Viwango vilivyopendekezwa na Serikali, Bima ya Afya kwa Wote

Viwango vilivyopendekezwa na Serikali, Bima ya Afya kwa Wote

Inasikitisha sana viongozi wanaposhindwa kujua hali za wananchi wao. Tunayo maelfu ya kaya zisizoweza kumudu milo miwili kwa siku, unawaambia walipe hiyo pesa wataitoa wapi?

Na kwanini swala la bima ya afya liwe lazima?

Wanasiasa wetu wakiondoka duniani wanachokutana nacho kitakuwa kitisho kikubwa.
Huna akili,mmebakia kulaumu kila kitu Cha serikali,
 
Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu alisema serikali itapeleka mswaada wa Bima ya Afya bungeni ili uweze kujadiliwa. Wakati mchakato huo unaendelea Serikali kupitia Wizara ya Afya imependekeza viwango vya kulipia kwenye Bima.

Prof. Makubi amesema uchangiaji unaopendekezwa ni Sh. 340,000 kwa kaya ya watu 6 na Sh. 84,000 kwa mtu mmoja asiye na familia kwa mwaka.Kiwango hiki ukilinganisha na gharama za matibabu ni ndogo na serikali bado itafidia gharama nyingine.

"Sheria hii ya Bima ya Afya kwa wote inaenda kuwakomboa wananchi, inaenda kuhakikisha kila mwananchi, Mtanzania anakuwa na Bima ya afya, kwa sasa hivi takribani 15% tu ya wananchi wanabima za afya mbalimbali, inawaacha 85% ya Watanzania kutokuwa na uhakika wa kutibiwa".

Prof. Makubi amebainisha kuwa kwa wananchi watakaotambuliwa kutokuwa na uwezo wataendelea kupatiwa huduma kwa utaratibu utakaowekwa na Serikali kwa kila mtu kuwa na kadi yake ya Bima ya Afya.
safi sana lakini huduma ziboreshwe vituo vya afya
 
Unanunua kwa sababu unajua ukienda hospital wni gharama ila ukiwa na bima ni rahisi kwenda tena hospital za private kama Rabininsia, Kitengure n.k.
Kuna matatizo ya kiafya ukiwa huna bima utayatibu kwa home remedies ila ukiwa na bima utajikuta tu unakwenda hospital.
Sana mkuu,mm nilikuwa na bima yangu basi kila hospital hata pua ikijikwaluza nakwenda mahospital makubwa kuleta vurugu
 
Raia wengi wanaumwa malaria,wataona usumbufu kwenda hospitali.. Sema hili janga la magonjwa ya lifestyle ndiyo shida
Hilo janga unalosema ni huko mijini but kule vijijini waliko 80 % hakuna hiyo kitu
 
Bima ya Afya kwa wrote ni MCHONGO was kukusanya pesa za watu ili KULIPIA MADENI ya NHIF
 
Hivi hawa asilimia kama 28 wanaoishi chini ya dola 1.5 kwa siku wataweza kulipia. Fikiria wauza karanga wakina mama wadogo wadogo waponda kokoto wauza bagia nk.

Pili mtu atakuwa huru kwenda hospitali anayoitaka iwe binafsi au ya umma au watu watapigwa pini waende hospitali za umma tu tena ngazi ya chini kama vituo vya afya na zahanati. Ikiwa hivyo maana yake watu bado wataenda hospitali bora za binafsi kwa kujilipia licha ya kuwa watakuwa wamechangia kiasi hicho cha pesa bima

Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu alisema serikali itapeleka mswaada wa Bima ya Afya bungeni ili uweze kujadiliwa. Wakati mchakato huo unaendelea Serikali kupitia Wizara ya Afya imependekeza viwango vya kulipia kwenye Bima.

Prof. Makubi amesema uchangiaji unaopendekezwa ni Sh. 340,000 kwa kaya ya watu 6 na Sh. 84,000 kwa mtu mmoja asiye na familia kwa mwaka.Kiwango hiki ukilinganisha na gharama za matibabu ni ndogo na serikali bado itafidia gharama nyingine.

"Sheria hii ya Bima ya Afya kwa wote inaenda kuwakomboa wananchi, inaenda kuhakikisha kila mwananchi, Mtanzania anakuwa na Bima ya afya, kwa sasa hivi takribani 15% tu ya wananchi wanabima za afya mbalimbali, inawaacha 85% ya Watanzania kutokuwa na uhakika wa kutibiwa".

