Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

mtoa mada umenikumbusha dogo wangu wa kitaa Martin tangazi alivyofanyiwa na TFF..hii nchi ni ngumu sana kama mnakumbuka miaka ya uko nyuma kuanzia 2011 kulikuwa na mashindano ya Airtel rising star wanatafutwa vijana wenye vipaji then wanapelekwa Qatar kwenye Academy ya mpira wakachaguliwa watu kutoka kwenye shule mbalimbali za sekondary alafu ukafanyika mchujo bahati nzuri uwo mchujo aliyekuwa anausimamia ni mzungu kutoka Spain ukapigwa mchujo dogo akapità wakapelekwa karume wakaungana na wengine ili upigwe mchujo wa mwisho kitaifa then waliyopita moja kwa moja Qatar basi dogo kama bahat napo pale akatoboa wakawa wamechaguliwa watu kama 10 ndio waliofuzu wanaenda Qatar dogo akaanza kufuatlia mambo ya pasport kila kitu kikawa sawa sasa siku ya kuondoka waliambiwa wote waliochaguliwa wafike makao makuu ya TFF asubuhi saa1 dogo saa 12 tayari alishafika muda ulipofika wakawa wanaitwa majina then wanaingia kwenye coaster la TFF moja kwa moja Airport dogo anashangaa majina yameisha alafu yeye ajasikia jina lake akauliza mimi sijasikia jina langu na kwenye mchujo nilipita wakamuuliza unaitwa nani akawajibu akaambiwa mbona Martin tangazi yupo ndani ya gari tayari akajaribu kuwaelewesha wapi kumbe nafasi yake walimpachika dogo mmoja mtoto wa kiongozi wa TFF gari likasepa wakampa nauli elf10 ya kurudia home haki ya mtu ailiwi niliamini siku ile kufika Airport wakakutana na ile crew ya yule mhispania wametoka hotelini tayari kwa kuanza safari kama zari yule mzungu akaingia ndani ya gari kuhakikisha wale aliowachagua kama ndio wenyewe yule mzungu ile kuwatazama wote akawaambia wale viongozi wa msafara kuna mtu mmoja ayupo apa sijamuona wakauliza nani uyo akawaambia martin ayupo apa kumbe yule mzungu alishamkubali dogo akawaambia apa atuondoki bila uyu mtu kuletwa apa dohh kwa aibu tumekaa kitaa tunasikia bi mkubwa wake anakuja na simu kumpa martin yule kiongozi alimwambia beba vitu vyako faster njoo airport kilichobaki ni historia dogo now ameshachukua na uraia wa Qatar kabisa
Daah..acha tu hii nchi ina mambo ya hovyo kabisa..kuna dogo alikua kipanga sana darasa la 7 enzi hizo..matokeo kuja jina halionekani asee.

Kumbe wahuni walishanunua jina wakapachika mtoto wao..dogo alikua kafaulu kwenda moshi tech.

Daah..dogo alilia sana..sema uzuri mzee wake kidogo naye alikua serikalini alipambana mpaka jina likaja na dogo akapata nafasi yake akaenda kusoma moshi tech sasa hivi dogo ni engineer anakula maisha tu.

Bongo bila pesa..au konekisheni haki yako unaweza kuiona inaondoka mbele yako hivi hivi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hizi ndizo kazi ukisomea zinakutafuta na sio kuzitafuta huko ulimwenguni. Vijana someni hizo kozi hapo na muajirike duniani maana ndio fami zenyewe hizo.
Nani kakudanganya au kukuaminisha mkuu? Kwa taarifa yako tupo wengi Sana humu ndani wenye Dani hizo[emoji115] na bado tupo tu mtaani. Mpaka Kuna Uzi mmoja kule jukwaa la kazi na ajira unahusu kupeana koneksheni kwa fani za engineering na kila mtu analia mkuu.
 
Daah..acha tu hii nchi ina mambo ya hovyo kabisa..kuna dogo alikua kipanga sana darasa la 7 enzi hizo..matokeo kuja jina halionekani asee.

Kumbe wahuni walishanunua jina wakapachika mtoto wao..dogo alikua kafaulu kwenda moshi tech.

Daah..dogo alilia sana..sema uzuri mzee wake kidogo naye alikua serikalini alipambana mpaka jina likaja na dogo akapata nafasi yake akaenda kusoma moshi tech sasa hivi dogo ni engineer anakula maisha tu.

Bongo bila pesa..au konekisheni haki yako unaweza kuiona inaondoka mbele yako hivi hivi.

#MaendeleoHayanaChama
Aaaah uongo bhana, mimi mbona sijawahi pata kazi kwa connection wala kunyang'anywa haki yangu?
 
