MOTOCHINI
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 28,064
- 31,401
MOSHI,
WAKATI baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania wakidai malori yaliyokamatwa yalikuwa hayatoroshi mahindi kwenda Kenya, wafanyabiashara wa Kenya walifika mjini Humo Jumanne juzi na kufanya vikao na wenzao wa Tanzania.
Inadaiwa katika kikao hicho, Wakenya walioingia nchini kwa mgongo wa ujirani mwema walitoa shinikizo kwa wenzao wa Tanzania wawape mizigo yao au warudishe fedha.
"Wako kwenye wakati mgumu maana wao (Wakenya) walishalipa kila kitu mpaka fedha za kusafisha njia. Sasa wanashangaa kwa nini yamekamatwa,” gazeti la Mwananchi lilidokezwa na chanzo chake.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, inadaiwa kuwa wafanyabiashara ambao malori yao yamekamatwa wanashinikiza yaachiwe kwa kisingizio hayakuwa yakienda Kenya kwa vile yalikamatwa Himo.
Ofisa wa Polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe alilithibitishia gazeti hili kuwapo kwa wafanyabiashara wa Kenya ambao wanaendelea kufuatilia nyendo zao kujua ni lini wataingia tena.
“Tulipata taarifa juzi kuwa waliingia na walikuwa wakifanya kikao pale stendi Njiapanda na baa moja pale Himo lakini inaonekana taarifa zilivuja wakatawanyika,” alisema ofisa huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah alipotafutwa kwa simu jana alijibu kwa kifupi kuwa alikuwa kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Himo Jamal Hussein, alikiri kwa wafanyabiashara kutoka Kenya kuingia Himo kwa kigezo cha ujirani mwema lakini hajui kama wanahusika na mahindi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira aliwaambia wanahabari kuwa katika operesheni ya kudhibiti utoroshaji wa chakula wameshakamata malori 103.
Kamatakamata hiyo iliongezewa nguvu na amri ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliyeagiza mahinndi yatakayokamatwa yakisafirishwa kwenda nje ya nchi yataifishwe pamoja na magari.