Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

mtoa mada umenikumbusha dogo wangu wa kitaa Martin tangazi alivyofanyiwa na TFF..hii nchi ni ngumu sana kama mnakumbuka miaka ya uko nyuma kuanzia 2011 kulikuwa na mashindano ya Airtel rising star wanatafutwa vijana wenye vipaji then wanapelekwa Qatar kwenye Academy ya mpira wakachaguliwa watu kutoka kwenye shule mbalimbali za sekondary alafu ukafanyika mchujo bahati nzuri uwo mchujo aliyekuwa anausimamia ni mzungu kutoka Spain ukapigwa mchujo dogo akapità wakapelekwa karume wakaungana na wengine ili upigwe mchujo wa mwisho kitaifa then waliyopita moja kwa moja Qatar basi dogo kama bahat napo pale akatoboa wakawa wamechaguliwa watu kama 10 ndio waliofuzu wanaenda Qatar dogo akaanza kufuatlia mambo ya pasport kila kitu kikawa sawa sasa siku ya kuondoka waliambiwa wote waliochaguliwa wafike makao makuu ya TFF asubuhi saa1 dogo saa 12 tayari alishafika muda ulipofika wakawa wanaitwa majina then wanaingia kwenye coaster la TFF moja kwa moja Airport dogo anashangaa majina yameisha alafu yeye ajasikia jina lake akauliza mimi sijasikia jina langu na kwenye mchujo nilipita wakamuuliza unaitwa nani akawajibu akaambiwa mbona Martin tangazi yupo ndani ya gari tayari akajaribu kuwaelewesha wapi kumbe nafasi yake walimpachika dogo mmoja mtoto wa kiongozi wa TFF gari likasepa wakampa nauli elf10 ya kurudia home haki ya mtu ailiwi niliamini siku ile kufika Airport wakakutana na ile crew ya yule mhispania wametoka hotelini tayari kwa kuanza safari kama zari yule mzungu akaingia ndani ya gari kuhakikisha wale aliowachagua kama ndio wenyewe yule mzungu ile kuwatazama wote akawaambia wale viongozi wa msafara kuna mtu mmoja ayupo apa sijamuona wakauliza nani uyo akawaambia martin ayupo apa kumbe yule mzungu alishamkubali dogo akawaambia apa atuondoki bila uyu mtu kuletwa apa dohh kwa aibu tumekaa kitaa tunasikia bi mkubwa wake anakuja na simu kumpa martin yule kiongozi alimwambia beba vitu vyako faster njoo airport kilichobaki ni historia dogo now ameshachukua na uraia wa Qatar kabisa
Hapo kwenye uraia tu ndio ujinga wake. Hana faida kwa nchi, amepunguza vipaji vya nchi; bora tu ange dhulumiwa.
 
Haya mauza uza ya hivi kwenye interviews huwa mara nyingi hayawakuti waliosoma Engineering, MD, Pharmacy na sciences nyingine, balaa liko kwa ngwini na biashara.
Nao sio muda itakuwa itakuwa kama biashara na sheria tu.
 
Huwezi kuniamini nitakachosema lakini ndiyo ukweli. Hata nikiwa na shida ya kazi namna gani bado kwenye mazingira kama haya wakati wa kusubiri interview nitakuwa najisikia vibaya sana kuona wenzangu anavyohangaika na kitu ambacho ni hewa. Kuna interview fulani nilienda nilipoangalia wahudhuriaji nikapiga story ya msahiliwa mmoja nikaonahuruma kweli kweli. Jamaa hata shati alilovaa aliazima kwa sababu hakuwa na shati lililo kwenye hali nzuri. Viatu maskini vilikuwa vimeisha lakini alijitahidi sana kuvingarisha kwa kiwi, da. Kweli dunia ni kubwa.
Duu,aisee.
 
Ilikuwa 2019 binamu yangu kaitwa interview huko serengeti mana alitoka jkt miaka miwili akaridi home.nikaforce kumpa chochote kumbe kadandia malori kafika hadi huko fresh.siku ya interview kaenda anaulizwa nani kakutuma uje?? Yan una mtu wako unaemfahamu hapa.?? Wewe ni kabila gani.? Jamaa hana la kusema mana yeye kaenda tu bila connection.basi alidunda...akarudi anatukana tu.

