Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Hili nalo litapita kimyakimya kama yalivyopita mengine.
 
kauli bado iko palepale
pale the clear information nilizonazo ni viungo vya binadamu na wala sio
maiti zaidi ya 100.

tuelewane kwanza, wapo wagonjwa wakisukari wanakatwa miguu hata mikono
na bodaboda wengi pia hukatwa miguu.

hapa tunasubili sasa clear statement ya polisi na wizara ya afya why
this? na ni nani anawajika au kuwajibishwa.

Unasema wahanga wa bodaboda na kisukari hukatwa viungo, Je! hivyo vichwa vilikuwa ni vyawagonjwa gani?
 
Ni kinyume na haki za binadamu,awajibike mtu asiwajibike ni ishara kuwa hata binadamu hai hana dhamani tanzania
Hili suala si dogo. Linahusu ubinaadamu wetu. Ile ni miili ya ndugu,jamaa na marafiki zetu.Hata kama ilikuwa ikitumika kisayansi,bado haikupoteza thamani yake kama ni miili ya binaadamu na hivyo heshima,staha na taratibu zilipaswa kufuatwa. Majibu kuhusu wapi imetoka miili ile ya Bunju hapa hayatakuwa na uzito bila ya kwanza kukubali kuwa kulikuwa na makosa juu ya kushughulika na miili ile.

Kwa majibu yoyote, hali ile haivumiliki. Iwe imetokea IMTU au kwingineko, yupo mtu au wapo watu wa kuwajibika. Hata kama ilikuwa ikitumika kisayansi,zipo taratibu za kushughulikia miili ile ikiwa ni pamoja na namna ya kuiteketeza.Mifuko ya rambo si namna ya kuiteketeza hata kama mimi si mwanasayansi. Kuitupa si jambo linalokubalika. Kwanza,kuitupa kiholela vile,kulihatarisha amani.Yangekosa mabomu ya Polisi,muda huu yangezungumzwa mengine.

Nitoe rai kwa wahusika wote wa sakata la jana la miili ya Bunju kujipima na kuwajibika. Tasnia yoyote ina miiko yake. Ya sayansi jana ilikiukwa. Yupo wa kuwajibika. Atambuliwe au ajitambue na kuwajibika haraka iwezekanavyo.
 
hapakuwepo na kiungo cha albino kweli ?
Bwashe!! Umetisha kweli. Umeshafikiria kupiga dili. Wenzako tunashangaa jinsi binadamu wenzetu walivyodhalilishwa baada ya miili yao kutumika kusomeshea madaktari, wewe umeona kuna fursa ya kupata mapene kwa Krismasi? Ufanye biashara ya kuuza viungo vya binadamu wenzako kwa ushirikina? We kweli intarehamwe!!
 
  1. The Interahamwe (Kinyarwanda, meaning "those who stand/work/fight/attack together" ) is a Hutu paramilitary organization. The militia enjoyed the backing of the Hutu-led government leading up to, during, and after the Rwandan Genocide.

    To be honest!, Now we have a similar situation here in Tanzania where this ill, corrupted, and infidel government trying to scare people to seek true democracy. they have little grip to stay on power before they slip away!

    God has judgement with them!
 
Duuuu hatari!isije. Kuwa hosp zetu hazina maeneo ya kuteketeza uchafu wa hosp.maana ktk hali ya kawaida viungo vya watu mia si mchezo.ngoja tuone
 
Kuna watu wanasema hii miili imetoka kadava muhimbili.
Hainiingii akilini. Kwanini wasifanye ivyo miaka yote waje wafanye ivyo now. Na je kadava si huwa wanakausha maiti. Hizi nyingi ni fresh na je kadava wanajifunza pia kuchuna ngozi ya binadamu na kukatakata viungo kama ndio watakuwa wauwaji sio waokoaji basi.

My take kuna haja ya sisi watanzania kuacha kuchukulia vitu easy. Ndio sababu hata perfomance ya serikali ni poor coz they know citizen cannot act upon anything but they will talk and 4get as usual.

