Mabibi na Mabwana habari zenu.
Sio kitu muhimu sana but kimenifanya nijione maisha kuna muda mwingine yanaweza kupoteza vitu flan maishani mwako ambavyo japo unavichukulia kama minor issues but in real sense they are not.
Kwanza kabisa fahamu kuwa;
Ni muhimu sana kuwa makini na mambo yanayoshauriwa mitandaoni. Yapo yenye manufaa japo yana sura ya ukawaida au ubaya. Na yapo mabaya japo yanashauriwa kwa uzuri na ushawishi mkubwa.
Nirudi kwenye mada:
Mfano mimi na utu uzima wangu huu, ni mtu ambaye nimekua najali sana family kuliko hata ninavyojijali mimi.
Mimi honestly sikuwah ona kama kwangu ni muhimu sana mambo ya kuvaa na muonekano, kuliko kujali wanangu wale na wavae vizuri. Japo zamani wakati wa ujana huko nilikua najali kidogo hizi mambo but baada ya kuoa Nikawa najichukulia aah ile less than average yan, kwangu kipaumbele ni family.
Sikuajua kitu nilichokua nakipoteza, the value..
Sasa siku moja nikakutana na uzi wa mdogo angu
Natafuta Ajira kuwa unapopambania familia na kuandaa future yao usijisahau na wewe pia, jipe kipaumbele kwanza 😂.
(Nimeshindwa kukumbuka exactly jina la ule uzi).
Sasa mimi at 35 now, nikawa najichukulia aahh nishazeeka tayari haya mambo ya kujali mjonekano na mavazi ninya vijana zaid, acha nifanye mambo ya msingi zaidi.
Honestly ndio hiv karibuni nimekuja kugundua kumbe nina viatu pair 2 tu, jinsi 2 na suarual 2 tu, shati chachee hazifiki 4 na tshirt hazifiki 3 😅😅. Haya yote nikikua naona normal tu, hata sijali, mimi najali family...wale vizur, wavae vizuri.. punda afe mzigo ufike.
Si nikajaribu bwana huu ushauri wa bwana
Natafuta Ajira 😂😂. Nikajikumbuka na kujaribu kujirudisha enz zangu za 20's, every time doing simple shopping for myself, nikiingia town, nunua nguo mbili tatu kali kila napopata fursa ya kuzunguka mjini, after every sometime kuji sop sop salon, weka kichwa safi (nina uwaraza so napendeleaga kunyoa dongo/upara wa wembe), weka ndevu fresh, marashi ya hapa na pale, vitu ambavyo nilishaachaga kufanya japo vyote viko ndani ya uwezo wangu, nikawa najifanya niko busy kupambania familia.
Doohhh!! Kiukwel nimeanza ku experience huge changes, kuanzia namna watu wanavyonitzama now, wanavyonichangamkia mpaka mabinti na mishangazi age mates wangu naona like i send attraction signals to them bila kusema neno and they are trully affected tofauti na hapo kabla.
Na kubwa zaid , am feeling veery good far better that before.
Najisikia raha kabisa.
KUbwa zaid mpaka wife juzi kaamua kunipiga kijembe maana hajanizoea hivi toka tumeoana for 10 years sasa, so naohisi kavumilia mwisho kachoka, akanambia " naona mwenyewe siku hizi unapendeeeeza , huku wanao unawasahau" 😂😂😂😂😂😂.
Nikajua hapa tayari dozi imeshakaa mahala pake....😆😆😆
Uzi tayari.