Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Kete moja? Yule jamaa alikua anakutolea hata kete nne.

Mwenzake Mangolele ndiyo alikua ametengeneza draft la ngozi anatembea nalo yeye moto mnauwasha popote.
Ila sometime alikuwa anashinda kwa maneno. Ana maneno ya karaha sana.

Kuna Mzee wetu mmoja tulikuwa tunamuaminia sana halafu akapigwa. Fikiria wengine kisaikolojia tuliathirika kiasi gani!
 
Me nimezaliwa A nimesoma mwananyamala B ile ya mwalimu Ndeka ninachokumbuka Ni mishkaki ile ya mia na kingine hapo minazini kuna nyumba pembeni inauza unga toka nipo mdogo mpaka leo halaf mbele kidogo kama unataka kwenda sokoni kushoto kulikua kuna nyumba imejaa mashoga wakina zungu yaan tukipita tukitoka shule tunawashangaa
Same to me mkuu

Nimezaliwa msisiri nimesoma mwananyamala b primary na kino sec yaani mwananyamala ni kitaa changu haswaaaaaa
 
Chama la wana. Mwananyamala ina wadau wengi sana apa jamii forum. Haha haha unanikumbusha kuna mshkaji alikuwa anakaa mwananyamala alafu akawa anawazuga masela wake pale Makongo Secondary kwamba anakaa kijitonyama, sasa siku iyo tunatoka pindi la tuition pale mapambano kalibia na Nakiette pharmacy wakatokea makonda wa daladala wa kitaa kwao na anko yake teja pale mwenge akaanza kumuita ankoo chukua izi kandambili peleka apo mwananyamala nyumbani sasa washkaji zake ambao walikuwa wakishua walicheka mbaya kwamba jamaaa ana anko yake TEJA
Aahahahah
 
Same to me mkuu

Nimezaliwa msisiri nimesoma mwananyamala b primary na kino sec yaani mwananyamala ni kitaa changu haswaaaaaa
He he usikute tunajuana kuna mdada tulisoma nae alifariki mwaka jana alikua anakaa huko msisiri Amina ridhiwani masikini
 
Ila sometime alikuwa anashinda kwa maneno. Ana maneno ya karaha sana.

Kuna Mzee wetu mmoja tulikuwa tunamuaminia sana halafu akapigwa. Fikiria wengine kisaikolojia tuliathirika kiasi gani!
Wacheza draft 80% wana maneno ya shombo. Na hiyo ni Tanzania nzima nafikiri, nimezunguka mikoa minne na wacheza draft wote wana maneno ya shombo
 
Pale maeneo ya msufini palikuwa na uwanja mkubwa sana unatumika ktk maswala mbali mbali km siasa, maulid ( madras)...jioni unakuta kuna cha ndimu gemu za ligi ya mbuzi unakuta vibinti micharuko na wakina mama na watoto mgongoni unasikia "usiniumizie uyoooo" hizo ligi wanacheza watu na ndevu zao ila mpira wa cha ndimu (sio gozi) hapa ndio alipotokea bondia CHEKA alikuwa golikipa kipaji chake cha ngumu kilikuja kuoneka kinondoni mahakamani(kambangwa) kuna kitu kinaitwa MTU BEE....gemu zikiisha huo uwanja unageuka sehem ya biashara samaki, vitumbua, chai n.k....biashara zikimalizia wanaingia wazee wa kazi NGETA hapo kuna kila aina ya wizi usije kukatisha eneo ilo msufini kuanzia saa tano usku UMEKWISHA
Bro pm nakujua kabisa yan
 
mshana jr you have made my day. Hilo la chapo kulipiwa ni kali kuliko. Ila ni kweli kwani uswazi kuna mengi. Nashangaa wana bongo movie wanaigiza vitu vya upeo wa juu vilivyowashinda uwezo wakati uswazi kumejaa kila aina ya hazina. Hata watunzi wa vitabu. BTW hata wewe ninahisi una kipaji cha kuandika kizuri sana
Daaah mshana umenikumbusha mbali enzi hizo nasali kanisa la wasabato mwananyamala,ilikuwa lazima nipite hapo kwenye uchochoro hili nifike kanisa lilipo
 
Back
Top Bottom