This is serious case and bad image ever the world and our kids.

hizo ni cadaver mkuu,tunachuna ngozi,tunakata viungo....in short tunajifunza system zote....it all helps in saving life unapokuwa daktari.unapokuja kwangu unasema tumbo linauma mahala fulani etc mi tayari picha ya cadaver niliyopasua nikiwa chuo inakuja kichwani na inanisaidia kujua hapo unapoumwa kuna nini na kimekaaje na nikusaidiaje
 
Vyomnpo vya ulinzi na usalama wametoka kwemye misingi yao ya utendaji kazi wanapambana na vyama vya upinzani na kuomba rushwa.
 
Unasema wahanga wa bodaboda na kisukari hukatwa viungo, Je! hivyo vichwa vilikuwa ni vyawagonjwa gani?
Kuna watu wengine hujitolea miili yao itumike kwa ajili ya sayansi pale watakapokufa, huenda ndio vichwa vyao hivyo.
 
umenena vema kabisa kabisa!

QUOTE=Petro E. Mselewa;10129821]Hili suala si dogo. Linahusu ubinaadamu wetu. Ile ni miili ya ndugu,jamaa na marafiki zetu.Hata kama ilikuwa ikitumika kisayansi,bado haikupoteza thamani yake kama ni miili ya
binaadamu na hivyo heshima,staha na taratibu zilipaswa kufuatwa. Majibu kuhusu wapi imetoka miili ile ya Bunju hapa hayatakuwa na uzito bila ya kwanza kukubali kuwa kulikuwa na makosa juu ya kushughulika na miili ile.

Kwa majibu yoyote, hali ile haivumiliki. Iwe imetokea IMTU au kwingineko, yupo mtu au wapo watu wa kuwajibika. Hata kama ilikuwa ikitumika kisayansi,zipo taratibu za kushughulikia miili ile ikiwa ni pamoja na namna ya kuiteketeza.Mifuko ya rambo si namna ya kuiteketeza hata kama mimi si mwanasayansi. Kuitupa si jambo linalokubalika. Kwanza,kuitupa kiholela vile,kulihatarisha amani.Yangekosa mabomu ya Polisi,muda huu yangezungumzwa mengine.

Nitoe rai kwa wahusika wote wa sakata la jana la miili ya Bunju kujipima na kuwajibika. Tasnia yoyote ina miiko yake. Ya sayansi jana ilikiukwa. Yupo wa kuwajibika. Atambuliwe au ajitambue na kuwajibika haraka iwezekanavyo.[/QUOTE]
 
hizo ni cadaver mkuu,tunachuna ngozi,tunakata viungo....in short tunajifunza system zote....it all helps in saving life unapokuwa daktari.unapokuja kwangu unasema tumbo linauma mahala fulani etc mi tayari picha ya cadaver niliyopasua nikiwa chuo inakuja kichwani na inanisaidia kujua hapo unapoumwa kuna nini na kimekaaje na nikusaidiaje

so .......,!!???
 
Idadi hiyo imeokotwa ktk mifuko ya viroba......ni hali ya kusikitisha kwa kweli miongoni mwao wapo watoto.

========
mh! huu ni unyama mkubwa!
NIMEISOMA BBC, NIKAWAZA DUNIA INAITAZAMAJE TANZANIA NA AIBU HII KUBWA JAMANI?
SOMA HII:
22 July 2014 Last updated at 12:09 [h=3]Share this page[/h]




[h=1]Tanzania arrests over Dar es Salaam body parts dump[/h]
_76437916_tanzania2.jpg
The bags were dumped in a landfill site
Eight people from a Tanzanian medical institute have been arrested after 85 bags containing body parts were found in the port city of Dar es Salaam.
A police officer told the BBC that human limbs, fingers, ribs and skulls were in the bags, discovered in a landfill site in the Bunju suburb.
Some of the bags contained surgical instruments and used disposable gloves.
The BBC's Aboubakar Famau in Dar es Salaam says the find has shocked the usually quiet city.
Dar es Salaam police chief Suleiman Kova said those arrested have links to the city's Institute of Medical and Training University (IMTU).
Residents said they became suspicious after a truck repeatedly dumped black plastic bags weighing approximately 25kg (55lb) each.




