Viwango vilivyopendekezwa na Serikali, Bima ya Afya kwa Wote

Viwango vilivyopendekezwa na Serikali, Bima ya Afya kwa Wote

Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu alisema serikali itapeleka mswaada wa Bima ya Afya bungeni ili uweze kujadiliwa. Wakati mchakato huo unaendelea Serikali kupitia Wizara ya Afya imependekeza viwango vya kulipia kwenye Bima.

Prof. Makubi amesema uchangiaji unaopendekezwa ni Sh. 340,000 kwa kaya ya watu 6 na Sh. 84,000 kwa mtu mmoja asiye na familia kwa mwaka.Kiwango hiki ukilinganisha na gharama za matibabu ni ndogo na serikali bado itafidia gharama nyingine.

"Sheria hii ya Bima ya Afya kwa wote inaenda kuwakomboa wananchi, inaenda kuhakikisha kila mwananchi, Mtanzania anakuwa na Bima ya afya, kwa sasa hivi takribani 15% tu ya wananchi wanabima za afya mbalimbali, inawaacha 85% ya Watanzania kutokuwa na uhakika wa kutibiwa".

Prof. Makubi amebainisha kuwa kwa wananchi watakaotambuliwa kutokuwa na uwezo wataendelea kupatiwa huduma kwa utaratibu utakaowekwa na Serikali kwa kila mtu kuwa na kadi yake ya Bima ya Afya.
Kwa hiyo kaya ya watu 2,3,4,5 nai watalingana uchangiaji n watu 6?

Hivi ni kweki hicho kiwango watu wote wanaweza kukilipa?

Hivi huko serikalini kuna watu au maroboti yanayoweka hivi viwango?
 
Inasikitisha sana viongozi wanaposhindwa kujua hali za wananchi wao. Tunayo maelfu ya kaya zisizoweza kumudu milo miwili kwa siku, unawaambia walipe hiyo pesa wataitoa wapi?

Na kwanini swala la bima ya afya liwe lazima?

Wanasiasa wetu wakiondoka duniani wanachokutana nacho kitakuwa kitisho kikubwa.
Swala la bima ni sawa likiwekwa lazima ila sasa hawa jamaa walishakosea hesabu tokea zamani.
 
Unaenda hospitalini, unapimwa malaria,unagundulika unayo dawa hakuna "Nenda duka la madawa, dawa zimeisha bado serikali haijaleta" .......MWEWE huyooo anaruka......
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hata mimi nawaza hivyo, kama tu ya watoto imewatoa jasho hii ndio itakuwa balaa kabisa.
Ni lazima italemewa halafu waanze zile style ya kuna shida ya network
Bima kwa wote ni siasa na ni ngumu sana kufanikiwa, kama kutoa tu vitambulisho vya nida serekali imeshindwa unategemea nin ni siasa tu na si kingine
 
Inasikitisha sana viongozi wanaposhindwa kujua hali za wananchi wao. Tunayo maelfu ya kaya zisizoweza kumudu milo miwili kwa siku, unawaambia walipe hiyo pesa wataitoa wapi?

Na kwanini swala la bima ya afya liwe lazima?

Wanasiasa wetu wakiondoka duniani wanachokutana nacho kitakuwa kitisho kikubwa.
Ni ngumu kutekeleza free health care kwasababu matibabu ni gharama. Ila angalau kwa bima ya 84,000 kwa mwaka itasaidia kupungaza mzigo wa gharama kwa raia
 
Sasa hili watu wa kipato cha chini wamudu wangeweka hiwe inalipwa kwa awamu au kwa mwezi
 
Ni ngumu kutekeleza free health care kwasababu matibabu ni gharama. Ila angalau kwa bima ya 84,000 kwa mwaka itasaidia kupungaza mzigo wa gharama kwa raia
Hakuna ugumu. Tatizo ni unaweka vitu gani kama vipaumbele vyako.

Huwezi kutanguliza ma V8 na kulipana posho ukawa na bakaa ya kuhudumia mambo mengine muhimu.

Once the cake is eaten, it's gone.
 
Inasikitisha sana viongozi wanaposhindwa kujua hali za wananchi wao. Tunayo maelfu ya kaya zisizoweza kumudu milo miwili kwa siku, unawaambia walipe hiyo pesa wataitoa wapi?

Na kwanini swala la bima ya afya liwe lazima?

Wanasiasa wetu wakiondoka duniani wanachokutana nacho kitakuwa kitisho kikubwa.
Unataka nani akutibia hata kama ni familiar hainakipato
 
Sijakupata, jaribu kuandika vizuri ueleweke.
Matibabu duniania kote ni gharam na ukifanya bure ndo utanyanyapaliwa mpaka ukome. Lazima utoe pesa ndo utibiwe .sasa kama huna hela nani unategemea akutibu
 
Matibabu duniania kote ni gharam na ukifanya bure ndo utanyanyapaliwa mpaka ukome. Lazima utoe pesa ndo utibiwe .sasa kama huna hela nani unategemea akutibu
Kuna pahala nimeandika kuwa sio gharama?
 
Back
Top Bottom