Vitu vya kuanza navyo kuchochea safari ya kutajirika mapema

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Pesa inayokutajirisha ni ile inayogeuka kama chambo ya kunasa pesa zaidi.

Kuna mambo unayotakiwa kuyadhibiti kabla hujakurupukia ndoto za utajiri. Mambo ambayo yatakusababisha kila kinachoingia kiingie ili kilete pesa zaidi

1: Chakula
Hakikisha una mfumo imara wa kula tena kula vizuri. Malizana na chakula kwanza. Usikimbilie kutajirika kwa kupuuza utajiri wa afya. Utakufa kabla ya utajiri wako. Masikini ndio wanakula mara tatu maana wao karibh 59% ya akili zao wanawaza kula. Ukidhibiti mfumo wa chakula hata ukila mara moja kwa siku huna wasiwasi maana unauhakika ukitaka kula muda wowote mfumo wako unakusuport.

2: Acha NGONO
Oa mke mmoja unayeendana naye. Safisha kitengo cha zinaa. Zinaa na pombe vinaukaribu sana na umasikini. Kuna takwimu hafifu sanaa za mabilionea wazinzi au mwenye kashfa za uzinzi. Mo, Bakhresa, Bilgate, Slim, Dangote, Motsape, Katumbi huwezi kuwakuta kwenye magazeti ya udaku eti wamefumaniwa.

3: Dhibiti malalamiko ya familia
Hakikisha umeituliza familia. Mama anakula vizuri, anavaa vizuri, watoto wanaamani. Pesa za maana hazikai kwenye magomvi. Utulivu wa familia unaambukiza hadi ubongo kitengo cha fedha.

4: Dhibiti mihemko ya fedha kwa kutokurupuka zinapoingia
Inashauriwa ukipata pesa yoyote angalau iache ipumue hata siku tatu ndio uanze kuitumia. Hii itakutolea wenge na uchu wa mikurupuko ya kifedha. Tena ukiweza chukua tu kiasi kikubwa tembea nacho mtaani bila kukitumia.

Mimi ni hayo tu,
Kama unanyongeza uwanja ni wako.
 
Point namba 4 ndo kubwa sana, kuna kipindi nilikuwa nakula msoto wa maana na kwenye savings kuna zaidi ya 80M kipindi nabeba zangu maboksi Texas ila nilikuwa najua hio hela ina kazi gani kwahyo i wasnt even moved kuanza kuishikilia.
Watu mna roho ngumu sana,yaani unachapika na shida na una 80mln🀣🀣🀣.

Wacha niishi mie ya watu sijawezi kwakweli.
 
m
madini Poor Brain dronedrake Intelligent businessman Mbaga Jr
 
Watu mna roho ngumu sana,yaani unachapika na shida na una 80mln🀣🀣🀣.

Wacha niishi mie ya watu sijawezi kwakweli.
Mimi ninaweza nikawa na ela il sina ela
Yaani una ela ya kitu kingine lakini ya kingine huna
Ndo ulimwengu wa pesa na displine ya peaa ulivyo hii ufundishwi darasani
 
Umetisha kinoma Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…