Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125]
Nacheka kama mwehu humu dalaldalani
 
Kile kijiwe kuna akina Bedui, Beka, kuna mzee mmoja anafanana na Mizengo Pinda, mzee Jose, Kobelo sijui, kuna mzee mmoja mpemba ana matusi sana nk
Bedui alikuwa anapiga sana draft. Anafahamika kwenye vijiwe vyote vya draft kuanzia Mwananyamala, Temeke, Chang'ombe mpaka Keko.

Alikuja kwenye kijiwe chetu siku moja akatupiga sana, halafu alivyo mjinga akasema game inayofuata anatoa kete moja. Mjinga sana Bedui
 
Ndeka ameshafariki bana toka mwaka 2012
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Pale maeneo ya msufini palikuwa na uwanja mkubwa sana unatumika ktk maswala mbali mbali km siasa, maulid ( madras)...jioni unakuta kuna cha ndimu gemu za ligi ya mbuzi unakuta vibinti micharuko na wakina mama na watoto mgongoni unasikia "usiniumizie uyoooo" hizo ligi wanacheza watu na ndevu zao ila mpira wa cha ndimu (sio gozi) hapa ndio alipotokea bondia CHEKA alikuwa golikipa kipaji chake cha ngumu kilikuja kuoneka kinondoni mahakamani(kambangwa) kuna kitu kinaitwa MTU BEE....gemu zikiisha huo uwanja unageuka sehem ya biashara samaki, vitumbua, chai n.k....biashara zikimalizia wanaingia wazee wa kazi NGETA hapo kuna kila aina ya wizi usije kukatisha eneo ilo msufini kuanzia saa tano usku UMEKWISHA
 
Kete moja? Yule jamaa alikua anakutolea hata kete nne.

Mwenzake Mangolele ndiyo alikua ametengeneza draft la ngozi anatembea nalo yeye moto mnauwasha popote.
 
Niko naandika thread kukuhusu yenye udadavuzi murua kukuhusu,ulivyosaidia wengi(nikiwemo),na kasoro chache kidogo, na ukweli nilioubaini.
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Nitakuwa nakufahamu
Chama la wana. Mwananyamala ina wadau wengi sana apa jamii forum. Haha haha unanikumbusha kuna mshkaji alikuwa anakaa mwananyamala alafu akawa anawazuga masela wake pale Makongo Secondary kwamba anakaa kijitonyama, sasa siku iyo tunatoka pindi la tuition pale mapambano kalibia na Nakiette pharmacy wakatokea makonda wa daladala wa kitaa kwao na anko yake teja pale mwenge akaanza kumuita ankoo chukua izi kandambili peleka apo mwananyamala nyumbani sasa washkaji zake ambao walikuwa wakishua walicheka mbaya kwamba jamaaa ana anko yake TEJA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…