Kwa uzoefu wangu katika saili nyingi ambazo nimesaili vijana, Taifa hili tuna changamoto kubwa sana ya uelewa wa mambo unakuta mtu kasoma special school na ana Bachelor ya Computer Engineering unamuuliza swali what is Operating System anabaki anashangaa akitoka njee anasema wana watu wao, Binafsi nimeapa nilipata kazi kwa haki na nitatenda haki siku zote japo majaribu ni Mengi na Mikuki ni Mingi, ila kuna vijana wana ufaulu mzuri ila interview wanachemka sana, sikatai uwepo wa upendeleo katika baadhi ya taasisi mbalimbali lakini rai yangu kwa vijana fanya maandalizi vizuri kafanye usaili notion za kusingizia watu wamepangwa achana nazo.

Sent from my SM-N950N using JamiiForums mobile app
Acha kuandika hivi,,,,Kuna mabaya mengi Sana yanaendelea wakati wa usaili na for sure hata officen kwako yapo,,,,ikiwa huyatendi wewe basi Kuna wenzio
 
Siji kuomba kazi taasisi binafsi Mimi nakomaa na ajila portal ukitaka kupoteza mda wako na pesa omba hizi taasisi.

Arusha city college mungu anawaona choma nauli mbeya to arusha na maladhi juu ila ata feed back amna dah maisha aya kama laki mbili imekatika. Mungu mwm ipo siku yangu inakuja.
Kwa uandishi wako brother jipange. Mbali na connection, lugha pia muhimu hasa kuandika
 
Juzi kati hapa kwenye mwezi wa 4 hivi mwaka huu, tuliitwa interview Taifa gas,walikua wanataka Business Development managers wawili.uzuri kwenye interview tulikua wawili na nafasi zinazotakiwa ni mbili pia.ila cha ajabu tukasikia wameajiri watu wengine tofauti na sisi tuliofanyiwa usaili.nikabaki kushangaa tu kwa kilichotokea.
Ila uzuri mmoja wa hizi kazi za kubebana madhara yake huwa yanaonekana mapema kabisa, efficiency ya kazi huwa ni zero kwenye taasisi husika.
 
bado naendelea sana kufuatilia huu uzi, Kwakweli kuna vitu vinaumiza sana.

Watu wa Takukuru mpo humu, watu wa TISS mpo humu na hawa wanaoteseka ni ndugu zenu jaribuni kusaidia jamii tabia hii ife mnusuru vizazi na vizazi.

Kuna haja sasa hizo mamlaka nilizozitaja kufanya kitu kwa kuanzia kwenye taasisi za Serikali kila nafasi zinapotangazwa na kuona nini kinatokea na ikibainika kuna shida basi hatua za haraka zichukuliwe.
Takukuru, tiss hawana matumbo, hawana mahawara, hawahitaji kundesha VX V8 na BMW X6 0km??
Hapa ni Afrika, tumbo kwanza mengine baadae!

#WapiKamandaMbowe
 
Unanikumbusha nikiwa nafanyiwa interview ya mtandao mmoja wa simu somewhere in Tz..tuko watu 14 na wanahitajika wawili....sasa wahuni washatoa handout kwa muhuni wao ya ile kazi inataka nini na kipi cha msingi kwenye ile kazi...basi naona nice boys wamekuja kwenye interview na mademu zao na ma pamphlet makubwa balaaa kuhusu huo mtandao...mi nikasema hiiiiiiii......basi full kumeza madude hadi ya kiuchumi..nikawaonea huruma ila ndo venye sikua na chakufanya kuwasaidia..maana survival for the fittest (maana usipomla simba haimaanishi kuwa yeye hatakukula eti kwakua umekua nice kwake)..... interview kuisha tu..ata ghetto sijafika kazi iko mkononi......from that time sijawahi kuomba kazi bila kuwa na connection..maana kinachoendelea huko kwenye ma interview ata shetani haungi mkono
 
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Vijana tunapitia mengi ya kukatisha tamaa, lakini leo niwape machache ya vituko vya sahili nilivyowahi kuviona kwa macho yangu.

1. Tuliitwa kwenye usahili mikoa ya nyanda za juu kusini, basi kwa furaha na kujiamini nikapaki vitu huyooo nikafika siku moja kabla nikaripoti na nikakuta watu wengine, siku ya pili yake tukawahi sana tu,basi wakati tunaendelea kusubili wasahili wakafika na gari aina ya cruiser wakashuka kama saba hivi, sisi tukajua wote ni wasahili, lahaula kumbe wengine ni wasahiliwa kama sisi na tuligundua baada ya kuona wanakuja kukaa kwa wasahiliwa. Baada ya usahili matokeo nakuachia utabiri mwenyewe.

2. Tuliitwa kwenye usahili wa serikali basi wakati tunaendelea kusahiliwa basi kuna kijana sijui wa mkubwa gani akawa ameondoka eneo lile, basi unaambiwa alitafutwa balaa na mwisho wa siku matokeo yumo.

3. Kuna siku tunasubiri usahili, kuna vijana wakawa wanasema wameagizwa kuja hapo kama utani vile, aisee haikuwa utani matokeo yalitujulisha.

