Habari za siku mbili tatu wakuu na wananzengo hapa jukwaani?
Your browser is not able to display this video.
Hi video ni ile ya uchaguzi Mkuu 2020 nimeitumia hapa kutaka kusema kitu kuhusu hizi chaguzi
Unajua kwa kawaida kabisa ni wazi Majeshi yetu hayatakiwi kuchagua upande, majeshi yetu hayatakiwi kuonesha hisia zao wazi kisiasa.
Askari wetu n majeshi yetu kwa ujumla wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo wakati huu wa uchaguzi ili uchaguzi uwe wa HAKI Na Amani.
1. Impartiality - Jeshi ama Askari hatakiwi kuchukua upande Na kuuweka wazi,Ni Hatari sana Kwa Askari kuuonesha umma Kuwa yupo upande gani,bahati mbaya Askari huyu kaonesha upande wake Ni upi (Partial)
2. Objectivity - Askari ama Jeshi hatakiwi kuonesha Na kuweka hisia zake pale anapokuwa Kwenye shughuli zake,bahati mbaya sana Askari huyu kaweka hisia Kwa kuhukumu,hakutakiwa kufanya hivyo.(Subjectivity).
3. Fairness - Askari anatakiwa Kutenda HAKI bila upendeleo.
4. Rule of Law - Katika kila anachofanya Askari Ni sharti afanye Kwa mujibu wa sheria Na siyo Kwa matakwa yake ama kadri anavyoona.
5. Human rights - Askari katika kutimiza wajibu wake anatakiwa kuhakikisha analinda Na kuheshimu HAKI za binadamu.
Wito wangu
Jeshi la Polisi Na Askari wake wajitenge Na mtego huu wa kuchukua upande, matokeo yake huwa hayana Afya Kwa ustawi na Amani ya nchi.
Watanzania wengi bado hawajajua tofauiliyopo kati ya CCM na serikali. Wengi huona CCM ni serikali. Ukiwa mpinzani unaonekana wewe ni muasi. Wanashindwa kutofautisha kati ya chama na serikali. Hiyo ni kutokana na historia ya CCM namna ilivyozaliwa. Wakati vyama vya TANU na ASP zinaungana kuunda CCM, pia nchi zikawa zinaungana na kuzaa Tanzania 🇹🇿. Pengine waliosanifu na kubuni muungano wa nchi walitoka kwenye vyama husika. Hivyo wanahisi serikali ya muungano ni mtoto wao. Hakuna namna ya kutenganisha. Wanaona ni kazi ya mikono yao. Hakuna mtu wa kuwapokonya. Hivyo elimu iendelee kuhusu utofauti kati ya vyama na serikali.