Nyingine hii hapa huzi tu sensa.....

Nimesema ngoja nikaombe kwa uncle nje ya mji kidogo vikindu tu hapa...la haula tumefanya interview fresh siku ya pili majibu bado lakin kuna watu tayar wanajua washapita na simu walipigiwa kama msiwe na wasiwasi mshapita......

Hii ndio tanzania yetu.
Inauma sana,kuna haja ya kubuni mfumo wa utoaji haki kwa wasahiliwa,japo sio rahisi.
 
bado naendelea sana kufuatilia huu uzi, Kwakweli kuna vitu vinaumiza sana.

Watu wa Takukuru mpo humu, watu wa TISS mpo humu na hawa wanaoteseka ni ndugu zenu jaribuni kusaidia jamii tabia hii ife mnusuru vizazi na vizazi.

Kuna haja sasa hizo mamlaka nilizozitaja kufanya kitu kwa kuanzia kwenye taasisi za Serikali kila nafasi zinapotangazwa na kuona nini kinatokea na ikibainika kuna shida basi hatua za haraka zichukuliwe.
Inauma sana mkuu.
 
Uko sahihi.

Ila dhana ya kuitegemea nchi/ serikali ndio itufanyie ndo inapunguza creativity kwa vijana wetu.

Inabidi tuone namna ya kutengeneza vijana watakawazo kufanya vilivyo ndani ya uwezo wao kuinuka, pasina kusubiri serikali.

We need creative generation.
Hili nalo ni neno,kuna huo uhitaji mapema sana ili kuokoa kizazi.
 
mtoa mada umenikumbusha dogo wangu wa kitaa Martin tangazi alivyofanyiwa na TFF..hii nchi ni ngumu sana kama mnakumbuka miaka ya uko nyuma kuanzia 2011 kulikuwa na mashindano ya Airtel rising star wanatafutwa vijana wenye vipaji then wanapelekwa Qatar kwenye Academy ya mpira wakachaguliwa watu kutoka kwenye shule mbalimbali za sekondary alafu ukafanyika mchujo bahati nzuri uwo mchujo aliyekuwa anausimamia ni mzungu kutoka Spain ukapigwa mchujo dogo akapità wakapelekwa karume wakaungana na wengine ili upigwe mchujo wa mwisho kitaifa then waliyopita moja kwa moja Qatar basi dogo kama bahat napo pale akatoboa wakawa wamechaguliwa watu kama 10 ndio waliofuzu wanaenda Qatar dogo akaanza kufuatlia mambo ya pasport kila kitu kikawa sawa sasa siku ya kuondoka waliambiwa wote waliochaguliwa wafike makao makuu ya TFF asubuhi saa1 dogo saa 12 tayari alishafika muda ulipofika wakawa wanaitwa majina then wanaingia kwenye coaster la TFF moja kwa moja Airport dogo anashangaa majina yameisha alafu yeye ajasikia jina lake akauliza mimi sijasikia jina langu na kwenye mchujo nilipita wakamuuliza unaitwa nani akawajibu akaambiwa mbona Martin tangazi yupo ndani ya gari tayari akajaribu kuwaelewesha wapi kumbe nafasi yake walimpachika dogo mmoja mtoto wa kiongozi wa TFF gari likasepa wakampa nauli elf10 ya kurudia home haki ya mtu ailiwi niliamini siku ile kufika Airport wakakutana na ile crew ya yule mhispania wametoka hotelini tayari kwa kuanza safari kama zari yule mzungu akaingia ndani ya gari kuhakikisha wale aliowachagua kama ndio wenyewe yule mzungu ile kuwatazama wote akawaambia wale viongozi wa msafara kuna mtu mmoja ayupo apa sijamuona wakauliza nani uyo akawaambia martin ayupo apa kumbe yule mzungu alishamkubali dogo akawaambia apa atuondoki bila uyu mtu kuletwa apa dohh kwa aibu tumekaa kitaa tunasikia bi mkubwa wake anakuja na simu kumpa martin yule kiongozi alimwambia beba vitu vyako faster njoo airport kilichobaki ni historia dogo now ameshachukua na uraia wa Qatar kabisa
Daa!Mungu alikuwa pamoja naye,hatakuja amsahau huyo mzungu,wazungu pamoja na madhaifu yao lakini wapo fair sana na hawana kona kona kama waswahili.
 
