Si kwamba sitaki.
Nauliza, inawezekana kuna historia ambayo mimi siijui.
Najua Museveni kakaa Upanga mtaa wa Mindu, najua mpaka bifu za Yoweri Museveni na jirani yake Tito Okello (ambaye baadaye alimpindua). Mpaka afande Karubi alivyowasuluhisha kwenye parties za wanajeshi Mindu. Mpaka Ben Mashiba alivyomwambia Mwalimu awatenganishe na Museveni akaondoka kwenda msituni. Jinsi Museveni alivyokuwa anakodi teksi halafu halipi mpaka madereva teksi wa Muhimbili wakawa wanamkimbia, mpaka jinsi Museveni alivyotoka flat aliyopewa na Ikulu Mindu Street bila kulipa bili ya umeme na maji, mpaka akalipiwa na aliyemfuatia kukaa kwenye hiyo flat.
Huko Mwananyamala alikaa mwaka gani? Inawezekana alikaa, sijui, nauliza tu.