Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Kuna boda moja maeneo ya msikiti wa mchangani unafanya kama unaenda Tandale....lilikuwa eneo hatari sana.
 
Nasubiria uzi wa Tandale na Mabibo .
Huwaga nakutana nao sana masela wa mabibo hapa uwanja kinesi kwenye mechi za ligi daraja la pili. Wana stori nyingi sana za uswahilini.
 
Mkuu nimefurahi sana na huu uzi mana umenikumbusha mbali niliwahi kukaa mwananyamala miaka ya 2002 mitaa ya nyuma ya guest ya kamanyola. Lakin kuna baadhi ya vituko nilikua sijui aisee labda kwa kuwa nilikuwa mtu wa kuja kulala asubuhi naondoka mpaka tena usiku usiache kuni tag ukileta uzi mwingine.
Pouwa na mimi ni almost same time 2001-2010 karibu na Tiger
 
Nimeona watu Wa Mwananyamala wanaulizana kuhusu pombe. Ila sisi wa magomeni kagera , Mburahati na kigogo tunaulizana ulifika au uliishia msumbiji?

kweli kaka yaani toka naanza primary nasikia huyu kazamia sijui yupo south, mara chindolo yupo nepal yaani full kuhustle
 
Kuna jamaa alikuwa anaitwa Stiba....sijui alishia wapi alikuwa anawakalisha sana wahuni wa kinondoni
 
Uzuri wa huu uzi umefanya watu wote wamekuwa marafiki, hakuna kuparuana watu kumbe wengine wanajuana kabisa toka enzi za utoto namuona JINGALAO naye kumbe ni mtoto wa kitaa kabisa safi sana mwisho wa siku wote ni ndugu.

Haya wazee wa Friends ranger, Messina, Kagera ranger, Nyarugusu Fc, Milambo, Faru dume, National, Las vegas, sheki utd, abajalo, sinza stars dah zama zile bwana ilikuwa hatari, MSHANA tuletee uzi wa Magomeni,Manzese, Sinza, Tandale, shekilango, mburahati,tiptop..

daaah umegusa pale pale hayo machama yote nayanyaka nimesona mwembechai karume, skani kagera mikoroshini
 
daaah umegusa pale pale hayo machama yote nayanyaka nimesona mwembechai karume, skani kagera mikoroshini

Hahahahaha Mzozo na vijana wake wapo, karume ya Machano? au karume ipi mkuu..
 
Hapo kamanyola kuna chochoro lilikuwa refu ndo lina madirisha ya gest kuna mshkaj anaitwa ibrahim alienda kupiga chabo akakuta mama yake mzaz anasukumiwa mashine mbuz kagoma jamaa alilia kwa sauti mpaka wakasikia wahudumu

Shenzi kabisa....!!!
 
Hiyo mitaa ya Mwananyamala,Tandale,Kino,Manzese,Magomeni nk hata askari wake walikuwa timamu sio legelege maana uhalifu ni sehemu ya maisha huko... Askari wengi wa hayo maeneo walikuwa wacheza ngumi kama akina KOBA KIMANGA, HASSAN MATUMLA nk.. Huko askari akiwa legelege kila siku unachezea vitasa maana watoto wa kihuni hawaendi polisi kizembe.. Ule uhalifu ndio ulisababisha kituo cha Mabatini kizaliwe.
 
Mada ya Mfahamu James Ngomero: Bingwa mtuhumiwa wa zile maiti 11 za watoto hospitali ya Mwananyamala imenikutanisha na watu wengi ambao kwa namna moja ama nyingine tunaweza kuwa tunafahamiana kabisa...

Si hilo tu bali nimegundua sehemu kubwa wanaJF Dar wengi ni wakazi wa Mwananyamala/Kinondoni katika ujumla wake...

Kuishi Mwananyamala pekee ni chuo tosha... Ikiwapendeza kwa uwingi wetu tunaweza kuwa na huu uzi wa vituko vya Mwananyamala mtaa kwa mtaa... Naamini kama umeishi Mwananyamala hutokosa cha kusimulia.

1. Madawa ya kulevya: Mwananyamala eneo lote la Mwananyamala A ni kituo na kitovu kikubwa cha madawa ya kulevya kuanzia wauzaji mapusha mpaka watumiaji... Hospital ya mwananyamala ina kituo cha kutoa tiba kwa mateja na nadhani ndio kituo kikubwa zaidi Tanzania.

2. Hospital ya mwananyamala: Ndio hospital maarufu zaidi yenye vituko na kashfa nyingi... Kuanzia kutoa mimba, kashfa ya vichanga 11, wizi wa maiti, rushwa... Maiti iliyofumuliwa na kutolewa madawa na madaktari kuiba hayo madawa,... Nk nk.

3. Matapeli: Hapo ndio kwake.. Mitaa maarufu ikiwa ni kuanzia kwa Kopa, A mpaka karibu na Kinondoni B, wale matapeli maarufu mmoja akijulikana kama doctor... Wale matapeli kiboko wa Jerry Muro, bar yao kubwa ilikuwa nyuma ya hospital ya Mwananyamala.

4. Ofisi na kampuni za mifukoni: Eneo lote la Kinondoni Mkwajuni mpaka Biafra ni hatari kwa shughuli hizo.. Utataka nini ukose.. Mihuri ya siri? Nyaraka za serikali? Mikataba mbalimbali, nyaraka za kusafisha mizigo.. Pesa bandia, madini bandia.. Kila kitu hukosi hapo. Mitaa hiyo ni maarufu kwa madaktari feki, Wanausalama, polisi, wanajeshi mahakimu, wanasheria, wabunge hata mawaziri nk

5. Machangudoa, wasagaji, mashoga, Mario nk... Mtaa wa wibu ndio kama kitovu cha mashoga.. Ukiwasikia kina anti abuu, anti Ali hiyo ndio ilikuwa mitaa yao.. Habari za Machangudoa na wasagaji zinajulikana wazi.. Kinondoni na Mwananyamala ndio headquarters..

