Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

2008 kuna jamaa tulikutana kwenye usaili wa JKT . Dogo kwa muonekano alitokea familia flani ivi duni afu za kidini sana mana alikuwa mnyenyekevu mpaka anaboa . Mimi tayari uhakika wa kupita ulikuwepo japo sikupenda kuwa mjeshi hivyo nilifata maelekezo tu.

Basi dogo umefika muda wakuhojiwa akatumwa sigara ile anarudi anaambiwa kachelewa dogo alilia mpaka makamasi kumbe ashaliwa pesa kibao toka wilayani then mkoani anakaziwa kijinga afu bosi mmoja akamwambia amepunguwa urefu fut3 wakati toka mwanzo ashapimwa na akapita. Dah! Ile hali ilinigusa sana nikajaribu kumshauri na kumpa moyo ndo akanambia kuwa mama yake kawekeza Sana ili ye aende jeshi mpaka kauza baadhi ya vitu vyake kuweka mazingira sawa. Basi nilichokifanya nikaongea na wakubwa walotamani niende jeshi kuwa me sivutiwi kwenda jeshi ila nafasi yangu kuna mtoto wamsaidie, basi wakanielewa wakampitisha ,aisee dogo hajaniangusha kapambana mpaka akapata nafasi na leo ni miongoni mwa connection zangu zinazonifanya nivimbe mjini apa.

My point : kama ipo ipo tu msikate tamaa ukiona umekosa ujue sio liziki yako ila kama ni liziki yako itakuja kwa njia yyt ile
 
Aisee hongera sana kwa kumhurumia,wenye mioyo hiyo ni wachache.
 
🤣🤣🤣🙏🙏 hadi usangoma ni connection muulize Mshana Jr

Anyways kuna interview jamaa walienda mkoani basi kabla ya chochote wakaambiwa wapashe misuli moto kidogo wakimbie kama umbali wa kama viwanja viwili vya mpira na kurudi. Basi unaambiwa wakati wa kurudi wakakuta wale wasaili wameweka kamba mithili ya watu wa riadha so wasailiwa walio wahi kuingia kwenye kamba ndio wakawa wameshinda usaili hivyo
 

Hahaha, mkuu japo sio mazuri, ila komenti yako imenichekesha sana.
 
ile tumemaliza chuo tu mimi na mwanangu milandu tukapewa mchongo na sista..sista yeye kasoma masomo ya ras simba tu mixer na vyuo vya mtaani..sisi tuna gamba, NGO ipo mikocheni ..kuna engineer pale ndo kampa mchongo..sista hakua hata na cv tukasema tumchoree cv fastaa asbuhi ya kuzugia,maana sisi zetu zipo zimeshiba.. tumeingia tumepiga sana yai baba..hahaha jioni me na mwanangu tumekalia kuti kavu sista huyo kapita kisa engineer ambaye pia panelist anamuelewa sista
 
Angalau hao walikua fair.
 
🤣🤣Mkafa na cv zenu,mambo haya yanachekesha na kuhudhunisha kwa pamoja.
 
Kaka yani umeenda kufanya interview ya public relations halafu kabla huja ingia kwenye oral uambiwe pasheni misuli kidogo kisha mrudi halafu wakati wakurudi ghafla wasaili wanasema walio rudi KWANZA ndio wameshinda usaili hiyo unaita fair?
Unaweza ishiwa nguvu,daa!.
 
Mm siku hiz naenda kuoga maji ya bahari Kwa muda wa mwezi alafu ntaanza kuomba ajira rasmi 😆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…