Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Makaburini kwa mwananyamala zipo sehem mbili maarufu.
1.Makaburi ya Mwananyamala KWA KOPA, ndo happ kwenye picha ambapo watu hupita na kutokea mwananyamala hospital
2.Mwananyamala Kwa Manjunju kuna mbuyu mkubwaaa na makaburi "ingawa kwa sasa yameshajaa".
Vibaka wengi wapo kwa MANJUNJU
Hayo ya kwa Kopa si umeona open space la kumwaga.

Manjunju kwenye huo Mbuyu manyau nyau alihangaika na huo mbuyu akatoa madude akasema ni chuma ulete, kuna sehemu kuna geti kubwa kila anayepita anachajiwa 200 na mapato ndiyo yanaangukia hapo.
 
Umenikumbusha hiyo ya maeno hatari kwa wizi wa simu miaka kama mi4 iliyopita hivi mida ya sa 10 alfajiri tunarudi toka njenje tupo kwenye gari kwa mama zakaria tunamshusha rafiki yetu mmoja nimeshika simu nachat kioo nimeshusha hata mtu alipotokea sijamuona anataka kukwapua simu yangu nilichofanya niliidindosha chini ndio salama yangu bila hivi simu ilikua inaenda
Same situation happened to me,nikiwa kwenye daladala,nikaodondoshea ndani ndo salama yangu,sitoi simu maeneo yale
 
Nakumbuka mwaka 2009,nililala guest fulani ipo maeneo karibu na mwananyamala magengeni.Naamka asbh nakuta suruali yangu haipo ndani wakati niliiweka kwenye kiti pembeni kabla sijalala.Kuchunguza dirishani nikakuta kuna tobo limetengenezwa.Nikajua tayari nishapigwa,nikatoka nje ya ile guest ili kujua ilipo nguo yangu,nikaikuta nje ya uzio imetupwa.Kusachi mfukoni nikakuta atm card zangu, ila hela hakuna,nilikuwa nimeacha mia tano ya noti.Nilishukuru sana kwani kabla sijalala usiku nilijihami kwa kuficha hela zote chini ya mto.Ila nilijiuliza hawa jamaa walipuliza dawa ya usingizi usiku ama,maana sikushtuka na wakaweza kuitungua suruali kwa uzuri hadi kutimiza mission zao,ilibidi hadi nijichunguze sehemu nyeti kama hawajafanya yao,maana usingizi ulikuwa mzito sana.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kujichunguza sehem nyet!!!
 
Nikiwa maeneo fulani nikaitwa baa kufika nikaagiza soda baada ya muda washkaji wakajua natokea mwananyamala, wakaniambia umeishi Mwananyamala halafu haunywi pombe?

Nikajibu ndiyo.

Wala hauvuti sigara wala bangi?

Nikajibu ndiyo.

Mshkaji akamalizia 'Ms.nge unajifanyisha siyo kweli'
 
Hayo ya kwa Kopa si umeona open space la kumwaga.

Manjunju kwenye huo Mbuyu manyau nyau alihangaika na huo mbuyu akatoa madude akasema ni chuma ulete, kuna sehemu kuna geti kubwa kila anayepita anachajiwa 200 na mapato ndiyo yanaangukia hapo.
Ule mbuyu uacheni kama ulivyo... Yule nesi aliyepoteaga alipatikana pale
 
Ahhha na kuna jamaa aliwahi kukamatwa sema location sikumbuki vzur,yeye alikuwa anakuunganisha dstv,azam ,startmies,nk kwa Pamoja nadhani alkuwa anachaji bk 5 pekee
Huyu anapatikana maeneo ya mwananyamala kwa njunju.. Jamaa alikuwa genius..! Yaani hao jamaa wa dstv na star times ilibd wamuulize kwanza aliwezaje wezaje kutoa huduma mixer kwa raia zaidi ya 2000 bila ya kugundulika..! Alitumia sayansi gani..! [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
mshana jr mipango ya safar bado ipo sana mwananyamala.
Kundi kubwa la vijana wapo Qatar kwenye ujenz wa viwanja vya mpira kwa ajili ya World Cup, wengine wanaenda sana ULAYA kwa ajili ya masuala ya sarakasi,
Michongo ya fake documents naona bado ipo sana,
Taarifa za safar huwq zinakuja maskani tu watu wanaambiwa na kupewa conditions za safari.
Kuna jamaa yangu alipata safar ya china,akatengeneza documents zote fake kasoro PASSPORT tu,cheti chake kinaonesha ana mafunzo ya upish wakat hajasomea na hajui kupika kama anavyojinasibu,akala shavu la kwenda China,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Amerud namuona na docs zake anaandaa safar ya kwenda Scandinavian countries.
 
Back
Top Bottom