Pale uwanjani misufini ni maajabu tosha.
Mchana unakuta wanacheza mpira, ikifika saa moja jioni ni uwanja wa mama ntilie, hapo ukiwa na buku unapata dona safi, samaki, maharage, mrenda nk yaani kwa lugha nyepesi mboga saba kwa hiyo buku yako. Hapo vijana kutoka pande zote kutoka Manyanya, Kota, Uso wa Mbuzi nk wanajazana kupata mlo wa bei chee, hapo hata ukiwa na jero ina kazi.
Sasa ikishafika mida ya wanga kuna watu huwa wanakuja kuroga pale waziwazi, tena usishngae kumwona huyu anachimbia dawa ardhini na mwingine amebana chochoroni anamsubiri mrogaji akimaliza tu amkabe.
Kuna mama ntilie mmoja anasema akishaona wameanza kuroga, kwa usalama wake huwa anaamua kufungusha kilicho chake na kuondoka, anajua muda wake umeisha.