Vitu/vifaa gani ulivinunua kwa mihemko na umejikuta huvitumii kabisa?

Vitu/vifaa gani ulivinunua kwa mihemko na umejikuta huvitumii kabisa?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
1. Kuna kitu kinadumu kama mkanda wa ngozi?nakumbuka nina mkanda huo nilinunuliwa na babu yangu 2012 huwezi kuamini mpaka leo ninatumia huohuo japokuwa umechoka sasa mwaka jana mwishoni nikaona duka la mikanda ya ngozi nikanunua ila ilanibidi niutafutie kwanza msumari nitoboe tobo basi hio kazi ya kutafuta msumari imenishinda mpaka leo wala sina time nao mkanda Mpya nimeufungia tu kabatini bado natamba nao wa zamani wenye miaka zaidi ya 10 na fresh tu japo umelegea sio smart.

2. Karibu yangu kuna swimming pool nikaogelea siku moja sasa kwa kuwa sijui kuogelea nikaingia mtandaoni nikaagiza swimming gears kama fins, goggles lengo niwe naogolea kila siku ..vifaa vikawasili ila hamasa ya kuogolea siioni tena kumbe sio hobby yangu kumbe ilikuwa mihemko tu.

3. Air fryer nilinunua maana niliiga kwa jamaa yangu ..nikalinunua ila nilipoonja tu kuku niliyemchoma nalo sikurudia tena kuku anakuwa hana ladha kabisa bora kukaanga na frying pan tu nimeliacha mpaka lile li basket lishaanza kupata kutu

4. Blender pia miyeyusho haitoi juice smoothie kama zile zilizosagwa na blender zenye nguvu..
vitu vingi watu tunanunua kwa kufuata Mkumbo tu.
 

Attachments

  • 20260430_123743.jpg
    20260430_123743.jpg
    184.8 KB · Views: 27
  • 20260430_123650.jpg
    20260430_123650.jpg
    185.2 KB · Views: 29
  • 20260430_123813.jpg
    20260430_123813.jpg
    341.1 KB · Views: 22
Back
Top Bottom