Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

Kikwete na Mwinyi mtabaki kuwa bora kuliko hao watatu waliobaki
 
Hata Marekani wanadhibiti kwa kasi sana, urusi pia, uhuru bila mipaka ni hatari kwa usalama wa nchi.Twende na JPM gari la uhakika
Marekani hawawezi kuwa wajima kama Tanzania. Freedom ndio iliyowafikisha hapo kimaendeleo.
 
Wakati wanasiasa wa upinzan wanafanyiwa vitendo vya kibabe hivi vyombo havikukemea basi subiri wanyooshwe
 
CCM hamuwezi kuvifunga mdomo vyombo vya nje kama ambavyo mmefanya kwa hivi vya ndani ambayo mmefanikiwa kwa 100%.....acheni huu mpango utawaghakimu mno..

BBC ni shirika kubwa sana....
 
RFA wamejiunga na DW,BBC na VOA km kawaida hao wengine ni uoga wao tu
 
Ukishaona kwenye nchi kuna sheria zinazotungwa kufuata tabia binafsi ya kiongozi wa nchi, ujue itakuwa vigumu kiongozi huyo kutoka madarakani, na sio kutoka tu, bali kutoka kwa amani.
Binafsi siilaumu TCRA bali navilaumu Vituo vya Habari kwa ujumla wake. TCRA ni chombo cha ukandamizaji na kinaendeshwa na washamba na limbukeni kwa matakwa na maelekezo ya mshamba mkuu na limbukeni mkuu. Uhusiano wa TCRA na Vituo vya Habari inanikumbusha ile hadithi ya ngamia na mwarabu.

TCRA ilianza kuviingilia vyombo vya habari taratibu bila upinzani wowote kutoka vyombo hivyo. Walianza na vyombo ya Umma na walipofanikiwa kwa kutowepo na upinzani wowote wakaanza kuviingilia vyombo binafsi. Ilifikia hatua waandishi wa vyombo hivi wakasalimu amri na kusahau wajibu wao kwa jamii.

Nguruwe wamevamia ghala...kwa leo nitaachia hapo.
 
kwani Radio Free Africa inasikika UK na Ujerumani??
Huu ndio ushamba unaosemwa kila siku na akina Zitto! Kwenye maisha lazima kuwe na watu/nchi/jamii kuzidiana. Wewe uliyezidiwa inakupasa kuiga/kudesa/ copy and paste kutoka kwa ambaye amekuzidi. Kwenye elimu hii kitu wameipa jina zuri la Literature Review, but ukweli ni lazima kuchukua vya waliotangulia uvitumie
 
Tanzania inakimbilia kuwa kama kisiwa. Sipati picha katiba inavyoenda kubadilishwa na Rais magufuli kuwa Rais wa milele kama Uganda na Rwanda.
 
Kingine wamesahau kuwa sikuhiz dunia iko kiganjani naweza soma chochote hata cha korea kaskazini
Hili Ni kwa maslahi yako binafsi.

Kwa maslahi ya umma hakika huyu mshamba aliyeshika remote lazima tumfurumishe ofisini.
 
hii ndo tz ya mwalim nyerere mpaka raha yani ok acha tu mungu atende juu ya taifa lake alilolitengeneza mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…