Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

Mbona shehe yahaya majini anauza vichupa vya maji ya baraka kutoka uarabuni.

Siku hiyo ndio niligundua kuna mashehe hama mitume na manabii. Vimaji vinanguvu maana alipofungua kamoja tu uwanja mzima wanawake wakalipuka mapepo.
 
kimeumana
 
Nmegundua, wote waliochangia hili bandiko hawajasikiliza wala kuangakia Video iliyowekqa. Leo ndo nmeamini bando limepanda bei.

Kuna watu wakilisikiliza hiyo Video, watafuta Post zao. Wakurupukaji wanaitwa.

Hata mleta mada hajaaangalia Video yote. Ajabu
 
Acha kujisahaulisha...
Mbona mnauza miti shamba huko misikitini?
 
[emoji23][emoji23][emoji23] zote kali.. Kinachoniacha hoi ni nabii mzinzi akilamatwa ugoni waumini wanamlinda na kumuombea eti ni vita!
 
Toa utapeli wako hapa.
 
In short ukiwa kama ni Mkristo, unapaswa utambue hakuna kanisa ambalo halina mwanzilishi (mwanadamu mmoja au kikundi cha wanadamu) na hiyo ipo hivyo kwa kanisa kongwe au la sasa...

Hivyo kama kuna udhaifu wowote, hayo ni matokeo ya uwepo wa wanadamu kama viongozi au waumini...

Sisi wanadamu tumekuwa wepesi sana wa kuona watu wengine wasio na msimamo sawa na sisi kama wanakosea, aliye mlokole ataona asiye mlokole kapotea na kinyume chake pia...

Kama kuna mwanadamu wa imani yoyote aliye kamili kwa kila idara, basi na anyooshe kidole...

Na kama wewe ni Mkristo kweli (kwa kufuata maandiko), inasemwa huko kwamba mwenzako akipotoka wewe muombee arejee kwenye mstari na sio kuanza kumsimanga (usihangaike kutoa kibanzi kwa mwingine, ingali una boriti)


Lk 6:41-45 SUV
Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako. Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maeneo ya mijini makanisa hayo yako mengi sana kuliko vijijini na sehemu ambazo watu hawana hela,

Je hii haitoshi kuonesha kuwa jamaa wako kutafuta pesa zaidi kuliko uinjilisti?
 
Dar ndio Ma mogul yamejazana huku.
1. Gwaji
2. Buldoza(Mwamposa)
3. Mzee wa Upako-mlevi mlevi huyu sikumbuki vizuri jina lake.


Sasa hivi wameanza kwenda Dodoma kama strategic region.

Wameona pamekuwa makao makuu pana fursa kidogo na watumishi wa Umma na wageni kwa hiyo sadaka zitapatikana kwa wingi kuliko zamani.

Yani wao wanalenga Penye kupata hela tu mengineyo ni ziada.

Wakati imeandikwa kuutafuta ufalme wa Mungu kwanza na haki yake yote na mengio kuzidishwa lakini wao wanaanza kutafuta mazidisho kwanza Yani mengineyo ufalme badae.

Utaua na kuridhika wafaa sana kuliko fedha na mali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…