Vitu vingine ni kama vya kijinga ila vina matokeo. Nimejaribu kufuata ushauri wa huyu Member, nimeona utofauti

Vitu vingine ni kama vya kijinga ila vina matokeo. Nimejaribu kufuata ushauri wa huyu Member, nimeona utofauti

Right Way In Light

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2024
Posts
1,322
Reaction score
3,461
Mabibi na Mabwana habari zenu.

Sio kitu muhimu sana but kimenifanya nijione maisha kuna muda mwingine yanaweza kupoteza vitu flan maishani mwako ambavyo japo unavichukulia kama minor issues but in real sense they are not.

Kwanza kabisa fahamu kuwa;
Ni muhimu sana kuwa makini na mambo yanayoshauriwa mitandaoni. Yapo yenye manufaa japo yana sura ya ukawaida au ubaya. Na yapo mabaya japo yanashauriwa kwa uzuri na ushawishi mkubwa.

Nirudi kwenye mada:

Mfano mimi na utu uzima wangu huu, ni mtu ambaye nimekua najali sana family kuliko hata ninavyojijali mimi.

Mimi honestly sikuwah ona kama kwangu ni muhimu sana mambo ya kuvaa na muonekano, kuliko kujali wanangu wale na wavae vizuri. Japo zamani wakati wa ujana huko nilikua najali kidogo hizi mambo but baada ya kuoa Nikawa najichukulia aah ile less than average yan, kwangu kipaumbele ni family.

Sikuajua kitu nilichokua nakipoteza, the value..

Sasa siku moja nikakutana na uzi wa mdogo angu Natafuta Ajira kuwa unapopambania familia na kuandaa future yao usijisahau na wewe pia, jipe kipaumbele kwanza 😂.
(Nimeshindwa kukumbuka exactly jina la ule uzi).

Sasa mimi at 35 now, nikawa najichukulia aahh nishazeeka tayari haya mambo ya kujali mjonekano na mavazi ninya vijana zaid, acha nifanye mambo ya msingi zaidi.

Honestly ndio hiv karibuni nimekuja kugundua kumbe nina viatu pair 2 tu, jinsi 2 na suarual 2 tu, shati chachee hazifiki 4 na tshirt hazifiki 3 😅😅. Haya yote nikikua naona normal tu, hata sijali, mimi najali family...wale vizur, wavae vizuri.. punda afe mzigo ufike.

Si nikajaribu bwana huu ushauri wa bwana Natafuta Ajira 😂😂. Nikajikumbuka na kujaribu kujirudisha enz zangu za 20's, every time doing simple shopping for myself, nikiingia town, nunua nguo mbili tatu kali kila napopata fursa ya kuzunguka mjini, after every sometime kuji sop sop salon, weka kichwa safi (nina uwaraza so napendeleaga kunyoa dongo/upara wa wembe), weka ndevu fresh, marashi ya hapa na pale, vitu ambavyo nilishaachaga kufanya japo vyote viko ndani ya uwezo wangu, nikawa najifanya niko busy kupambania familia.

Doohhh!! Kiukwel nimeanza ku experience huge changes, kuanzia namna watu wanavyonitzama now, wanavyonichangamkia mpaka mabinti na mishangazi age mates wangu naona like i send attraction signals to them bila kusema neno and they are trully affected tofauti na hapo kabla.

Na kubwa zaid , am feeling veery good far better that before.

Najisikia raha kabisa.

KUbwa zaid mpaka wife juzi kaamua kunipiga kijembe maana hajanizoea hivi toka tumeoana for 10 years sasa, so naohisi kavumilia mwisho kachoka, akanambia " naona mwenyewe siku hizi unapendeeeeza , huku wanao unawasahau" 😂😂😂😂😂😂.

Nikajua hapa tayari dozi imeshakaa mahala pake....😆😆😆

Uzi tayari.
 
When you are 35, priority inakuwa kuboresha muhimu vikutegemeavyo na vinavyokuzunguka vilivyo muhimu kwa ajili ya maisha yako (family, wazAzi, kazi yako, kujenga, afya, etc)

Ndio maana at 35 kama ni mtu timamu hauwez kukuta anafukuzana na mademu au fashion.
 
Mabibi na Mabwana habari zenu.

Sio kitu muhim sana but kimenifanya nijione maisha kuna muda mwingine yanaweza kupoteza vitu flan maishani mwako ambavyo japo unavichukulia kama minor issues but in real sense they are not...
Nimecheka mpaka nimelia yaani umeamua kujikumbuka ,hapo Safi kabisa sio muda na shemeji ataanza kujijali zaidi akihofia usijepata lidada lizuri huko kazini ukasahau familia.
 
When you are 35, priority inakuwa kuboresha muhimu vikutegemeavyo na vinakuzunguka vilivyo muhimu kwa ajili ya maisha yako

Ndio maan at 35 kama ni mtu timamu hauwez kukuta anafukuzana na mademu au fashion.
Hata mimi huu umekua ni mtazamo wangu kwa miaka yote, ila nimeamua kubadil fikra as long as majukumu ya msingi natimiza na pia sifukizan na madem wala fasheni.
Kujipenda hakuhusiani na fashion
 
Ahahahah mkuu yan una haki kabisaa ya kunicheka. Niliji susa mnnooo
Uwa ni hatua nahisi katika nyakati za uanaume wetu ,hata Mimi nimewahi kata miezi nane bila nguo mpya ,nguo zikachakaa Sana ,viatu vikawa vinapokezana kuchanika ila sikuacha kuvivaa ,Sasa kazini wakasema nimepata ngoma hivyo nimejizira niko tayari kufa muda wowote 😀😀

Nikaja nikabahatisha hela Fulani ya mkopo ,walinikoma kama ,yaani nilikuwa na unyunyu huo nikijipulizia wote wanajua ni Mimi hata Kama sijafika walipo .

Wanaume tujipende jamani ,mwanaume asifiwi kutokuwa mtanashati eti ndiyo uanaume
 
Picha ya before and after
Screenshot_20241016_173535_Samsung Internet.jpg

Now vs Before
 
inatakiwa uwe nadhifu si kwa ajili ya mabinti na mishangazi,
Hakuna mahala nimesema hiki kitu mkuu, unanizushia tu, but i dont mind, probably hujanielewa
pia kama una changamoto na mkeo zitatue badala ya kumpiga vijembe huku jf.
SIna changamoto na mama watoto wangu, kwa miaka 10 pamoja, hakuna changamoto yoyote mpya .
Na wala sijampiga vijembe..
 
Wanaume tujipende, tujiongezee thamani, tujipe kipaumbele vile vile tufanye maandilizi ya kuweza ku-survive nyakati zetu za uzeeni.

Tusiweke matarajio makubwa sana kwa watoto. Watoto wakiwa wakubwa na kuanza kujitegemea wana kawaida ya ku-reside zaidi upande wa mama
 
Wanaume tujipende, tujiongezee thamani, tujipe kipaumbele vile vile tufanye maandilizi ya kuweza ku-survive nyakati zetu za uzeeni.

Tusiweke matarajio makubwa sana kwa watoto. Watoto wakiwa wakubwa na kuanza kujitegemea wana kawaida ya ku-reside zaidi upande wa mama
Muhim kulizingatia hil kwa hakika
 
Back
Top Bottom