Viwanja vya starehe na burudani vilivyovuma sana ila leo havipo tena

Mwanza
Tivoli Cinema
Liberty Cinema
Deluxe discotheque
Magnum DISCOTHEQUE
Capri Cabana club -Capri point

Dodoma
Dodoma cinema
Paradise CINEMA
NK Discotheque
Hivi paradise hotel ndo hapo karibu na TRA? (Kuna kipindi nilipita Dom nikakuta Kuna jengo linajengwa). Maana nachanganya whichi is which kati ya Dodoma Cinema na Paradise cinema ambayo moja ndio baadae ikawa ukumbi wa NK Discotheque. Tulikuwa tunatimba enzi za utoto enzi zile picha za kihindi za kina Mithun
 
yeah, you're right
 
Yenu bar & Sisimizi bar Ubungo
Sisimizi bar ubungo njia panda ya kwenda udsm, Yenu ubungo mataa, watu wa wizara ya maji kabla hawajahama wanaitambua vyema ilikuwa na misosi poa sana. Karambezi bar ubungo kibo karibu na kanisa la ufufuo/gwajima, kihedu bar ubungo kibo, alikuwa akipiga hapo Dr Remy ongala.
 
Wapi wapis ilikuwa moto. Kipindi hicho bendi zinapiga pale. Hivi DDC Kariakoo haipo tena? Hivi maeneo ya Ubungo si kulikuwa na bar inaitwa White House?
 
Killy Night club Shekilango
 
Wewe umeishi sana dar,na umeishi kiduuchu pale mbeya. Ntarudi kuongezea viwanja
 
Lango la Jiji
Madoto Bar
Silent Inn
Mbalamwezi
Escape one
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…