jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Daah..acha tu hii nchi ina mambo ya hovyo kabisa..kuna dogo alikua kipanga sana darasa la 7 enzi hizo..matokeo kuja jina halionekani asee.mtoa mada umenikumbusha dogo wangu wa kitaa Martin tangazi alivyofanyiwa na TFF..hii nchi ni ngumu sana kama mnakumbuka miaka ya uko nyuma kuanzia 2011 kulikuwa na mashindano ya Airtel rising star wanatafutwa vijana wenye vipaji then wanapelekwa Qatar kwenye Academy ya mpira wakachaguliwa watu kutoka kwenye shule mbalimbali za sekondary alafu ukafanyika mchujo bahati nzuri uwo mchujo aliyekuwa anausimamia ni mzungu kutoka Spain ukapigwa mchujo dogo akapità wakapelekwa karume wakaungana na wengine ili upigwe mchujo wa mwisho kitaifa then waliyopita moja kwa moja Qatar basi dogo kama bahat napo pale akatoboa wakawa wamechaguliwa watu kama 10 ndio waliofuzu wanaenda Qatar dogo akaanza kufuatlia mambo ya pasport kila kitu kikawa sawa sasa siku ya kuondoka waliambiwa wote waliochaguliwa wafike makao makuu ya TFF asubuhi saa1 dogo saa 12 tayari alishafika muda ulipofika wakawa wanaitwa majina then wanaingia kwenye coaster la TFF moja kwa moja Airport dogo anashangaa majina yameisha alafu yeye ajasikia jina lake akauliza mimi sijasikia jina langu na kwenye mchujo nilipita wakamuuliza unaitwa nani akawajibu akaambiwa mbona Martin tangazi yupo ndani ya gari tayari akajaribu kuwaelewesha wapi kumbe nafasi yake walimpachika dogo mmoja mtoto wa kiongozi wa TFF gari likasepa wakampa nauli elf10 ya kurudia home haki ya mtu ailiwi niliamini siku ile kufika Airport wakakutana na ile crew ya yule mhispania wametoka hotelini tayari kwa kuanza safari kama zari yule mzungu akaingia ndani ya gari kuhakikisha wale aliowachagua kama ndio wenyewe yule mzungu ile kuwatazama wote akawaambia wale viongozi wa msafara kuna mtu mmoja ayupo apa sijamuona wakauliza nani uyo akawaambia martin ayupo apa kumbe yule mzungu alishamkubali dogo akawaambia apa atuondoki bila uyu mtu kuletwa apa dohh kwa aibu tumekaa kitaa tunasikia bi mkubwa wake anakuja na simu kumpa martin yule kiongozi alimwambia beba vitu vyako faster njoo airport kilichobaki ni historia dogo now ameshachukua na uraia wa Qatar kabisa
Kumbe wahuni walishanunua jina wakapachika mtoto wao..dogo alikua kafaulu kwenda moshi tech.
Daah..dogo alilia sana..sema uzuri mzee wake kidogo naye alikua serikalini alipambana mpaka jina likaja na dogo akapata nafasi yake akaenda kusoma moshi tech sasa hivi dogo ni engineer anakula maisha tu.
Bongo bila pesa..au konekisheni haki yako unaweza kuiona inaondoka mbele yako hivi hivi.
#MaendeleoHayanaChama