Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

Halafu huko Arusha ndio yamejaa makanisa ya ajabu ajabu kweli....itakuwa wameona waarusha wengi Ni manzwanzwa tu ndio maana machungaji mengi ya uongo yanakimbilia hukoo
Wapo kila mahali mkuu.

Kuna kijiji kimoja kule Machame, hawaruhusu kabisa mahema, kwasababu wanatapeli watu.
Wao wameweza kuyadhibiti kabisa.
 
[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hii mbona km chai mkuu
Inaweza isiwe chai mkuu.
Hukumbuki ile iliyotrend sana Ya Jamaa alipeleka mke wake aolewe na Mchungaji wake.
 
Dini ya kikristo imeyeyuka sana na imeshuka thamani michango mingi.

Saivi hakuna uhuru ukisali agrican wewe mroma unapigwa madongo, ukiwa mlokole ukihama kanisa unapigwa madongo, ukisali roma wewe ni kkt utapigwa madongo saa zingine unaonekana ni kondoo uliepotea hakika kwa sasa ubinafsi mkubwa wa kuona kila mmoja ana thamani tumekua wakujipenda wakati sisi wote kilio chetu ni kupitia mwana wa adam aliekufa msalabani,sisi ni watoto wa abraham, isaka na yakobo ila ukisema umeungana nao wanakupokea na kusema karibu ila ukiwa umeenda kujisalia vijembe vingi kuliko neno lenyewe.

Ubaguzi kama huna jumuiya kanisani utaisoma namba utasemwa sana, kuna watu tunataka kusali na kuondoka ila mwishoni makanisa mengine mnapigwa madongo jamani kwa biblia inalazmsha hayo kuna maeneo huwezi kuta kanisa lako.

Michango imekua mingi wakati hali hairuhusu kila kukicha ni kujenga makanisa likikamilika ujenzi mwingine sijui unatokea wapi Hakuna Amani Ya Kusali tena.

Kwa kweli hizi zama ni za mwisho tunasali kufuata ratiba lakini tumekosa uhusiano na Mungu kupitia kristo tunasali kutimiza wajibu ila ndani hakuna kitu kabisa.


All in all makanisa ya kilokole madhabahu zao wanaweka mazindiko mazito sana haiwezekani tulazimshwe kuzizunguka na kuomba wakati unaweza omba ukiwa hata umekaa kwenye siti yako.

Kuna kanisa moja hapa kati kati ya tz dodoma watu walipangwa kufanya ibada asubuhi kumbe kuna ng,ombe kachinjwa toka saa kumi usiku kufika saa kumi na mbili kisha iva wakaambiwa kuleni lakini mifupa kusanyeni sehemu moja, ilivyofika saa kumi na mbili wakiwa wamemaliza kula walianza ibada alitua tai mkubwa mida ya saa kumi na mbili na madakika wakaambiwa wamzunguke waombe wakiwa wamefumba macho.

Walivyomaliza watu walibaki mdomo wazi wakuhama walihama wakuendelea waliendelea.


Nimepita makanisa Mengi kwa sababu sio kila eneo utakuata kani lako mfano KKKT, AGRICAN na T.A.G lakini ROMAN CATHOlIC wamejipanga mpka vijiji ambavyo huwezi tegemea lakini wapo.
😁😁😁Umenikumbuka nilivyopewa madongo kanisa Moja hivi lipo maili moja mbele kidogo ya kiluvya.
 
Ukiwaambia ukweli utaambiwa unamkufuru Mungu , na vifungu kazaa vya “ Ole Wake .....” utasomewa
Msela aliyeachana na mke tulikuwa tunaishi eneo moja, yaani ndani ya compound moja.
Ni vituko kwa kweli na wanafanya hadi mikesha ya maombi na kufunga.
 
Baba mmoja mkewe alikuwa anasali kanisa moja la kilokole ,ulokole ukamuingia kweli kweli yule mama,jumatatu hadi jumapili yeye ni kanisani akikosa kanisani anaenda nyumbani kwa mchungaji asubuhi anadamka anapika chakula cha kushinda nacho mpaka jioni muda ataokuwa kanisani,baba mwenye nyumba ile tabia ikamchomsha jumapili akaamka akaenda kanisani akawakuta wako kwenye maombi mchungaji yuko mbele,akamchukua mke wake mpaka mbele akawa anawagonganisha vichwa na mchungaji anawaambia eti "oaneni sasa"[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

[emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bahati Buku katalakiana na mumewe, kaanzisha kanisa Tabata Segerea, Chama
Wakuu, ni dhahiri kuwa kuna makanisa yanaibuka sasa kama uyoga. Sioni shida kuibuka kwa makanisa kila kukicha, kwasababu hata baa mpya zinaibuka kila siku.

Pamoja na yote, haya makanisa kuna baadhi yana vituko sana, yaani Mtumishi anaweza kuwa Mtume, Nabii au Mchungaji lakini mambo wanayofanya ni vituko na ajabu! Cha kushangaza bado waumini wapo.

Nianze mimi.
1. Hichi kituko kinaendelea kutokea kanisa moja Arusha, mtumishi kaacha familia Dar, kaenda kutumika Arusha kapachika muumini mimba, mke Kaenda Arusha, kulalamikia kanisa kuwa amefunga ndoa na huyo mtumishi, kituko Kanisa linamtetea Mtumishi kuwa wao hawakujua kama ameoa. Hivyo ataendelea kutoa huduma kanisani, can you imagine!!

2. Jamaa yangu huyu kaanzisha kanisa lake, kapata waumini wakutosha! Kaoa mke November, February mwaka unaofuata mke anaondoka na kila kitu, kwa madai mume wake ni mzinzi, shutuma zinafika kanisani, waumini wanaungana na mchungaji wao kukemea [emoji23][emoji23][emoji23]. hii ni Kilimanjaro.

3. Christina Shusho anaanzisha kanisa baada ya kutalakiana na Mume wake na ana waumini wakutosha. Ya kujifunza ni mengi hapa.

Tuendeleze vituko vingine....

4. Kituko kingine kitazame hapa kwa huyu Jamaa, anasema amemmisi sana Shetani.
Hii ni hatari sana.

 
Siku asimame shekhe msikitini aseme kaoteshwa na mungu kwa hiyo kuna maji ya upako anauza kikombe Jero, huyo shekhe kama akitoka salama humo msikitini sijui,,,, lkn upande huu pili sijui kwanini mnaongopewa kizembe, yani masanja nae mchungaji achilia mbali yule wa kuitwa nabii frola😄
 
Siku asimame shekhe msikitini aseme kaoteshwa na mungu kwa hiyo kuna maji ya upako anauza kikombe Jero, huyo shekhe kama akitoka salama humo msikitini sijui,,,, lkn upande huu pili sijui kwanini mnaongopewa kizembe, yani masanja nae mchungaji achilia mbali yule wa kuitwa nabii frola😄
Na mwingine yuko hapo Kimara anajiita Musa huyo ni noma balaa
 
Back
Top Bottom