6. Wezi, vibaka majambazi, wakora nao wako: Ukisikia roba za mbao na watu wanaitwa mbavu Mwananyamala ndio kwao

7. Wachawi wanga na waganga Wamo pia.. Mwananyamala kuna military base kubwa sana/KILINGE ya wachawi.... Lile anga limechafuka.

8. Wasanii wanamuziki wa aina zote: Bongo movies, Taarab, na kadhali kaliba yote hii kwa sehemu kubwa chimbuko ni Mwananyamala

9. Wahamiaji haramu: Wakongo, Wamalawi, Wakenya, Waganda, Warundi nk... Sehemu kubwa wamejazana Mwananyamala.

Yako mengi ya kuandika kuhusu Mwananyamala siwezi kuyamaliza yote... Mengine yataandikwa na kusimuliwa na WanaJF - Mwananyamala Wing...
Kuna jamaa alipigwa hela pale nyuma ya hospitali, aliulizwa simple tu, unajua kingereza? we mtoto wa mjini? akajibu ngeli napiga na mimi mtoto wa mjini wakampa bunda la blue blue na wakamwambia kabisa huo mzigo famba wanataka kumpiga mzungu, yaani ampelekee mzungu mmoja halafu eti yule mzungu atampa dola aje nazo moja kwa moja pale walipo halafu yeye ujira wake dola 100 akasema poa, hawa jamaa wakampa sharti aache wallet pale na vitambulisho vyote, jamaa kaangalia lile bulungutu la bluu bluu halafu wallet yake ina kilo tu (100,000) akaaingia line akaacha wallet na vitambulisho vyake, kapewa namba ya mzungu wakaanza kuwasiliana mpaka wakakutana na mzungu, akachukua bluu bluu akapewa bulungutu la dola katia mfukoni kasepa, kurudi kule kakuta hamna mtu, kumbe mzungu naye mpigaji tu dola alizopewa juu ilikuwa 100 famba chini dola , katikati makaratasi. Laki imeondoka.
 
Hahahahaha Mzozo na vijana wake wapo, karume ya Machano? au karume ipi mkuu..

iyo iyo ya machano, mzozo yupo na friends ranger ipo daraja la 1, mzozo kasaidia wachezaji wengi sana tatzo tu elimu hana ila jamaa peace sana
 
Kuna jamaa alipigwa hela pale nyuma ya hospitali, aliulizwa simple tu, unajua kingereza? we mtoto wa mjini? akajibu ngeli napiga na mimi mtoto wa mjini wakampa bunda la blue blue na wakamwambia kabisa huo mzigo famba wanataka kumpiga mzungu, yaani ampelekee mzungu mmoja halafu eti yule mzungu atampa dola aje nazo moja kwa moja pale walipo halafu yeye ujira wake dola 100 akasema poa, hawa jamaa wakampa sharti aache wallet pale na vitambulisho vyote, jamaa kaangalia lile bulungutu la bluu bluu halafu wallet yake ina kilo tu (100,000) akaaingia line akaacha wallet na vitambulisho vyake, kapewa namba ya mzungu wakaanza kuwasiliana mpaka wakakutana na mzungu, akachukua bluu bluu akapewa bulungutu la dola katia mfukoni kasepa, kurudi kule kakuta hamna mtu, kumbe mzungu naye mpigaji tu dola alizopewa juu ilikuwa 100 famba chini dola , katikati makaratasi. Laki imeondoka.
Kweli Bongo Daslam[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Kuna jamaa alipigwa hela pale nyuma ya hospitali, aliulizwa simple tu, unajua kingereza? we mtoto wa mjini? akajibu ngeli napiga na mimi mtoto wa mjini wakampa bunda la blue blue na wakamwambia kabisa huo mzigo famba wanataka kumpiga mzungu, yaani ampelekee mzungu mmoja halafu eti yule mzungu atampa dola aje nazo moja kwa moja pale walipo halafu yeye ujira wake dola 100 akasema poa, hawa jamaa wakampa sharti aache wallet pale na vitambulisho vyote, jamaa kaangalia lile bulungutu la bluu bluu halafu wallet yake ina kilo tu (100,000) akaaingia line akaacha wallet na vitambulisho vyake, kapewa namba ya mzungu wakaanza kuwasiliana mpaka wakakutana na mzungu, akachukua bluu bluu akapewa bulungutu la dola katia mfukoni kasepa, kurudi kule kakuta hamna mtu, kumbe mzungu naye mpigaji tu dola alizopewa juu ilikuwa 100 famba chini dola , katikati makaratasi. Laki imeondoka.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nasikia kuna wizi wa majeneza umeibuka msisiri B... Mzee mmoja anasema anashangaa miaka yote haijawah kutokea[emoji3]
 
mshana jr ebu nifafanulie mtaa wa Pamba Street pale Mwananyamala A, una kasoro gani? Nasikia ale kuna Mze mmoja hivi alikuwa mchawi kishenzi na alikuwa anafanya kazi bandarini. Huko bandarini watu wakimuudhi tu hupotea majini na pale mtaani kwao watu walikuwa hawakanyagi. Una ufahamu wowote juu ya huu mtaa? Mimi nilkuwa natokaga na demu fulani toka pale na ndipo nilipokuwa nasikiaga hizi story za kutisha ila huyo mze mwenyewe sijawahi kumuona.
 
Back
Top Bottom