Kuna thread nimeona unapewa elimu ya uhalisia sana kuhusu huu mgogoro lakini huelewi... Potelea mbali watu kama nyinyi inatakiwa mjifunze kwenye matendo kama ilivyo sasa.
Urusi aliweka wazi matakwa yake ila NATO wakawa wanamtishia eti mara wamepeleka silaha hatari Ukraine, mara watamsaidia kijeshi, mara watampa kila msaada unaohitajika... Leo hii mwanaume Putin anaongea kivitendo zaidi huku wale makuwadi wa Magharibi wakijifungia ndani eti wanawaombea waukrine juu ya madhila yatakayowapata.
Victoire naomba utafute historia ya Urusi kabla ya vita vya kwanza vya dunia, vya pili na mpaka kuvunjika USSR ndipo uweze kuelewa maswala mengi ya dunia