4. Tumefanya usahili, matokeo watu ambao hawakuwepo kwenye usahili ndio waajiliwa.

5.Umetoka umejiandaa na kile ulichosomea mfano mechanical engineering na vile vitu vinavyoendana na umejiandaa haswaa,unaingia wanaanza kukuzodoa,mara huyu aulize mambo ya demokrasi yaani ni ujinga tuu maadamu wakukere tu maana hawana mpango na wewe ni vile umekuja acha wapoteze tu muda, inakera acha tu.

Dah mambo ni mengi sana, ushauri wangu vijana msio na connection mkaze sana na kumuomba Mungu, lakini naamini kila kitu kinawezekana.

Kama una kisa ni ruhusa kuweka.
Visa ni vingi sana mkuu acha tu
 
Unanikumbusha nikiwa nafanyiwa interview ya mtandao mmoja wa simu somewhere in Tz..tuko watu 14 na wanahitajika wawili....sasa wahuni washatoa handout kwa muhuni wao ya ile kazi inataka nini na kipi cha msingi kwenye ile kazi...basi naona nice boys wamekuja kwenye interview na mademu zao na ma pamphlet makubwa balaaa kuhusu huo mtandao...mi nikasema hiiiiiiii......basi full kumeza madude hadi ya kiuchumi..nikawaonea huruma ila ndo venye sikua na chakufanya kuwasaidia..maana survival for the fittest (maana usipomla simba haimaanishi kuwa yeye hatakukula eti kwakua umekua nice kwake)..... interview kuisha tu..ata ghetto sijafika kazi iko mkononi......from that time sijawahi kuomba kazi bila kuwa na connection..maana kinachoendelea huko kwenye ma interview ata shetani haungi mkono
Mkuu kwa hiyo ulikuwa na connection hapo?
 
dah nasoma comments, dah kuna watu wana dhambi sana na inahuzunisha sana.

Hivi binti unajisikiaji kutoa uchi wako ili upate kazi? na wewe mwanaume unajisikiaji kumfanya mtoto wa mwenzio ili umpe kazi bila kupitia vigezo?, unajisikiaje na binti yako akifanyiwa hivyo tena analiwa tigo ili apewe kazi is that fair? INASIKITISHA SANA.

Kama umeita watu kwa ajili ya interview, ni vyema ukawafanyia usaili woote na kuchagua kulingana na vigezo sio hizi blah blah na kujuana, huu ni upumbavu na mambo ya kizamani saaana shenzi kabisa.

Halafu majitu ya hivi yanakwenda msikitini na kanisani full time.
Huku makanisani ndio hasa wachawi wanapojificha kwenye chaka la UKRISTO.

Unaweza kukuta ASKOFU MCHAWI NA AMEVAA JIMSALABA KUBWA.
 
Kwa uzoefu wangu katika saili nyingi ambazo nimesaili vijana, Taifa hili tuna changamoto kubwa sana ya uelewa wa mambo unakuta mtu kasoma special school na ana Bachelor ya Computer Engineering unamuuliza swali what is Operating System anabaki anashangaa akitoka njee anasema wana watu wao, Binafsi nimeapa nilipata kazi kwa haki na nitatenda haki siku zote japo majaribu ni Mengi na Mikuki ni Mingi, ila kuna vijana wana ufaulu mzuri ila interview wanachemka sana, sikatai uwepo wa upendeleo katika baadhi ya taasisi mbalimbali lakini rai yangu kwa vijana fanya maandalizi vizuri kafanye usaili notion za kusingizia watu wamepangwa achana nazo.

Sent from my SM-N950N using JamiiForums mobile app
Tatizo lenu nyie interviewers mnauliza maswali ya KUKARIRI kama kasuku.

MFANO: Nyerere alizaliwa mwaka gani?Bwawa la mtera lilizinduliwa na nani?

Total Bullshit. Uliza maswali ya utendaji kazi. Practical question.

Some questions are too silly with no academic value.

Mbadilike. Acheni mentality za kinjekitile.
 
Niliwahi kuhudhuria interview moja miaka ya nyuma. Sasa nilipofika eneo la interview nilibahatika kubaini ya kwamba kuna watu tayari walishachaguliwa.

Sisi kumbe ilikuwa ni danganya toto. Nilishikwa na hasira sana.
Zamu yangu ilipofika nikaitwa kwenye panel kwa ajili ya kuulizwa maswali.

Baada ya utambulisho niliwachana live wale panelist. Niliwaambia hv nakumbuka "Samahani ndugu zangu nimekuja kimakosa hapa sikupaswa kuwepo kwasababu tayari mna watu wenu mifukoni" kisha nikatoka kwa speed. Kugeuka nyuma nikaona kuna karani amekaza mwendo kunifuata akiniita nikakaza mwendo nikapotelea kusikojilikana mpaka leo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom