kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu alisema serikali itapeleka mswaada wa Bima ya Afya bungeni ili uweze kujadiliwa. Wakati mchakato huo unaendelea Serikali kupitia Wizara ya Afya imependekeza viwango vya kulipia kwenye Bima.
Prof. Makubi amesema uchangiaji unaopendekezwa ni Sh. 340,000 kwa kaya ya watu 6 na Sh. 84,000 kwa mtu mmoja asiye na familia kwa mwaka.Kiwango hiki ukilinganisha na gharama za matibabu ni ndogo na serikali bado itafidia gharama nyingine.
"Sheria hii ya Bima ya Afya kwa wote inaenda kuwakomboa wananchi, inaenda kuhakikisha kila mwananchi, Mtanzania anakuwa na Bima ya afya, kwa sasa hivi takribani 15% tu ya wananchi wanabima za afya mbalimbali, inawaacha 85% ya Watanzania kutokuwa na uhakika wa kutibiwa".
Prof. Makubi amebainisha kuwa kwa wananchi watakaotambuliwa kutokuwa na uwezo wataendelea kupatiwa huduma kwa utaratibu utakaowekwa na Serikali kwa kila mtu kuwa na kadi yake ya Bima ya Afya.