Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Ila nakumbuka zamani kuna Shost wangu alikuwa anaishi mwananyamala kwa msisiri.ni zamani nyumba yao ilikuwa karibu na gesti imenibidi nimuulize ile gesti inaitwaje ameniambia ni kamanyola watu walikuwa wanapiga chabo mno.shost wangu mwenyewe ameshahama nyumba mamaake aliiuza wakahama
Anaitwa nan shost wako?
 
MITAA YANGU YOTE ILE KUANZIA MKWAJUNI MPAKA A,
ila kino mango garden ni zaidi ya nyumbani,mkuu mshana aliyoongea yote nilikua mshiriki mzuri tu ofisi bar tunakula monde tunapiga hela,ujamaa kwa matapeli ni wa kuheshimiwa,nikipiga pesa,tunakula na kunywa wote hivyohivyo ukipiga pesa wewe.
Deal zikikosekana wafadhili wapo utakula bia na nyamachoma km kawa ila hakuna atakayekukopesha hela
 
Kuna mzee alikuwa anaitwa mzee Mbaga tajiri alikuwa na mifugo mingi tu ng'ombe, mbuzi, kondoo sehem yake ya machungio makaburini kwa kopa pale ukimfukuza mfugo wake anakwambia "nitukane mimi" nipige mimi" ila sio ng'ombe wangu alikuwa mtata balaa..alipokufa alizikwa makaburi hayo hayo na kaburi lake walikuwa wanalinda wamasai alizikwa na Mali pia na bunduki yake..aftr km 3years or 4 sina kumbukumbu vizur walikuja watoto wake walikuwa wanaishi japan au america kaburi likafukuliwa maiti ikatolewa ikiwa ktk sanduku wakaenda kumzika upya kinondoni mwembe jini
Mzee mbaga jaman alikua na hela daah
 
Huyo hadija mkandu aliwahi kunipiga mkwara hapo shuleni m/nyamala B...nilikuwa nikimuona sina amani.
Sasa hivi amekuwa mwalimi
Mwaka aliokufa nyerere yuleeee nyerere..mwalimu elias, mwalim mshana, martin, ndeka,....unamkumbuka Msuto, balowa, zamarad, khadija mkandu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hadija mkandu sijaamini nilivyoambiwa mwalimu wapi wakina mwanunu mpate group lao jaman daah nimekumbuka yale maisha yule mama aliyekua anatuuzia supu na ndizi na ubwabwa he he kayumba bana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah nitashuka chini kule pale kwa wazee wake japo kaubani aisee km namuona amina kuanzia darasa la kwanza to seven nimesoma nae mitaa yetu ya kujidai msisiri pale ccm kuangalia mapicha + vichwa vya kuku...
Waonesha muvi, bubu,mbwana,rashd matata n.k ful kolokolo pale ....kamali asubuhi ,mchana muv usiku pilau,kishoka hahaha kuna siku nilitoroka hom kwenda kucheck pilau mida ya saa 5 nkaingia nkakaa mbele kabisa chini ile nageuka nyuma nakuta mjumbe wetu wa nyumba kumi nae ndani ya nyumba daaaaah
 
Draft bila maneno ya shombo halinogi. Mfano pale umemfunga mpinzani wako ambaye anakudharau utasikia anakuambia wewe ni baiskeli ya miti atakukuta mlimani/kwenye tambarare au anakwambia ndege kumnyea mtu sio shabaha ni bahati tu. Pia ukifunngwa na mtu mwenye shombo atakuambia ulikuwa unalia nataka cheza na kaka huku kabana pua kama anavyoongea mtoto mdogo. Yaani draft kama una hasira za haraka huwezi utakuwa unarusha ngumi kila mara.
Draft nimeona nyamala wanachezea kamari wati wanapandiana
 
