deo paul555, GANZI, ni tatizo linaloashiria kukosekana kwa fahamu katika sehemu hizo. Hisia ndiyo inakosekana kwa sababu hakuna damu na neva zinakosa mawasiliano ya moja kwa moja na ubongo.
Ni jambo la kawaida linalowapata watu wengi sana katika miaka ya hivi karibuni, lakini pasipo kujua nini chanzo chake wala tiba.
Vyanzo vya ganzi mwilini
Vifuatavyo vinatajwa kuwa vyanzo vya ganzi mwilini mwa binadamu:
1. Shinikizo la muda mrefu.
2. Kuwa karibu na vitu vyenye baridi sana kwa kipindi kirefu.
3. Mabadiliko ya muda mfupi kwenye neva/mishipa.
4. Ajali kwenye neva.
5. Kunywa pombe kupita kiasi.
6. Uvutaji sigara na bangi.
7. Uchovu usioisha.
8. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo kila mara.
9. Ukosefu wa vitamini B12 na Magnesiamu mwilini,
10. Ugonjwa wa kisukari n.k
Kwa kawaida, ganzi inayotokea kwa dakika kadhaa na kupotea huwa haina shida yoyote.
Inaelezwa, ni vyema kuonana na daktari mapema ili kupata vipimo, iwapo ina kawaida ya kutokea kila mara na inadumu muda mrefu. Inaweza kuwa ishara ya ugonjwa fulani unaohitaji matibabu ya haraka.