Viwango vilivyopendekezwa na Serikali, Bima ya Afya kwa Wote

Viwango vilivyopendekezwa na Serikali, Bima ya Afya kwa Wote

Kulipa kwa mwezi hakuna aliyezuiliwa. Issue ni kuwa kuna watu hata ungeweka utaratibu gani hawana uwezo wa kulipa.
Ko unashauri nin kifanyike? Hapo inabidi labda uje na mada ya kuwakwamua hao watu ila sio kupiga kelele kusema ni gharama kubwa wakati ukiangalia kwa undani utaona hizo gharama ni za chini mno tena sanaa

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu alisema serikali itapeleka mswaada wa Bima ya Afya bungeni ili uweze kujadiliwa. Wakati mchakato huo unaendelea Serikali kupitia Wizara ya Afya imependekeza viwango vya kulipia kwenye Bima.

Prof. Makubi amesema uchangiaji unaopendekezwa ni Sh. 340,000 kwa kaya ya watu 6 na Sh. 84,000 kwa mtu mmoja asiye na familia kwa mwaka.Kiwango hiki ukilinganisha na gharama za matibabu ni ndogo na serikali bado itafidia gharama nyingine.

"Sheria hii ya Bima ya Afya kwa wote inaenda kuwakomboa wananchi, inaenda kuhakikisha kila mwananchi, Mtanzania anakuwa na Bima ya afya, kwa sasa hivi takribani 15% tu ya wananchi wanabima za afya mbalimbali, inawaacha 85% ya Watanzania kutokuwa na uhakika wa kutibiwa".

Prof. Makubi amebainisha kuwa kwa wananchi watakaotambuliwa kutokuwa na uwezo wataendelea kupatiwa huduma kwa utaratibu utakaowekwa na Serikali kwa kila mtu kuwa na kadi yake ya Bima ya Afya.
Nafikiri ni sahihi lakin serikali ijiandae kuxidiwa .vilevile kwa garama hiyo people wata afford
 
Unadhani Utapata kiasi gani cha kuweza kugharamia watanzania 60M+??
Tuuze ma V8 yoooteee nchi nzima na utolewe mwongozo wa kupiga marufuku matumizi ya hayo magari serikalini. Badala yake turudi kwenye RAV4, TOYOTA Hilux double cabin, Toyota Corolla & carina etc kulingana na ofisi husika na mazingira ya kazi.Malipo ya wabunge yapunguzwe by 30 to 40 % na baadhi ya vikao vifanyike kwa mtandao wakiwa majimboni mwa kwani wote walipewa tablets. Fedha zootee watakazo pata hapa zipelekwe kwenye hii bima ya afya kwa kila mtu. Hata hivyo kuchangia ni lazima kwa kila Mtanzania, ila viwango viangaliwe na kupunguzwa,huku serikali

Tuuze ma V8 yoooteee nchi nzima na utolewe mwongozo wa kupiga marufuku matumizi ya hayo magari serikalini. Badala yake turudi kwenye RAV4, TOYOTA Hilux double cabin, Toyota Corolla & carina etc kulingana na ofisi husika na mazingira ya kazi.Malipo ya wabunge yapunguzwe by 30 to 40 % na baadhi ya vikao vifanyike kwa mtandao wakiwa majimboni mwa kwani wote walipewa tablets. Fedha zootee watakazo pata hapa zipelekwe kwenye hii bima ya afya kwa kila mtu. Hata hivyo kuchangia ni lazima kwa kila Mtanzania, ila viwango viangaliwe na kupunguzwa,huku serikali ikitoa ruzuku kwenye huo mfuko.
 
Serekali irudishe ada kwa shule za secondary na itoe huduma za afya bure Ni Bora Mara Mia kuliko kijitibu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hivi unajua gharama za kuingiza madawa nchini na kuyasambaza kwenye mahospital na vituo vya afya?. Na una takwimu ya viwanda vingapi vya kutengeneza madawa ya binadamu nchini mwetu?. Sahau hilo na hakuna kitu kama hivyo istoshe kwa gharama hizo kuhusu bima serikali imejitahidi, swali ni kwamba utekelezaji na kumudu itawezekana??. Wewe kuhudumia wananchi si mchezo.
 
Mfano majuzi nilikuwa wilaya ya Uvinza, Kigoma huko, yaani mazingira yenyewe niliyoyaona huduma ya Bima ya afya ambapo unapata huduma zote kama Benjamin Mkapa Hospital ni mtihani mkubwa
Tukubar tukatae huwezi tumia bima mara zote ukiumwa maana saa nyingine umesafir umeacha bima unajikuta unaingia dispensary au duka la madawa kwa cash.
 
Hizo gharama mboa kubwa 84k Ni hela kubwa sioni Kama imekaa logically ya kuiita bima kwa wote mimi naomba hizo Bima watoe bure kwa kila Mtu regardless Ni civil servant or not naona hii program imekuwa kwa ajili ya kujipatia hela na sio kusaidiana wananchi a lot of shit and blunders
 
Kama una mtonyo bei ya kawaida sana sema ndiyo hivyo waTZ wengi tunaishi chini ya dola 1 kwahiyo ni mziki kupata 340k.
 
Tegemeeni packages za ajabu ajabu tu.

Vipimo kama CT Scans &MRI mtajilipia.

Dawa muhimu nyingi mtajinunulia tu.

Lengo la hii Bima liliwekwa wazi ni kuiokoa NHIF isijifie kutokana na kuwa taabani wala si kingine.
 
Hivi unajua gharama za kuingiza madawa nchini na kuyasambaza kwenye mahospital na vituo vya afya?. Na una takwimu ya viwanda vingapi vya kutengeneza madawa ya binadamu nchini mwetu?. Sahau hilo na hakuna kitu kama hivyo istoshe kwa gharama hizo kuhusu bima serikali imejitahidi, swali ni kwamba utekelezaji na kumudu itawezekana??. Wewe kuhudumia wananchi si mchezo.
Ujinga Mtu sisi tunakamuliwa tozo kibao then tutalipa Kodi TRA

Wao kutoa Huduma za Afya bure wanashindwa Nini ?

Kama Serikali inaweza kumsomesha Mtu bure from primary to form six how comes washindwe ku-toa free social services kwa wananchi wake wote nchi nzima

Hivi unafikiri ni idadi ngapi ya Watz wataweza kulipa. Hiyo 84 f
Ktk bima
 
Back
Top Bottom