Viwanja vya makazi vinaongezeka ila mashamba yanapungua

komasalonde

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
2,742
Reaction score
3,523
Sijui kama naliona vibaya jambo hili. Kila mahali mahitaji ya viwanja vya makazi yanongezeka kwa kadi hasa kwa sababu ya idadi ya watu kuongezeka. Mahala palipokuwa mashamba katika Majiji, miji, Wilaya, vijiji na vitongoji leo ni makazi, viwanda shule, vyuo nk. Miaka kama 50 ijayo sijui hali ya chakula itakuwaje kama hayatatengwa maeneo ya Kilimo cha kimkakati.
 
Itoshe tu kusema wewe hujatembea wala huijui Tanzania.

Dar tu yenyewe bado ina mapori.
 
Wapi huko?
 
Itoshe tu kusema wewe hujatembea wala huijui Tanzania.

Dar tu yenyewe bado ina mapori.
Labda hajafika Kigamboni huyo.

Kibada,kisarawe2,Mwasonga,Magodani,Kigobedi Pemba mnazi huko ni Dar na kuna mapori ya kutosha.
 
Sasa si ndio Chaka huko
Unataka kiwanja Kinyerezi kwa bei hiyo?

Watanzania somo la hesabu limetushinda shule mpaka darasani.

Soma hesabu za Wahindi na Waarabu kwa nini wanakaa mjini?

Nunuwa kiwanja Kinyerezi kwa millioni 20 kama uwezo unao utaokowa sana gharama za kujenga mbali kwa kudhani kiwanja cha bei rahisi ndio umejikombowa, calculate kilometer na muda, na kwa siku utatumia pesa kiasi gani kwenda kwenye movement zako na kurudi.

Mimi kutoka kwangu kwenda town ni jero tu kwa daladala, boda haizidi buku tatu, nina hesabu za kihindi kwenye kuselect residential.
 
Labda hajafika Kigamboni huyo.

Kibada,kisarawe2,Mwasonga,Magodani,Kigobedi Pemba mnazi huko ni Dar na kuna mapori ya kutosha.
Mwaka 1983 Kariakoo ilikuwa na nyumba za makuti na mwenge, Tegeta huko ilikuwa ni mapori. Leo ikoje wakuu. Kila jiji, mji iko hivyo hivyo. Arusha Seliani ilikuwa pori leo ikoje ? Dodoma kilometa 50 Kuzunguka mji ni viwanja tupu. Nadhani ipo haja kulitazama vinginevyo sisi hatutakuwepo ila wajukuu na vitukuu vyetu
 
Hayo maeneo.yalikuwa yanalimwa? Au wanafyeka mapori na kupima viwanja
 
Sahihi kabisa mkuu,kama mbeya hapa hakuna shamba hata moja🥴
Tunaposema Tanzania ina mapori ya kutosha, wakati ardhi inauzwa kama njugu, tutakuwa tunajifungia kufikiri. Ni sawa na walisema miaka ya 1970 na 1980 kuwa barabara za Dsm ni Pana na zinatosha. Vipi leo ikoje?? Wenye kuwaza mbele hujua na kubaini idadi ya watu na ardhi isiyo zaa, bali kupungua. Maeneo ya viwanda, makazi, mashamba, mifugo taasisi nk. Ila tukibakia na kauli huyu hajatembea sijui wapi wapi Mapori yapo. Haya. Hayo mapori kaulize utaambiwa hili la waziri nani nani hopa kwa Rais mstaafu yule nk
 
Unataka kiwanja Kinyerezi kwa bei hiyo?

Watanzania somo la hesabu limetushinda shule mpaka darasani.

Soma hesabu za Wahindi na Waarabu kwa nini wanakaa mjini?

Nunuwa kiwanja Kinyerezi kwa millioni 20 kama uwezo unao utaokowa sana gharama za kujenga mbali kwa kudhani kiwanja cha bei rahisi ndio umejikombowa, calculate kilometer na muda, na kwa siku utatumia pesa kiasi gani kwenda kwenye movement zako na kurudi.

Mimi kutoka kwangu kwenda town ni jero tu kwa daladala, boda haizidi buku tatu, nina hesabu za kihindi kwenye kuselect residential.
Ndio maana nikakuambia utapata huko Chaka sio karibu na town
 
Mwaka 1983 Kariakoo ilikuwa na nyumba za makuti na mwenge, Tegeta huko ilikuwa ni mapori. Leo ikoje wakuu. Kila jiji, mji iko hivyo hivyo. Arusha Seliani ilikuwa pori leo ikoje ? Dodoma kilometa 50 Kuzunguka mji ni viwanja tupu. Nadhani ipo haja kulitazama vinginevyo sisi hatutakuwepo ila wajukuu na vitukuu vyetu
Jiulize kwanini haitokei kariakoo nyingine usikariri sehemu inaweza kuwa pori mpaka vitukuu vikafa
 
Tunaposema Tanzania ina mapori ya kutosha, wakati ardhi inauzwa kama njugu, tutakuwa tunajifungia kufikiri. Ni sawa na walisema miaka ya 1970 na 1980 kuwa barabara za Dsm ni Pana na zinatosha. Vipi leo ikoje?? Wenye kuwaza mbele hujua na kubaini idadi ya watu na ardhi isiyo zaa, bali kupungua. Maeneo ya viwanda, makazi, mashamba, mifugo taasisi nk. Ila tukibakia na kauli huyu hajatembea sijui wapi wapi Mapori yapo. Haya. Hayo mapori kaulize utaambiwa hili la waziri nani nani hopa kwa Rais mstaafu yule nk
Kuna vijiji mpaka leo ukiwa mwanakijiji unapewa shamba la kijiji kwa lazima na ni lazima ulime, usipolima unashtakiwa.

Tanzania tuna shida zingine siyo ardhi, wenye shida ya ardhi ni Wakenya.
 
Back
Top Bottom