Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Marekani hawawezi kuwa wajima kama Tanzania. Freedom ndio iliyowafikisha hapo kimaendeleo.Hata Marekani wanadhibiti kwa kasi sana, urusi pia, uhuru bila mipaka ni hatari kwa usalama wa nchi.Twende na JPM gari la uhakika
Tutarara mbere na wewe. Kwanza unatumia rifrekwensi gani uko ?Mimi nasikiliza online BBC na DW, Mkurugenzi wa BBC amesema jioni hii atatoa msimamo rasmi
Hahahaha huku natumaiga ribando rangu ra TigoTutarara mbere na wewe. Kwanza unatumia rifrekwensi gani uko ?
Wakati wanasiasa wa upinzan wanafanyiwa vitendo vya kibabe hivi vyombo havikukemea basi subiri wanyooshweKatika hali ya kushangaza na, vyombo vya habari ambavyo awali vilikuwa vinajiunga na vyombo vya nje kurusha matangazo sasa vimesitisha urushaji huo. Leo Radio One, Abood Radio na baadhi leo havijajiunga na vyombo hivyo vya kimataifa kurusha matangazo yao. Hii inawezekana ni kutokana na mkwara wa TCRA ambao wameanza kwa kuichapa faini Radio One Stereo ya shilingi milioni 15. Hali inaanza kuwa mbaya sasa katika uhuru wa habari
RFA wamejiunga na DW,BBC na VOA km kawaida hao wengine ni uoga wao tuKatika hali ya kushangaza na, vyombo vya habari ambavyo awali vilikuwa vinajiunga na vyombo vya nje kurusha matangazo sasa vimesitisha urushaji huo. Leo Radio One, Abood Radio na baadhi leo havijajiunga na vyombo hivyo vya kimataifa kurusha matangazo yao. Hii inawezekana ni kutokana na mkwara wa TCRA ambao wameanza kwa kuichapa faini Radio One Stereo ya shilingi milioni 15. Hali inaanza kuwa mbaya sasa katika uhuru wa habari
Binafsi siilaumu TCRA bali navilaumu Vituo vya Habari kwa ujumla wake. TCRA ni chombo cha ukandamizaji na kinaendeshwa na washamba na limbukeni kwa matakwa na maelekezo ya mshamba mkuu na limbukeni mkuu. Uhusiano wa TCRA na Vituo vya Habari inanikumbusha ile hadithi ya ngamia na mwarabu.Ukishaona kwenye nchi kuna sheria zinazotungwa kufuata tabia binafsi ya kiongozi wa nchi, ujue itakuwa vigumu kiongozi huyo kutoka madarakani, na sio kutoka tu, bali kutoka kwa amani.
Huu ndio ushamba unaosemwa kila siku na akina Zitto! Kwenye maisha lazima kuwe na watu/nchi/jamii kuzidiana. Wewe uliyezidiwa inakupasa kuiga/kudesa/ copy and paste kutoka kwa ambaye amekuzidi. Kwenye elimu hii kitu wameipa jina zuri la Literature Review, but ukweli ni lazima kuchukua vya waliotangulia uvitumiekwani Radio Free Africa inasikika UK na Ujerumani??
wale nimewaheshimu kwa kuendelea kurusha matangazo. wengine wamemuwa utopolo tuRFA wamejiunga na DW,BBC na VOA km kawaida hao wengine ni uoga wao tu
Hili Ni kwa maslahi yako binafsi.Kingine wamesahau kuwa sikuhiz dunia iko kiganjani naweza soma chochote hata cha korea kaskazini
hii ndo tz ya mwalim nyerere mpaka raha yani ok acha tu mungu atende juu ya taifa lake alilolitengeneza mwenyewe
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo amevitaka Vituo vya Utangazaji (Radio, Televisheni, Blogs na Online Tv) kuzingatia Kanuni mpya za Maudhui Mtandaoni 2020 na Kanuni Mpya za Redio na Televisheni 2020.
Mihayo ameyasema hayo wakati wa kikao kati ya TCRA na Vituo vya Utangazaji (Radio,Televisheni,Blogs na Online Tv) Kanda ya Ziwa ambacho pia kimehudhuriwa na Maandishi wa Habari wa vituo hivyo, kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 10,2020 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Kikao hicho kilichoandaliwa na TCRA kwa kushirikiana na COSOTA kililenga kukusanya maoni ya wadau yatakayotumika kwenye marekebisho ya Kanuni za hakimiliki,uwasilishaji mada za namna ya kuripoti wakati wa Uchaguzi mkuu na marekebisho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za 2020.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhandisi Mihayo alisema Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya Habari na Utangazaji imetoa maboresho ya Kanuni za maudhui mtandaoni zijulikanazo kama “THE ELECTRONIC AND POSTAL COMMUNICATIONS (ONLINE CONTENT) REGULATIONS,2020” ambapo Kanuni hizo zimelenga kuboresha huduma za maudhui mtandao na usimamizi wake kutokana na uzoefu uliopatikana kwa kipindi cha miaka miwili toka Kanuni za zamani zilipoanza kutumika mwaka 2018.
Mkuu huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa,alisema Kati ya maboresho muhimu yaliyofanyika kwenye Kanuni za mwaka 2018, na kuingizwa kwenye Kanuni mpya za maudhui mtandao mwaka 2020 ni pamoja na Mgawanyo wa makundi ya leseni mtandao.
Alitaja makundi hayo kuwa ni Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya Habari na Matukio (News and Current Affairs), Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya waburudishaji kama vile filamu, muziki, vichekesho, cartoon, drama n.k (entertainment), Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya utoaji elimu tu (education programmes) na Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya maudhui ya dini (religious content).
“Kwa kuzingatia uzoefu uliopatikana kwa miaka miwili, Kundi la watoa huduma za maudhui ya elimu na dini limepunguziwa gharama za leseni na malipo ya kila mwaka kwa asilimia 50%. Kutoka fedha ya Kitanzania Million moja (1,000,000/=) mpaka laki tano (500,000/=) Punguzo hilo limelenga kuwafanya watanzania wengi washiriki kutoa huduma za maudhui mtandao bila kuvunja Sheria”,alisema Mhandisi Mihayo.
Alibainisha kuwa Kanuni mpya za maudhui mtandao 2020 imeweka vifungu vya maelekzo ya kuwalinda watoto na maudhui yasiyofaa na kuzuia maudhui yasiyofaa mtandaoni huku akiwasisitiza watoa huduma mtandaoni kuepuka kutangaza vitu ambavyo hawana uhakika navyo.
Aidha kwa upande wa adhabu kwa wenye leseni za kutoa huduma mtandao alisema adhabu kwa wenye leseni za kutoa huduma za maudhui mtandao zimefafanuliwa na kuongeza adhabu zingine ambazo ni sasa mtoa huduma mtandaoni atapewa Onyo kali,Kuomba msamaha kutumia vyombo vya habari na Kuamriwa kuondoa maudhui yasiyofaa.
Katika hatua nyingine Mihayo alivitaka Vituo vya Utangazaji vinavyojiunga na vyombo vya habari vya nje kuomba kibali TCRA ili kupatiwa kibali cha kujiunga na vyombo vya nje ili kuendelea kupokea matangazo.
View attachment 1532913
Mhandisi Mwandamizi TCRA Kanda ya Ziwa,William Mnyippembe akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za uchaguzi katika kikao kati ya TCRA na Vituo vya Utangazaji (Radio,Televisheni,Blogs na Online Tv) Kanda ya Ziwa.
CHANZO: Malunde