Prof. Makubi amebainisha kuwa kwa wananchi watakaotambuliwa kutokuwa na uwezo wataendelea kupatiwa huduma kwa utaratibu utakaowekwa na Serikali kwa kila mtu kuwa na kadi yake ya Bima ya Afya.
Kanuni ya msingi ya bima ya afya, wachangie wengi ila waumwe wachache hapo mfuko utakuwa stable.Changamoto yetu wengi wanakata bima tayari wanaumwa tena magonjwa makubwa na hivyo lazima mfuko uyumbe.Nashauri Watanzania tujenge tabia ya kuchangia bima ya afya hata kama hatuumwi ili kuwezesha mfuko huu wa bima ya afya uwe endelevu.Vinginevyo tutalaumu viongozi na mwishowe tufe
 
Inasikitisha sana viongozi wanaposhindwa kujua hali za wananchi wao. Tunayo maelfu ya kaya zisizoweza kumudu milo miwili kwa siku, unawaambia walipe hiyo pesa wataitoa wapi?

Na kwanini swala la bima ya afya liwe lazima?

Wanasiasa wetu wakiondoka duniani wanachokutana nacho kitakuwa kitisho kikubwa.
Hili jambo lingekuwa la hiari tuu na waruhusu kuwe na ushindani wa hizi bima za afya kwa watu ambao siyo waajiriwa. Then watoe elimu ili watu waanze kuvutiwa na kujiunga wenyewe. Kuna wakulima mtu anavuna gunia 30 za mahindi,au mpunga na gunia moja ni laki moja sasa hivi hivyo wanaweza kulipa hiyo laki 3 au 4 kwa mwaka kwa familia. Pili hii ya mtu mmoja elfu 80 iwekewe utaratibu kiasi kwamba mgonjwa akifikushwa hospital aweze kulipia na kupata risiti ili aendelee na huduma wakati mengine yakifuata.
 
Inategemea, labda nikitoka nje tu ya nyumba ndo naiona aghakan hii hapa ndo nikiumwa naenda, lkn asilimia kubwa hoptl kubwa na zinazotumia bima huwa mbali na makazi kwa hiyo kichwa kinauma nipande bus wakati naona duka la dawa hili naliona naweza kupata flagile tumbo likatulia.
Bima kwa wote maana yake kumbuk mpaka wa vijijin pia
Mfano majuzi nilikuwa wilaya ya Uvinza, Kigoma huko, yaani mazingira yenyewe niliyoyaona huduma ya Bima ya afya ambapo unapata huduma zote kama Benjamin Mkapa Hospital ni mtihani mkubwa
 
njoo na alternative.
Tuuze ma V8 yoooteee nchi nzima na utolewe mwongozo wa kupiga marufuku matumizi ya hayo magari serikalini. Badala yake turudi kwenye RAV4, TOYOTA Hilux double cabin, Toyota Corolla & carina etc kulingana na ofisi husika na mazingira ya kazi.Malipo ya wabunge yapunguzwe by 30 to 40 % na baadhi ya vikao vifanyike kwa mtandao wakiwa majimboni mwa kwani wote walipewa tablets. Fedha zootee watakazo pata hapa zipelekwe kwenye hii bima ya afya kwa kila mtu. Hata hivyo kuchangia ni lazima kwa kila Mtanzania, ila viwango viangaliwe na kupunguzwa,huku serikali ikitoa ruzuku kwenye huo mfuko.
 
Inasikitisha sana viongozi wanaposhindwa kujua hali za wananchi wao. Tunayo maelfu ya kaya zisizoweza kumudu milo miwili kwa siku, unawaambia walipe hiyo pesa wataitoa wapi?

Na kwanini swala la bima ya afya liwe lazima?

Wanasiasa wetu wakiondoka duniani wanachokutana nacho kitakuwa kitisho kikubwa.
Ushawahi umwa au uguza kwa muda mrefu? At least mwezi ?

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Mtu hata unashindwa kujua hawa binadamu wana vitu gani vichwani mwao.

Na kila siku yanaingia makanisani na misikitini.
Wew unapendekeza kiwango kiwaje? Au utaratibu wa bima uwaje ili kuwaondolea mzigo wananchi wa gharama kubwa za matibabu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom