Viwango vilivyopendekezwa na Serikali, Bima ya Afya kwa Wote

Huna akili,mmebakia kulaumu kila kitu Cha serikali,
 
safi sana lakini huduma ziboreshwe vituo vya afya
 
Sana mkuu,mm nilikuwa na bima yangu basi kila hospital hata pua ikijikwaluza nakwenda mahospital makubwa kuleta vurugu
 
Raia wengi wanaumwa malaria,wataona usumbufu kwenda hospitali.. Sema hili janga la magonjwa ya lifestyle ndiyo shida
Hilo janga unalosema ni huko mijini but kule vijijini waliko 80 % hakuna hiyo kitu
 
Bima ya Afya kwa wrote ni MCHONGO was kukusanya pesa za watu ili KULIPIA MADENI ya NHIF
 

Kanuni ya msingi ya bima ya afya, wachangie wengi ila waumwe wachache hapo mfuko utakuwa stable.Changamoto yetu wengi wanakata bima tayari wanaumwa tena magonjwa makubwa na hivyo lazima mfuko uyumbe.Nashauri Watanzania tujenge tabia ya kuchangia bima ya afya hata kama hatuumwi ili kuwezesha mfuko huu wa bima ya afya uwe endelevu.Vinginevyo tutalaumu viongozi na mwishowe tufe
 
Hili jambo lingekuwa la hiari tuu na waruhusu kuwe na ushindani wa hizi bima za afya kwa watu ambao siyo waajiriwa. Then watoe elimu ili watu waanze kuvutiwa na kujiunga wenyewe. Kuna wakulima mtu anavuna gunia 30 za mahindi,au mpunga na gunia moja ni laki moja sasa hivi hivyo wanaweza kulipa hiyo laki 3 au 4 kwa mwaka kwa familia. Pili hii ya mtu mmoja elfu 80 iwekewe utaratibu kiasi kwamba mgonjwa akifikushwa hospital aweze kulipia na kupata risiti ili aendelee na huduma wakati mengine yakifuata.
 
Mfano majuzi nilikuwa wilaya ya Uvinza, Kigoma huko, yaani mazingira yenyewe niliyoyaona huduma ya Bima ya afya ambapo unapata huduma zote kama Benjamin Mkapa Hospital ni mtihani mkubwa
 
njoo na alternative.
Tuuze ma V8 yoooteee nchi nzima na utolewe mwongozo wa kupiga marufuku matumizi ya hayo magari serikalini. Badala yake turudi kwenye RAV4, TOYOTA Hilux double cabin, Toyota Corolla & carina etc kulingana na ofisi husika na mazingira ya kazi.Malipo ya wabunge yapunguzwe by 30 to 40 % na baadhi ya vikao vifanyike kwa mtandao wakiwa majimboni mwa kwani wote walipewa tablets. Fedha zootee watakazo pata hapa zipelekwe kwenye hii bima ya afya kwa kila mtu. Hata hivyo kuchangia ni lazima kwa kila Mtanzania, ila viwango viangaliwe na kupunguzwa,huku serikali ikitoa ruzuku kwenye huo mfuko.
 
Ushawahi umwa au uguza kwa muda mrefu? At least mwezi ?

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Mtu hata unashindwa kujua hawa binadamu wana vitu gani vichwani mwao.

Na kila siku yanaingia makanisani na misikitini.
Wew unapendekeza kiwango kiwaje? Au utaratibu wa bima uwaje ili kuwaondolea mzigo wananchi wa gharama kubwa za matibabu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…