Pre GE2025 Viwanja vya Mwembetogwa Iringa mjini Mchungaji Msigwa afunguka sababu 4 za kuondoka CHADEMA

Pre GE2025 Viwanja vya Mwembetogwa Iringa mjini Mchungaji Msigwa afunguka sababu 4 za kuondoka CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Pigilia misumali ufipa mpaka wakose usingz LEO, chadema syo chama Cha siasa ni mradi wa mbowe,
fukia chadema mitaa yote ya semtema na wilolesi kote
MSIGWA HOYEEE
Leo yeye ndio kajimaliza. Sidhani kama atapews microphone.
 
Yaani cdm imalizwe na Msigwa aliyesema akihamia ccm nyumba yake ichomwe moto? Huyo Msigwa namfananisha na wale watu wanaobebeshwa unga, a.k.a punda. Ccm wanamtumia hadi wanaishia kumchora. Hicho kizazi cha kuelewa hizo porojo za Msigwa kinatoka wapi?
Inaonyesha unaumia Sana mbona umepaniki. Atawamaliza mpaka presha ziwapande, Lazima mudate
 
Mkuu ondoa hyo DP.
Chadema sahz haina mwenyekiti aliyopo muda wake umeisha, apishe uchaguzi wa Mwenyekiti mwngne
Tuwe na subira mkuu. Nitaitoa siku Mbowe akitangaza kugombea uwenyekiti Tena, maana atakuwa ameniudhi kupita kiasi.
 
Mazingira ya taharuki wanazoleta CHADEMA ni hatari kwa Usalama wa Taifa hili.

Nitachukua tahadhari za Msigwa na kuziweka moyoni.

Nitachagua kwa umakini 2025.
=========

CHADEMA isajiliwe kama NGO ama chama cha Wanaharakati tu.
 
Kama unaamini kuwa CHADMA ni Chama cha Siasa basi karibu umsikilize mchungaji Msigwa atakavyokuprove wrong.

Mchungaji Msigwa anaijua CHADEMA nje ndani na ametuomba wana CCM tuamini anayosema kwa sababu yeye ni mtumishi wa Mungu.

Karibuni sana na mkutano utarushwa mubashara na Vyombo mbalimbali vya habari vya Kitaifa na Kimataifa kwani hata BBC wameonekana.

Sabato Njema 😄


Hoja za Livingstone Lusinde
"CCM na vyama vya upinzani ni kama babu na mjuu, hakuna ugomvi kati yao. Mjukuu anaweza kucheka anavyotaka na mjukuu wake, kama babu ana mapengo mjukuu anaweza kuingiza mpaka vidole kwenye mapengo yake, babu anacheka hana shida, anacheka na mjukuu wake

"Mjukuu akishika (sehemu za siri) lazima ale kofi. Kwahiyo wao wacheze na mikutano ya hadhara, waimbe nyimbo zao lakini ikifika kwenye uchaguzi wa kijiji, diwani, ubunge na Urais watoe mikono.

"Huawezi kuruhusu mjukuu wako afikir kiwango hicho!"

Msigwa Apanda Jukwaani
Mchungaji ameanza kwa kukabidhi kadi 15 za Wanachama wa CHADEMA waliohamia CCM ambao pia wamepanda Jukwaani na kupewa mavazi ya CCM.

Sehemu ya Hotuba ya Mchungaji Msigwa
Nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyekiti wa Chama na Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kunipokea niwe Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi. Pia nawashukuru viongozi wote wa Mkoa na Wilaya kunikaribisha kuwa miongoni mwenu.

Kwakuwa muda umeenda naomba niwashukuru wale wote walionisemea vizuri kwenye Jukwaa hili.

