Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Hayo ni mabaki ya teaching AIDS aina ya CADAVER ,Ni mfano wa umbo la mwanadam kwa kila kitu lakini ni man-made na huwa kama plastic.Wanafunzi wanafanya mafunzo kwa vitendo na kusoma Blood-system na muscles za mwili.Kinacho kuwa tatizo ni kwamba njia waliyotumia kuyahifadhi baada ya kuwa used ndo imeleta utata.Walitakiwa watumie hata kemikali kuyateketeza kuliko kufunga kwenge mifuko ya rambo na kupeleka dampo.

Poleni kwa mshtuko lakini asanteni wanachi mliotaka kujua undani wa swala hilo.

Ina maana hakuna wanafunzi wengine watakaosoma masomo hayo !!! Maana katika shule na vyuo vingine tena katika nchi masikini kama Tanzania teaching aids zilizoachwa na Wakoloni bado zinatumika!!! Iweje hizo teaching aids tena kwa ajili ya masomo ya udaktari zitupwe, halafu nyingine zikiwa bado mbichi kama zinatoa damu.
 
Du! Only in Tanzania can happen. Sasa watu wote hao walikuwa hawana ndugu?kuna ndugu yangu aliondoka home tangu miaka ya 78 mpaka leo hajarejea..sijui....
 
Usishangae chikutentema. Hayo ni sehemu tu mazingira ya anayokutana nayo daktari wa binadamu katika masomo yake ya miaka 5+1. Ukifika kazini,bado huwezi kutekeleza kikamilifu yale uliyosoma. Madaktari wakidai mazingira bora ya kazi,inakuwa nongwa, wananchi wanataka kuwapiga mawe. Picha za miili hiyo,tayari watu wanataharuki; ukiingia kwenye chumba chenyewe.....

Ni kweli mkuu wana kazi ngumu imagine watu wameona hapo panic je madaktari hali wanayokumbana naye.serikali iongeze budget kwenye wizara ili waweze ku improve kwenye hiyo sector
 
Last edited by a moderator:
Siyo Bunju ya Gaza bali ni Gaza ya Bunju, ila ni kwakua tanuru la kuchoma viungo hivyo hapa Muhimbili liliharibika so the only options ikawa kuvitupa jalalani
du watazania ni zaidi ya waisraeli/mayahudi kwa sasa,, watu tunahangaika kuwasomea dua marehemu wetu ili wakae kwa amani kule barzak wakisubiri hukumu siku ya kiama kumbe watolewa ngozi na kutupwa au kuchomwa... mhhh
 
Hili kwa namna moja ama nyingine haiwezi kuliacha hivi hivi!

Haikubaliki hata kidogo!
 
Je hao watu / miili waliwatoa wapi?
Na kama walifukua maiti ni kwanini wasiwarudishe kwenye makaburi yao?
Chuo cha kuweza kufanya kitu kama hicho hakifai;
kama kufungwa na kifungwe ili wakajipange upya.


Tatizo ukikifunga nini itakua hatima ya watoto weti wanosoma hapo. Ila kuna haja ya kuchunguza zaidi kujua hicyo mili ilipatikanaje, isije ikawa kuna wengine walienda wanaumwa vichwa wakaishia huko.
 
Je hao watu / miili waliwatoa wapi?
Na kama walifukua maiti ni kwanini wasiwarudishe kwenye makaburi yao?
Chuo cha kuweza kufanya kitu kama hicho hakifai;
kama kufungwa na kifungwe ili wakajipange upya.

Watu kila siku wanafariki mahospitalini sis..maiti nyingi tu kila leo zinatelekezwa na ndugu mahospitalini, viungo vingi tu vinakatwa kutoka kwa wagonjwa baada ya kuonekana vimepoteza kazi..haya yote yanatosha kabisa kuwa resources kwa kujifunzia na si kwamba hufukua maiti, ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa hawa watu wa tiba walichokosea ni namna tu ya kuzihandle baada ya kuzitumia.
 
