Vituko;- WAKENYA WATUA NCHINI TANZANIA KUDAI MAHINDI YAO

Vituko;- WAKENYA WATUA NCHINI TANZANIA KUDAI MAHINDI YAO

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
28,064
Reaction score
31,401
MOSHI,

WAKATI baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania wakidai malori yaliyokamatwa yalikuwa hayatoroshi mahindi kwenda Kenya, wafanyabiashara wa Kenya walifika mjini Humo Jumanne juzi na kufanya vikao na wenzao wa Tanzania.

Inadaiwa katika kikao hicho, Wakenya walioingia nchini kwa mgongo wa ujirani mwema walitoa shinikizo kwa wenzao wa Tanzania wawape mizigo yao au warudishe fedha.

"Wako kwenye wakati mgumu maana wao (Wakenya) walishalipa kila kitu mpaka fedha za kusafisha njia. Sasa wanashangaa kwa nini yamekamatwa,” gazeti la Mwananchi lilidokezwa na chanzo chake.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, inadaiwa kuwa wafanyabiashara ambao malori yao yamekamatwa wanashinikiza yaachiwe kwa kisingizio hayakuwa yakienda Kenya kwa vile yalikamatwa Himo.

Ofisa wa Polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe alilithibitishia gazeti hili kuwapo kwa wafanyabiashara wa Kenya ambao wanaendelea kufuatilia nyendo zao kujua ni lini wataingia tena.

“Tulipata taarifa juzi kuwa waliingia na walikuwa wakifanya kikao pale stendi Njiapanda na baa moja pale Himo lakini inaonekana taarifa zilivuja wakatawanyika,” alisema ofisa huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah alipotafutwa kwa simu jana alijibu kwa kifupi kuwa alikuwa kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Himo Jamal Hussein, alikiri kwa wafanyabiashara kutoka Kenya kuingia Himo kwa kigezo cha ujirani mwema lakini hajui kama wanahusika na mahindi.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira aliwaambia wanahabari kuwa katika operesheni ya kudhibiti utoroshaji wa chakula wameshakamata malori 103.

Kamatakamata hiyo iliongezewa nguvu na amri ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliyeagiza mahinndi yatakayokamatwa yakisafirishwa kwenda nje ya nchi yataifishwe pamoja na magari.
 
Ngoja tuwaonyeshe Sisi wavivu kama tuna Walisha wasio wavivu
sawa mnatulisha kweli ila mbona bidhaa zetu chungu nzima na benki za kenya zimejaa kote tanzania..viwanda vya maziwa...ndege za KQ na jambojet zapaa anga za Bongo..watalii wanakuja kuiona Kilimanjaro toka Amboseli....ni biashara tu bro usipandwe na mori...mpunguze mihemko...😀😀japo mnatulisha, biashara kati ya TZ na KE favors Kenya more than TZ in terms of volume of trade...we export more than we import from you...sasa mahindi tu isikupe mihemko jirani..tukipeleka biashara kwingine, wakulima wataumia..usishangae wakati fahali wanapigana, nyasi ndio huumia kama sasa vile wauzaji gesi wa tz na wanunuzi toka kenya wanaumia...
 
Ngoja tuwaonyeshe Sisi wavivu kama tuna Walisha wasio wavivu
Wameshaanza kununua ya Ethiopia. Kulingana na BBC Swahili, wamenunua tani 260 kwa $21.3m.

Lakini ya Ethiopia hayana muda sana, wenyewe njaa kali.Ni mara ngapi waethiopia wanakimbia kwao sababu ya njaa?
 
basi tutanunua kwingine...nadhani mahindi ni bidhaa rahisi kupata..mbona nchi nyingi tu zinafanya kilimo ch mahindi....mahindi si kama dhahabu
Mwaka huu ugali utakuwa anasa kwa manyangau ukipika ugali unaitwa mweshimiwa[emoji2]
 
Uwezo wa serikali yetu kununua mahindi toka kwa wakulima ni mdogo ukilinganisha na kiasi kinacholimwa.

Wakulima wetu hawana uwezo wakuhifadhi mahindi yote wanayovuna kutokana na uwezo wao mdogo na njia zakuhifadhi mahindi yasiharibike.

Wakiuza kwa bei nzuri angalau (kwamajirani) japo nao waboreshe maisha yao serikali inaleta nongwa.

Sasa hawa wakulima wafanyeje? Ukizingatia soko la ndani limedorora na wanauza kwahasara!

Huku wakulima hao hao wana mikopo kwenye mabenki, vikoba, Sacco's bila kusahau pembejeo wanataka chao.
Hapo mi ndio nashindwa kuelewa hii nchi yetu ni yaaina gani. Kila kitu siasa
 
Wameshaanza kununua ya Ethiopia. Kulingana na BBC Swahili, wamenunua tani 260 kwa $21.3m.

Lakini ya Ethiopia hayana muda sana, wenyewe njaa kali.Ni mara ngapi waethiopia wanakimbia kwao sababu ya njaa?
Hayo nimahindi madogo sana
rejea waliyo nunua Israel
 
Back
Top Bottom