Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Nimeona picha za viungo husika. Kuna gloves na nyembe za upasuaji ambazo zimehifadhiwa pamoja na hivyo viungo. Japo sijui mazingira ya tukio, lakini ni muhimu pia kujua baadhi ya vyuo vya magonjwa ya tiba ya binadamu huwa vina dispose wapi mabaki ya cadavers wanazotumia...

Mkuu vyuo vina zaidi ya miaka 10 ..mfano muhimbili ni kikongwe sana ina maana leo ndio wamebadili utaratibu wa kutupa hizo cadavers!! tuache wafanye uchunguzi tu tutajua...lakini hii sio utu ss ni unyama tuwe na heshima kwa watu waliofariki hta km ni cadavers tuwahifadhi vzr si kutupatupa ovyo..
 
Pyongyang kuna internet ya kuwasiliana na outside world kweli??.
Ninashaka na kauli yako kuwa upo N Korea.

Are u two serious kweli?!!! This a shocking newz eti au nyie mmezoea newz kama hizi?!!!
 
very sory kwa ndugu na jamaa waliofiwa
hivi nchi yetu inaelekea wapi?
nimeona taarifa TBC1 juu ya jamaa mmoja amekamatwa anaenda kutupa mifuko zaidi ya 80, maeneo ya bunju akienda kutupa mifuko iliyojaa viungo vya binadam ikiwemo mafuvu mikono mapafu na mioyo.
hapo nikaanza kujiuliza hao jamaa wamekuwa wakiuwa watu wote hao bila kujulikana na inteligensia yetu?
where are we going? nahisi maisha yangu na yako wewe unayesoma hapa tu hatarini.

:embarrassed::embarrassed::embarrassed:
 
Hizi taarifa ni za kweli na picha ninazo pamoja na gari lililokamatwa na hiyo miili ya watu!hatuko salama watanzania!
 
Tanzania inatisha...
Dar ndo kabisaaa.
Kufa kupo ndio ila huu ukatili...mh
Nahisi kama kuna watu watavamia humu ndami kutuchinja.
Nimetishika kupita maelezo.
 
Well;
1. Surgical gloves , surgical blades, body parts (cut at joints???????), non-odourous, in plastic bags...of the same colour,size and material (institutional bulky procurement/consistence???!!!)

2. Hakuna nguo, vitambaa wala nylon aprons vyenye damu kuashiria kuwa watu hao waliuliwa na kulikuwa na utokaji wa damu "haemorrhage/exsanguination"?????????!!!!!!!

Sum the dots and sleep well!!!!!
 
hili ni tukio la aibu kwa nchi yetu inayosifika kwa amani na utulivu.
"Mungu, tunakwenda wapi??!?"
 
unajua mleta mada kaileta issue hii kimzamzaa wkt kama ni kweli ni kitu si cha masihara.atupe habari kamili au yeye naye kaambiwa

mtoa mada kaileta kama ilivyotolewa na vyombo vya habari. Si ITV wala TBC aliyetoa picha na kuiongelea kwa undani, tufuatilieni media ila habari ipo juu juu hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom