Plot4Sale Viwanja vinauzwa Dodoma Mjini

Hivo viwanja si ndo vyenye mgogoro na Manispaa? Si ndo wenye eneo wameingizwa chaka?

Ngoja niishie hapa
Hapana, tukihitaji kuuziana unaenda kukagua ili ujiridhishe, hakuna mgogoro wowote na wala haujawahi kutokea hapa
 
Hapana, tukihitaji kuuziana unaenda kukagua ili ujiridhishe, hakuna mgogoro wowote na wala haujawahi kutokea hapa
Mbona unaelekezea tu umbali kwa sq na km kutoka sehemu maarufu?

Wewe sema ni D/ makulu?, ng'ong'ona?, ntyuka? Au nzuguni? N.k
 
Vya kuambiwa changanya na zako we ungenunua tu utakayo ya kuta utapambania tu.

Hapana mkuu we nunua tu,, litalotokea utapambania tu ila ukae chonjo.
Utapambania vipi Mkuu? Unaujua mziki wa kununua kiwanja chenye mgogoro wewe au unausikia tu?
 
Utapambania vipi Mkuu? Unaujua mziki wa kununua kiwanja chenye mgogoro wewe au unausikia tu?
Rejea maada nilizozijibu hapo juu mkuu, napenda kutangaza biashara ambayo nina uhakika nayo, ndiyo maana kabla ya biashara mteja unajiridhisha kote then tunafanya biashara
 
Unapaswa kudhibitisha kwa vielelezo kuwa sio kweli,
Okay, uthibitisho wangu mkubwa ni kwamba yale maeneo yamepimwa juzi tu kwahiyo ni viwanja vipya, Dodoma viwanja vilivyopata migogoro ni vile ambavyo vilipimwa na CDA kwani CDA hawakulipa Fidia kwa watu ambao maeneo yao yalitwaliwa na hao CDA wakasababisha mgogoro kwa watu. Ila haya maeneo yaliyopimwa kipindi hiki cha manispaa kukabidhiwa ishu ya ardhi viko salama kabisa, kuweni na amani ndugu zangu Watanzania
 
Asante kwa ufafanuzi
 
vina hati? bila hati ni kimeo pale manispaa kuna wafanyakazi mashetani hati ni mbinde kichizi
 
Tatizo kupata hati kimbembe...pale manispaa kuna wafanyakazi washenzi washenzi sana..sina hamu kabisa
 
Tatizo kupata hati kimbembe...pale manispaa kuna wafanyakazi washenzi washenzi sana..sina hamu kabisa
Suala la hati tutakusaidia kuondoa kusumbuliwa, tuachie jukumu hilo tutakubaliana kwenye mikataba kuhakilisha unapata hati yako,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…