------------------------



-------------------------

attachment.php


attachment.php



attachment.php
HAWA WANA HAKI KAMA MAREHEMU WENGINE LAKINI KWANINI KUFANYIWA HIVI?]
 
Taarifa za upelelezi zinaonesha kuwa kabla ya viungo kutupwa pale vilikuwa chuo na hospital ya IMTU!
 
  1. The Interahamwe (Kinyarwanda, meaning "those who stand/work/fight/attack together" ) is a Hutu paramilitary organization. The militia enjoyed the backing of the Hutu-led government leading up to, during, and after the Rwandan Genocide.

    To be honest!, Now we have a similar situation here in Tanzania where this ill, corrupted, and infidel government trying to scare people to seek true democracy. they have little grip to stay on power before they slip away!

    God has judgement with them!

So stupid and utter nonsense, hapa Interahamwe inakujakuja vipi?Tatito la propaganda zilizofanywa na RPF mpaka wakaonekana kama kilikuwa kikundi cha kigaidi kama Boko Haram ama Alishababu.Kumbuka Interahamwe lilikuwa tu jina la kuhamasisha maana hakukuwa na jinsi maana walikuwa wanapambana na wavamizi.Sasa tell me wewe hapa Interahamwe limekujakuja vipi kwenye hii issue ya watu waliokufa Dar na kupakiwa kwenye mifuko ya plastic nayo ndiyo Interahamwe
 
Mkuu sio maiti zile,wala sio viungo halisi vya binadam.Ni teaching aids zinaitwa cadaver!.Yaan unatengenezwa mwil wa mtu kwa plastic ili kufundishia masomo ya udaktar katika vyuo.Hakukuwa na kiungo halis.

Una idea ya taaluma ya udaktari hata kidogo tu? Yaani hata angalau ule upumbavu Wa udaktari tu? Chuo gani kinachotumia plastic hicho? Plastic inatoa damu? Si umesikia watu wanasema vipande vingine vilikuwa vibichi!! Sasa hayo ni maplastik gani hayo?
 
Kitendo hicho ni cha kinyama mno. Kokote kule huo mzigo ulikotoka walipashwa aidha wachome moto au wachimbe shimo wafukie sio kutupa namna ile ambapo wananchi tayari tumeona na tunajiuliza kulikoni? Ni heri wangeenda kwa mkiti serikali ya mtaa kuomba kibali cha kutupa taka zisizokuwa za kawaida ktk eneo lake!

Polisi watupe taarifa inayoeleweka.

Kama viungo hivyo vimetoka hospitali kwa nini wameviweka mpaka vikawa vingi kiasi hicho!

Ila kweli kama ni teaching aids kwa nini hawakuwashirikisha polisi ili kuweka mazingira bora ya kuihifadhi hiyo miili? Kama sisi tu pale SUA cadaver tunazihifadhi kwenye decomposition pits iweje hawa Wa binadamu wanashindwa kuwa na mazingira bora ya kuhifadhi miili ya binadamu? Sasa naanza kuamini kuwa madaktari Wa mifugo ni bora kuliko Wa binadamu! Mnakosaje utu kiasi hicho?
 
Huyo dereva namtafakari simpatii jibu...
Alilewa au hana akili nzuri??
Na hicho chuo kimeshapoteza hadhi kabisaaa
KIFUNGWE TU
Hili tukio limeleta athari kubwa sana kwa jamii... bado magazeti ya udaku yatakavyokuja kuvuruga zaidi

Mungu ibariki Tanzania[/QUOTE
Kifungwe alafu?tunahitaji madaktari.
 
Back
Top Bottom