Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

Mimi sina cv ,sina sponsor ila namshukuru mwenyezi mungu yaani kila interview niliyowahi kufanya nilichaguliwa...

Nilishafanya interview kama tatu na kuna baadhi ya interview sikuwa na sifa kabisa ila inatokea tu wamenipitisha.

Sina mengi zaidi ya kumshukuru sana mungu muweza wa yote.
Ina maana hukuwa unaridhika na kazi ulizokuwa unapata hivyo hata ukifaulu interview ya kwanza una-apply tena kazi nyingine, na nyingine?
 
Hakuna raha kama unaenda kwenye saili unajua umepita ila unaamua kujichanganya na walala hoi mnakazana kupeana possible huku ukisubiri zamu yako ifike uende hakuna wanachojua kinachoendelea
Huwezi kuniamini nitakachosema lakini ndiyo ukweli. Hata nikiwa na shida ya kazi namna gani bado kwenye mazingira kama haya wakati wa kusubiri interview nitakuwa najisikia vibaya sana kuona wenzangu anavyohangaika na kitu ambacho ni hewa. Kuna interview fulani nilienda nilipoangalia wahudhuriaji nikapiga story ya msahiliwa mmoja nikaonahuruma kweli kweli. Jamaa hata shati alilovaa aliazima kwa sababu hakuwa na shati lililo kwenye hali nzuri. Viatu maskini vilikuwa vimeisha lakini alijitahidi sana kuvingarisha kwa kiwi, da. Kweli dunia ni kubwa.
 
Kizazi cha vijana cha sasa ni magoigoi wala siwaonei huruma. Mijadala yao yote ni ''jinsi ya kula tunda kimasihara'' au Yanga na Simba. Kwa nini hawaongozi kudai mabadiliko ya mfumo na serikali kuwajibika. Ndiyo maana hata serikali inawadharau na kuwaita kwenye interview eg watu elfu tano wakati nafasi zinazotakiwa ni mbili tu.
Vijana WA sasa hivi wako radhi kuandamana kudai haki za zali au diamond na sio kudai haki zao za Ajira.

Sasa hivi huwa hatasiumii kuona kijana WA kitanzania anaumia

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe 100%. Ila kadiri siku zinavyosonga mbele ndiyo mtaani kunazidi kufurika na itafikia hatua watajielewa.
 
Pilot
Aircraft engineer
Marine and nautical engineer
Drilling Engineer
Well completion engineer
Fishing engineer
Mining Engineer
Robotic and Automation engineer.
Cyber security expert.
Software developer.
Artificial Intelligence expert.
Reliability and Mechanical Engineer.
ROV operator.
Automation engineer.
Instrumentatio engineer
Electric Engineer.
Mechanical Engineer.
Civil Engineer
nk, nk, nk.

Taifa halitoi direction kwa vijana wasome nini, matokeo yake vijana huishia kutia huruma na kunyenyekea wapumbavu.
Una umri juu ya miaka 55 mzee wangu?
 
2008 kuna jamaa tulikutana kwenye usaili wa JKT . Dogo kwa muonekano alitokea familia flani ivi duni afu za kidini sana mana alikuwa mnyenyekevu mpaka anaboa . Mimi tayari uhakika wa kupita ulikuwepo japo sikupenda kuwa mjeshi hivyo nilifata maelekezo tu.

Basi dogo umefika muda wakuhojiwa akatumwa sigara ile anarudi anaambiwa kachelewa dogo alilia mpaka makamasi kumbe ashaliwa pesa kibao toka wilayani then mkoani anakaziwa kijinga afu bosi mmoja akamwambia amepunguwa urefu fut3 wakati toka mwanzo ashapimwa na akapita. Dah! Ile hali ilinigusa sana nikajaribu kumshauri na kumpa moyo ndo akanambia kuwa mama yake kawekeza Sana ili ye aende jeshi mpaka kauza baadhi ya vitu vyake kuweka mazingira sawa. Basi nilichokifanya nikaongea na wakubwa walotamani niende jeshi kuwa me sivutiwi kwenda jeshi ila nafasi yangu kuna mtoto wamsaidie, basi wakanielewa wakampitisha ,aisee dogo hajaniangusha kapambana mpaka akapata nafasi na leo ni miongoni mwa connection zangu zinazonifanya nivimbe mjini apa.

My point : kama ipo ipo tu msikate tamaa ukiona umekosa ujue sio liziki yako ila kama ni liziki yako itakuja kwa njia yyt ile
Mwanangu kwa uungwana ulioufanya utalipwa pakubwa na hutoamini. Hongera sana kwa kuwa na moyo wa ubinadamu.
 
Huwezi kuniamini nitakachosema lakini ndiyo ukweli. Hata nikiwa na shida ya kazi namna gani bado kwenye mazingira kama haya wakati wa kusubiri interview nitakuwa najisikia vibaya sana kuona wenzangu anavyohangaika na kitu ambacho ni hewa. Kuna interview fulani nilienda nilipoangalia wahudhuriaji nikapiga story ya msahiliwa mmoja nikaonahuruma kweli kweli. Jamaa hata shati alilovaa aliazima kwa sababu hakuwa na shati lililo kwenye hali nzuri. Viatu maskini vilikuwa vimeisha lakini alijitahidi sana kuvingarisha kwa kiwi, da. Kweli dunia ni kubwa.
So, wewe siyo mlala hoi?

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom