Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Hayo ya kwa Kopa si umeona open space la kumwaga.

Manjunju kwenye huo Mbuyu manyau nyau alihangaika na huo mbuyu akatoa madude akasema ni chuma ulete, kuna sehemu kuna geti kubwa kila anayepita anachajiwa 200 na mapato ndiyo yanaangukia hapo.
 
Same situation happened to me,nikiwa kwenye daladala,nikaodondoshea ndani ndo salama yangu,sitoi simu maeneo yale
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kujichunguza sehem nyet!!!
 
Nikiwa maeneo fulani nikaitwa baa kufika nikaagiza soda baada ya muda washkaji wakajua natokea mwananyamala, wakaniambia umeishi Mwananyamala halafu haunywi pombe?

Nikajibu ndiyo.

Wala hauvuti sigara wala bangi?

Nikajibu ndiyo.

Mshkaji akamalizia 'Ms.nge unajifanyisha siyo kweli'
 
Hayo ya kwa Kopa si umeona open space la kumwaga.

Manjunju kwenye huo Mbuyu manyau nyau alihangaika na huo mbuyu akatoa madude akasema ni chuma ulete, kuna sehemu kuna geti kubwa kila anayepita anachajiwa 200 na mapato ndiyo yanaangukia hapo.
Ule mbuyu uacheni kama ulivyo... Yule nesi aliyepoteaga alipatikana pale
 
Ahhha na kuna jamaa aliwahi kukamatwa sema location sikumbuki vzur,yeye alikuwa anakuunganisha dstv,azam ,startmies,nk kwa Pamoja nadhani alkuwa anachaji bk 5 pekee
Huyu anapatikana maeneo ya mwananyamala kwa njunju.. Jamaa alikuwa genius..! Yaani hao jamaa wa dstv na star times ilibd wamuulize kwanza aliwezaje wezaje kutoa huduma mixer kwa raia zaidi ya 2000 bila ya kugundulika..! Alitumia sayansi gani..! [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
mshana jr mipango ya safar bado ipo sana mwananyamala.
Kundi kubwa la vijana wapo Qatar kwenye ujenz wa viwanja vya mpira kwa ajili ya World Cup, wengine wanaenda sana ULAYA kwa ajili ya masuala ya sarakasi,
Michongo ya fake documents naona bado ipo sana,
Taarifa za safar huwq zinakuja maskani tu watu wanaambiwa na kupewa conditions za safari.
Kuna jamaa yangu alipata safar ya china,akatengeneza documents zote fake kasoro PASSPORT tu,cheti chake kinaonesha ana mafunzo ya upish wakat hajasomea na hajui kupika kama anavyojinasibu,akala shavu la kwenda China,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Amerud namuona na docs zake anaandaa safar ya kwenda Scandinavian countries.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…