  • Thanks
Reactions: mij
MITAA YANGU YOTE ILE KUANZIA MKWAJUNI MPAKA A,
ila kino mango garden ni zaidi ya nyumbani,mkuu mshana aliyoongea yote nilikua mshiriki mzuri tu ofisi bar tunakula monde tunapiga hela,ujamaa kwa matapeli ni wa kuheshimiwa,nikipiga pesa,tunakula na kunywa wote hivyohivyo ukipiga pesa wewe.
Deal zikikosekana wafadhili wapo utakula bia na nyamachoma km kawa ila hakuna atakayekukopesha hela
Kweli hela ya laana haikai[emoji3][emoji3]
 
Waonesha muvi, bubu,mbwana,rashd matata n.k ful kolokolo pale ....kamali asubuhi ,mchana muv usiku pilau,kishoka hahaha kuna siku nilitoroka hom kwenda kucheck pilau mida ya saa 5 nkaingia nkakaa mbele kabisa chini ile nageuka nyuma nakuta mjumbe wetu wa nyumba kumi nae ndani ya nyumba daaaaah
Dah umenikumbukusha kitambo kidogo
 
Huyo hadija mkandu aliwahi kunipiga mkwara hapo shuleni m/nyamala B...nilikuwa nikimuona sina amani.
Sasa hivi amekuwa mwalimi
Alikuwa anachonga sana yule mdada ila aliyaanza mambo ya kikubwa akiwa mdogo sana...wakati naanza darasa la kwanza B kwa mwalimu elias kuna dogo anaitwa rashid anaishi ujiji na mwingine anaitwa msafiri nowdys yupo soko la mapinduzi anauza mkaa walinipiga biti la maana mpaka kesho yake sikurudi tena shule B kisa nimekaa ktk dawati sehem niliyoka ni sehem ya mwenzao siku hio alikuwa ajakuja shule maana nilichelewa km week moja kuanza shule so wale walikuwa wajanja wakawa wananiambia "toka nenda ukakae chini au nenda ukakae kwa wanawake wenzio" yanii dawati la mbele yupo fatm mnyeto na zamarad wananiambia "nenda ukakae pale kwa wanawake wenzio toka hapa" huyo rashid mweusiiii niliogopa sana kurudi home nikalia sana kwa mzee nikamwambia wananiambia mimi mwanamke mara wananivuta na nywele wakati mim mwanaume mwenzao bibi kubwa kusikia ivyo akamaind sana maana alikuwa ananidekeza sana akanipeleka mtendeni primary wakati yeye bi mkubwa anafanya kazi pale pale akiba mimi nasoma mtendeni akitoka job tunarudi mwanyamala sasa nikirudi mtaani nakuwa mnyonge maana watoto wakihindi wanishia town tu hapa uswaz kwetu watoto wote wanasoma B stori zao za B za shule kwao..kuingia la pili nikataka tena kurudi B mzee akanichukua mwanyamala B nikarudishwa darasa lile la mwalimu elias dah makamanda nikawakuta tena wapo vile vile this time nilikuwa nishachangamka kidogo mapumziko ni ngumi tu pale uwanjani B wakati huo vumbi jekunduuu
 
Kuna mwanangu mmoja nilisoma nae A level kwao ni Kigoma uko alikua hajawahi kukanyaga Dar akawa anatuganda kinoma tuibuke nae angalau asafishe macho(tulikua tunasoma Uyui Tabora uko) basi wana Darisalama tukambeba swahiba mpaka mjini baada ya wiki kadhaa akakutana na ndugu yake anakaa M'nyamala hosp pale swahiba akanogewa na ruti za mjini ile alivyomaliza shule akaibuka mazima Mungu sio Mshana jr akachaguliwa UDSM basi hata nafasi ya kugusa darasa la chuo hakupata maana nakuja kumuona amechakaa kwa unga yule ndugu yake alimgeuza kifaa cha majaribio ya unga hata taarifa kua amepata nafasi chuo cha ndoto yake hakua nayo.
 
Back
Top Bottom