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Vijana tunapitia mengi ya kukatisha tamaa, lakini leo niwape machache ya vituko vya sahili nilivyowahi kuviona kwa macho yangu.

1. Tuliitwa kwenye usahili mikoa ya nyanda za juu kusini, basi kwa furaha na kujiamini nikapaki vitu huyooo nikafika siku moja kabla nikaripoti na nikakuta watu wengine, siku ya pili yake tukawahi sana tu,basi wakati tunaendelea kusubili wasahili wakafika na gari aina ya cruiser wakashuka kama saba hivi, sisi tukajua wote ni wasahili, lahaula kumbe wengine ni wasahiliwa kama sisi na tuligundua baada ya kuona wanakuja kukaa kwa wasahiliwa. Baada ya usahili matokeo nakuachia utabiri mwenyewe.

2. Tuliitwa kwenye usahili wa serikali basi wakati tunaendelea kusahiliwa basi kuna kijana sijui wa mkubwa gani akawa ameondoka eneo lile, basi unaambiwa alitafutwa balaa na mwisho wa siku matokeo yumo.

3. Kuna siku tunasubiri usahili, kuna vijana wakawa wanasema wameagizwa kuja hapo kama utani vile, aisee haikuwa utani matokeo yalitujulisha.

4. Tumefanya usahili, matokeo watu ambao hawakuwepo kwenye usahili ndio waajiliwa.

5.Umetoka umejiandaa na kile ulichosomea mfano mechanical engineering na vile vitu vinavyoendana na umejiandaa haswaa,unaingia wanaanza kukuzodoa,mara huyu aulize mambo ya demokrasi yaani ni ujinga tuu maadamu wakukere tu maana hawana mpango na wewe ni vile umekuja acha wapoteze tu muda, inakera acha tu.

Dah mambo ni mengi sana, ushauri wangu vijana msio na connection mkaze sana na kumuomba Mungu, lakini naamini kila kitu kinawezekana.

Kama una kisa ni ruhusa kuweka.
Hhhhh nimecheka sana
 
Daah..acha tu hii nchi ina mambo ya hovyo kabisa..kuna dogo alikua kipanga sana darasa la 7 enzi hizo..matokeo kuja jina halionekani asee.

Kumbe wahuni walishanunua jina wakapachika mtoto wao..dogo alikua kafaulu kwenda moshi tech.

Daah..dogo alilia sana..sema uzuri mzee wake kidogo naye alikua serikalini alipambana mpaka jina likaja na dogo akapata nafasi yake akaenda kusoma moshi tech sasa hivi dogo ni engineer anakula maisha tu.

Bongo bila pesa..au konekisheni haki yako unaweza kuiona inaondoka mbele yako hivi hivi.

#MaendeleoHayanaChama
Bongo bila pesa au connection utalia na kusaga meno,labda iwe bahati yako tu.
 
Pilot
Aircraft engineer
Marine and nautical engineer
Drilling Engineer
Well completion engineer
Fishing engineer
Mining Engineer
Robotic and Automation engineer.
Cyber security expert.
Software developer.
Artificial Intelligence expert.
Reliability and Mechanical Engineer.
ROV operator.
Automation engineer.
Instrumentatio engineer
Electric Engineer.
Mechanical Engineer.
Civil Engineer
nk, nk, nk.

Taifa halitoi direction kwa vijana wasome nini, matokeo yake vijana huishia kutia huruma na kunyenyekea wapumbavu.
Iyo marine and nautical engineer kwa hapa tz ni chuo kipi wanatoa??
 
Back
Top Bottom