Habari za mchana wanna jf, inasemekana kuwa vile viungo vilivyo kuwa vinapelekwa kumwagwa huko bunju vilitolewa IMTU chuo cha medicine kilichopo opposite na interchick. Ni mabaki ya miili inayotumiwa name wanafunzi was udaktari. Habari inafuatiliwa zaidi il I kupata ukweli.
 
kwahiyo nyinyi ndio mliodikia mwai kibaki kafa mkaleta uzushi wenu humu? ujinga mtupu.

nyinyi ndio mliosababisha Tanzania iwe ranked in top 10 poor iq's population.
v

vipi bado kauli yako no Hii Hui?
 
Ina maana hakuna wanafunzi wengine watakaosoma masomo hayo !!! Maana katika shule na vyuo vingine tena katika nchi masikini kama Tanzania teaching aids zilizoachwa na Wakoloni bado zinatumika!!! Iweje hizo teaching aids tena kwa ajili ya masomo ya udaktari zitupwe, halafu nyingine zikiwa bado mbichi kama zinatoa damu.

Hahahah,mkuu kila kitu kina wakati wake wa kutumika na hata ku-expire.Kuna haja gani ya kutumia Teaching-Aids mfululizo miaka 5/7,wakati zipo zingine?.Muda wake uliisha na zilitakiwa kubadilishwa ziletwe nyingine ama zitupwe kwenye tanuru kama ilivo kawaida.

Kwan mkuu hujasoma hata sayansi form2 ?.Zile chemicals zikikaa sana kuna wakati hata uchanganye vipi hafanyi reaction yoyote maana zimepitwa muda na zinahitaji kubadilishwa.Hiyo ni kawaida na sio mara ya kwanza kutokea sema mara zote huwa wanachoma katika tanuru sio kutupa hadharan kama hivi.
 
Hii ni HATARI kabisa. Vyovyote vile ila maiti za watu mia na hakukuwa na taarifa zozote eidha za kupotea watu au za mauaji? Hii kweli ni kitendawili. Labda walikuwaga wanakusanya maiti moja moja. Na je katika hizo maiti sijui kama kuna ambazo zinaonyesha zilijeruiwa ingawa kwenye picha zipo zinazoonekana kukwanguka ngozi kutokana na ukavu. Tusubiri taarifa za uchunguzi zitasemaje. Ila vyovyote vile, hii HAIKUBALIKI kabisa na wahusika WAPEWE ADHABU KALI.

Mkuu sio maiti zile,wala sio viungo halisi vya binadam.Ni teaching aids zinaitwa cadaver!.Yaan unatengenezwa mwil wa mtu kwa plastic ili kufundishia masomo ya udaktar katika vyuo.Hakukuwa na kiungo halis.
 
Viungo mbali mbali vya binadamu vimekutwa katika eneo la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika mazingira ambayo haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.
Kwa mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema viungo hivyo vya binadamu vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani ya mifuko.

[h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]



Hata pamoja na viungo hivyo pia vifaa vya upasuaji vimekutwa zikiwemo glovuzi.
Mtu mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.
Haijafahamika mara moja miili hiyo ya binadamu imetolewa wapi na ilipelekwa eneo hilo kwa lengo gani.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na mauaji ya walemavu hao.
 
Mkuu sio maiti zile,wala sio viungo halisi vya binadam.Ni teaching aids zinaitwa cadaver!.Yaan unatengenezwa mwil wa mtu kwa plastic ili kufundishia masomo ya udaktar katika vyuo.Hakukuwa na kiungo halis.

Mbona nimwjaribu ku google maana ya cadaver ni maiti iliyoifadhiwa kwa lengo la kutumika kwa mafunzo na sio plastic kama unavyotaka kutuaminisha mkuu
 
v

vipi bado kauli yako no Hii Hui?

kauli bado iko palepale pale the clear information nilizonazo ni viungo vya binadamu na wala sio maiti zaidi ya 100.

tuelewane kwanza, wapo wagonjwa wakisukari wanakatwa miguu hata mikono na bodaboda wengi pia hukatwa miguu.

hapa tunasubili sasa clear statement ya polisi na wizara ya afya why this? na ni nani anawajika au kuwajibishwa.
 
Back
Top Bottom