wewe huko mtaani kwenu mwenye sifa kama hizi na yuko singali!!!aise mwamba umetisha...hakika wifi huko kila siku a namshukuru Mungu kwa ajili yako kukupata...
Wanaume kama wewe aiseh sidhani kama bado wapo😆😆😆
Chakorii mama nikisema kupika ujue ni kupika kila kitu,Hapa nilipo sina chakula sijui kupika Nadhani hii n kwasababu ya maisha yangu ya biashara biashara,labda utajiuliza nimejuaje kupika vyakula hivyo?!
Jibu ni kwamba :
Unajua mimi ni mfanyabiashara na moja ya biashara ninazofanya ni biashara za chakula,nina sehemu za kuuza vyakula zakutosha tu lakini mwanzo kbla sijawa expert wa jiko niliingiia ktk hii biashara nikiwa sijui lolote na nilianza kwa
kuajiriwa nilikua mtu wa jikoni kutumwa viungo vya jikoni na kuviandaa yani kama nikiletea makaroti,hoho,vitunguu,nk natakiwa vikatakata na kuviweka tayari CHIEF COOKER atapokuja anakuta kila kitu kipo tayari yeye anapika tu.
sasa ktk hatua hiyo nikawa najua aina za viungo na jinsi ya kuviandaa,maisha yaliendelea hadi nikawa siku 1 moja naambiwa
CONTROLA hebu pika kitu flani,natumwa nifanye ila ndio hivyo najifunza mwisho nikajua.
Nikafungua sehemu yangu nikaajiri raia waliokua wanapka ila nikawa napata changamoto ya wapishi,akifanya kazi wiki 1 wiki ya pili anakwambia ana dharura mwanae anaumwa,au amepata msiba,nikawa nateseka sana siku ambazo mpishi haji ikabdi nianze pikia wateja kibishi hivyo hvyo,napika wali m'bichi au umeiva upande mmoja mteja akija nifokea na kunikosoa au kunitukana nawabembeleza hivyo hivyo nikazoea nikawa najua kidogo kidogo,mwisho nikawa
MTU HATARI ZAIDI NIKIWA JIKONI.
Nikisema mtu hatari nikiwa jikoni ujue namaanisha,ukitaka ujue makali yangu au haya ninayoyaongelea nafananaje ingia insta mtafute chief cooker niliekua namuandalia viungo enzi hizo,huyo ndio mwalimu wangu anaitwa
Chefkile,napika namna hiyo aina zote za vyakula vya kitanzania ktk ubora wa chakula kuliwa na Wateja wakatingisha kichwa kukubali msosi ni wenyewe.