Nianze kwa kusema uamuzi wangu wa kuhama CHADEMA, chama ambacho nimekitumikia zaidi ya miaka 18 haukuwa rahisi, ulikuwa ni mgumu lakini ni uamuzi sahihi. Uamuzi huu umezaa makundi matatu:

1. Wako ambao wamefurahi wamenishangilia na wamenitumia mseji za kunipongeza nawashukuru sana.​
2. Wapo ambao wamechukia wamenitukana na wamenitumia meseji za matusi ninawashukuru sana.​
3. Wapo ambao wapo confused​
Nina matumaini nitakapomaliza kuzungumza hapa wale waliofurahi watafurahi zaidi na yamkini wale walionichukia na kunitukana watanielewa na natumai wale walio confused watapata majibu wataamua wanichukie au waniunge mkono. Kwahiyo kwakuwa wote ni Watanzania na wote tunajenga nyumba moja ninaamini mtanisikiliza vizuri lakini naomba muelewe ni Msigwa yuleyule mwenye akili ileile. Sijaruka mental nimeyachukua maaamuzi haya baada ya tafakuri ya kina.

Wakati ule nimetoka TLP wengi mliniunga mkono, lakini CHADEMA kiliaminisha vijana wakati ule nilikuwa fresh nikiwa nimetoka Afrika Kusini. Kiliaminisha vijana wengi wakati ule walikuwepo wakina Zitto, Halima Mdee waliaminisha kuwa chama hiki ni chama chenye misingi ya haki, uhuru, demokrasia na maendeleo na muda mwingi walionesha udhaifu wa CCM. Vijana wengi walishawishiwa wakajiunga na chama.

Aeleza sababu za kuondoka CHADEMA:
Nataka nizungumze vitu vinne vya kwanini nimetoka CHADEMA:

CHADEMA tumekuwa tukilalamika serikali ya CCM haina Demokrasia, inaua demokrasia, kitu cha kwanza kilichonitoa ni CHADEMA wana maneno mazuri sana kwa nje lakini kwa ndani uozo mkubwa sana. Chadema ukiwasikia kwa maneno ni malaika lakini kwenye vikao na matendo ni shetani. Wengine wanasema Msigwa umeshatoka chadema sasa usiwaseme seme.

Mbowe anaruka na Helikopta kuwaambia Watanzania Serikali ya Rais Samia ni mbaya ichaguliwe CHADEMA. Huyu ni mtu anayetaka apewe nchi, apewe uamiri jeshi Mkuu huyu ni mtu anataka IGP awe chini yake huyu ni mtu anataka Usalama wa Taifa uwe chini yake tusimseme, lazima tumseme tumjue ana tabia gani, tumfungue kwapa tuone ana sifa hizo, ni kweli anaweza akapewa nchi

Leo navyozungumza ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia na nitatoa sababu. Toka miezi mitatu ndani ya CHADEMA kumepasuka vipande viwili kimoja kipo kwa Mnyika kingine kwa Kigaila. Kigaila alipewa maagizo kuwa hakikisha unavuruga uchaguzi wa Kanda ya Nyasa ntakupa ukatibu Mkuu na Mrema utakuwa Naibu Katibu Mkuu. Mnyika alivyoona hivyo naye amesusa hata ofisini haendi.

Anayesababisha ni Mwenyekiti wa Chama. Mwenyekiti wa Chama alitoa maagizo chama chetu kina katba inasema uongozi wa ngazi ya chini unasimamiwa na ngazi ya juu. Mbowe sababu anataka madaraka aliunda kitukinaitwa Oparesheni wakaundwa watu wanaitwa zonal oparational manager wanateuliwa huko Dar wanaletwa wao ndiyo wanasimamia uchaguzi kinyume na utaratibu. Wamevuruga uchaguzi Tanzania nzima, ninavyosema hivi CHADEMA wananielewa.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Chadema ni chama kubwa

kama inaongozwa nchi Uzi mrefu namna hii
Siyo kawaida

Bwashee tuna matatizo mengi kama nchi juzi kati leaks katutonya kuwa hazina imekauka ndo maana hata kulipa mishahara ni shida

Kwa hiyo chadema na mambo yake si kipaumbele kwa sasa
 
Back
Top Bottom