Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ebu funguka mkuu!
habari hii hainiingii akilini,mbona hizi picha zimepigwa mchana jamani au mimi chongoo?
Habari Wakuu.
Kwa habari zilizothibitika ni kwamba masalia ya viungo vya binadamu vilivyotupwa maeneo ya Bunju yametoka Chuo cha Udakatari IMTU kilichopo Mbezi Beach Dar baada ya wanafunzi kumaliza kuyatumia kwa mazoezi ya Practical (Cadaver).
Imekuwaje vikatupwa Bunju?
Kwa kawaida taka hatari kama hizi huwa zina mfumo maalum wa kuteketezwa kwenye tanuru (kuwa incinerated).
Kwa hiyo taka hizi walizipeleka Muhimbili kwa ajili ya kuteketezwa lakini hawakuwa na fedha za kulipia hivyo Muhimbili wakashindwa kuziteketeza kwenye tanuru maalum.
Baada ya hapo ndipo wakaamua kuja kumwaga maeneo ya Bunju.
My Take : Serikali sasa iamke kutoka usingizini sasa na ichukue hatua za haraka ikiwemo kuwachukulia hatua kale wale wote waliohusika na huu uzembe kwani ni hatari kwa mazingira na afya za watu.
Haingiii akilini eti IMTU walishindwa kulipa ndipo wakaamua kwenda kutupa jalalani viungo vya binadamu? hapana hapana bado sikubaliani na hili. Sidhani kama thamani ya binadamu imefikia hatua hii ya kutupwa kwenye jalala.
we umetumwa wewe izo maiti hazina ndugu majaribio na miili ya watu wachawi
sio ivo mkuu ii kitu umepost vipi yani imekuingiaje akilini...io haipo kabisaLabda kama umenituma wewe mkuu!
BREAKING NEWS: VIUNGO VYA BINADAMU VYANASWA VIKISAFIRISHWA
Tunaomba radhi kwa picha kama zinatisha.
Hivi ndivyo viungo vya binadamu vilivyokutwa kwenye mfuko usiku huu jijini dar es salaam!
Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba kuna gari zimenaswa likiwa limebeba shehena ya viungo vya binadamu maeneo ya bunju, dar es salaam.
Chanzo chatu ambacho ni whatsap kinasema kuwa viungo hivyo vilikuwa vimebebwa kwenye gari kama takataka vikiwa kwenye maroba madogo madogo na kutupwa kwenye jalala la takataka na dereva kufuata viungo vingine!
Hata hivyo kuna chanzo kingine kinadai kuwa miili hiyo ilikuwa inatumiwa na wafunzi madaktari wa chuo cha IMTU chilichoko Tanki Bovu Dar es es salaam.
Mmoja ya Kiungo cha Mguu
Baadhi ya Mifuko ambamo Maiti izo zilikuwa zimewekwa
Moja ya kichwa cha Binadamu ambacho kimetolewa katika moja ya Mifuko hiyo
Taarifa kamili itatolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam.
ndugu tukio limetokea usiku na ss hivi ni asubuhi je huo mchana unatoka wapiii,mwisho wa siku tusubiri uhalisia zaid kutoka kwa wahusika