Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Ni maiti mbili tu zilizokuwa na vichwa, nyingine zote hazina vichwa. Kwa mujibu wa askari polisi walizochukua kuzipeleka muhimbili usiku wa leo, maiti zote zikiwemo zile zilizokuwa zinavuja damu hazitoi harufu. Nyingi zilikuwa zimekaushwa na zimekatwatwa vipande vipande. Kwa wale tunaofikiri zimetoka vyuo vya kufundisha madaktari, wana JF madaktari watueleze kama kweli miili ya kujifunzia hukatwakatwa vipande?

ni kweli hukatwakatwa, hizi ni cadavers zitakuwa zimetoka kwenye vyuo hapo Dar.....???? wahindi
 
Hao wataalam wanaosema hivyo ni wataalam wa nini labda? Cz haingii akilini hata kidogo kutupa maiti namna hiyo,bora hata wangezizika pamoja.
Labda maktari waje watuambie kuwa wakimaliza mafunzo yao kwa vitendo ndio wanatupa maiti majalalani kweli? kwanza kiafya ni hatari kwani magonjwa ya milipuko yanaweza zuka.

kikawaida baada ya mafunzo viungo vilivyo baki vinakua incinerated....pengine kuna chuo hapo Dar hakuna incinerAtor
 
Ni maiti mbili tu zilizokuwa na vichwa, nyingine zote hazina vichwa. Kwa mujibu wa askari polisi walizochukua kuzipeleka muhimbili usiku wa leo, maiti zote zikiwemo zile zilizokuwa zinavuja damu hazitoi harufu. Nyingi zilikuwa zimekaushwa na zimekatwatwa vipande vipande. Kwa wale tunaofikiri zimetoka vyuo vya kufundisha madaktari, wana JF madaktari watueleze kama kweli miili ya kujifunzia hukatwakatwa vipande?

Maiti zinazotumika kufundishia yaani cadaver hukatwa vipande vipande katika process yakujifunza muscles za mwili huo lakini kwenye swala la maiti hizo kuvuja damu nina mashaka kwamba hizo hazijatoka katika vyuo vya udaktari sababu cadaver huwa damu inakua imeganda kabisa na hazivuji damu maana zinakua zimekaa mda mrefu maana kigezo moja wapo cha maiti kutumika kama cadaver ni inatakiwa ikae mortuary sii chini ya wiki mbili bila kutambuliwa..wiki mbili zikipita ndio itaruhusiwa kutumika kujifunzia kwahyo swala la damu kuvuja linaleta mashaka
 
kuna uwezekano mkubwa hayo mabaki yametoka chuo cha IMTU coz ndo kipo jirani na maeneo ya bunju!! kwa daktari au mwanafunzi wa udaktar nadhan ameshatambua kabisa kwamba hzo ni cadaver
 
Hii inaonesha uzembe wa hali ya juu kabisa. Chuo kitakachobainika kiwajibike kwa hili. Hii ni kuonyesha ni namna gani taasisi za afya zimekua na uzembe hata katika kujali afya za watu. Kwa kawaida, hii miili(Cadaver) hutumika kujifunzia wanafunzi wa udaktari wa mwaka wa kwanza kwa somo liitwalo Anatomy na mabaki yote huchomwa. Kwa kawaida, hadi mwisho wa course miili huwa imekatwakatwa vipande kwani kira sehemu ya miili huwa imefukiwa. Na hii huwa mara nyingi ni miili ya watu wasiojulikana au wamekosa ndugu.
 
i think ni hivi vyuo vya wahindi wasiothamini chochote zaidi ya pesa tu... kila medical facility inayodeal na products za viumbe hai hassa binadamu inalazimika kuwa na system ya kuondoa hizo taka kwa kufukia viwango vilivyowekwa, where ni tanuri, kuhifadhi, kusafirisha na hata kufukia chini.... chuo au hospitali haitakiwi kupractice kama hivyo vitu havijafanyika

corruption imezaa dharau kwa kila required condition kwa tanzania

Tunadhani tu, ngoja tusikie uchunguzi utasemaje, isije ikawa mambo ya kishirikina ya kula nyama za watu!

Miafrika Ndivyo Tulivyo - Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
Jaman hata mimi nimezipata izo newz kutoka ktk blog ya jestina ni kweli ilo tukio limetokeaa
 
Mie nimepiga picha mwenyewe nashindwa kuziuppload

jamani hizo ni cadava zinazotumikaga vyuoni kufundishia first year. sema hicho chuo husika wameshindwa kuzidispose/incinerate ili zisilete shida. ukiangalia hizo nyama ni namna ambavyo huwa zinatenganishwa ili kujifunza misuli, mishipa ya damu, mifupa nk. Sema tanzania yetu watakuja na kauli za uongo uongo ili kuwaficha chuo kilichohusika. hawa wanatakiwa wachukuliwe hatua kali na dar kuna vyuo vitatu tuu Muhas, IMTU na Kairuki
 
Idadi hiyo imeokotwa ktk mifuko ya viroba......ni hali ya kusikitisha kwa kweli miongoni mwao wapo watoto.

========
UPDATE 1:

Kwa mujibu wa Radio One:
Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limekamata viungo mbalimbali vya binadamu vilivyohifadhiwa ktk mifuko ya plastiki ktk machimbo ya kokoto ya Bunju nje kidogo ya jiji la Dsm

Jamani tusalini sana. Mmesikia kilichotokea jioni hii huko Bunju. Bodaboda wamefanikiwa kuikatama Susuz Carry iliyokuwa na miili ya watu zaidi ya 20 idadi kubwa ikiwa ni wanawake. Wamegawanywa vipande vinne na miili yote haina ngozi. Kwa mujibu wa reporter wetu aliyopo kituo cha Usalama Bunju anasema inasadikika miili hiyo imetoka maeneo ya Inter chick ila dereva ni wa Bunju hivyo wanasubiri uongozi Wa Juu Wa Polisi ufike eneo la tukio. Eeh Mungu tunusuru Watoto wako🙏
 
nilielezwa na jamaa yangu nikadhani utani hadi nikamtukana..kumbe kweli.
 
mi mtu inawaza hela tu bila kujari utu yaani mtu anapewa gari akawamwage binadam wenzie dampo? Hivi kweli ni hapa Tanzania?
 
Back
Top Bottom