Vodacom Premier League Lipuli FC 1-1 Simba SC, Uwanja wa Samora Mkoani Iringa

Vodacom Premier League Lipuli FC 1-1 Simba SC, Uwanja wa Samora Mkoani Iringa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League (VPL), kuendelea leo katika uwanja wa Samora Mkoani Iringa ambapo Lipuli FC Wanapaluhengo, wakiwa nafasi ya 8 kwa alama 31, wanawakaribisha vinara Simba Sports Club Wekundu wa Msimbazi. wenye alama 58 katika msimamo wa VPL

Simba SC chini ya Kocha Lechantre itamkosa kiungo Jones Mkude kwa kuwa kadi za njano lakini amesema kamwe hawapumzishi Straika wake Emmanuel Okwi na John Bocco kwa kuhofia Yanga kwani lengo ni kujimarisha kileleni ili kutwaa ubingwa.

Kwa upande wa Lipuli FC chini ya Seleimani Matola na Amri Said wamesema watafanya kila liwezalo kuhakikisha wanavunja mwiko wa Simba SC kutofungwa.

Mechi ya mzungumko wa kwanza timu hizi zilitoka sare 1-1, Leo itakuwaje? Usikose ukaambiwa kaa nasi usiende mbali. Kumbuka Azam Sports 2 watakuwa mubashara, huku TBC Taifa ikipeperusha matangazo hayo kwa njia ya redio kuanzia saa 10:00 jioni.

==> Vikosi vya timu zote mbili tukianza na wenyeji wa mchezo Lipuli FC

Mohamed Yusuph, Steve Mganga, Paul Ngelema, Ally Mtoni, George Owino, Fred Tangalo, Daluwesh Saliboka, Mussa Nampaka, Adam Salamba, Malim Busungu, Seif Karihe

Sub; Fadhil Butam, Omega Same, Moka Shaban, Lambeka Jerome, Samwel Mkomola, Martin Kazila, Zamoyoni Pangapanga.


IMG_20180421_074503_571.jpg
IMG_20180421_125448_856.jpg


==> Vikosi vinaingia uwanjani tayari kuanza kwa mtanange huu wa VPL

Lipuli FC wakiwa na jezi zao rangi nyekundu kama wenyeji na Simba SC wakiwa wamevaa jezi nyeupe kama wageni.

Timu zinakaguliwa pamoja na kupiga picha za kumbukumbu. Na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi inatolewa kwa Adam Salamba wa Lipuli FC

00' Naam mpira umeanza uwanja wa Samora katika mchuano wa VPL

Anakwenda kwake Okwi anamtafuta Kichuya.. Ni mpira wa kuelekea Lipuli FC

02' anapiga Okwiiii, laa laa mpira unatoka nje lango.

04' Lipuli anaanza shambulizi lao la kwanza nakupiga mpira ulitoka nje na kuwa Goal Kick

Okwi anakotroo kwake Kichuyaaa lakini wanakaa vema mabeki wa Lipuli FC

10' Lipuli FC 0-0 Simba SC uwanja wa Samora mkoani Iringa mtanange wa VPL

15' mashabulizi ni makali kwa timu zote hapa uwanja wa Samora

Lipuli FC 0-0 Simba SC

18' golikipa wa Lipuli anafanya kazi ya ziada kwa kudaka mpira ambao ulikuwa hatari

Boccoooo..analazimisha kuingia lango la Lipuli lakini mpira unakosa mmaliziaji na kutoka nje

25' Lipuli FC 0-0 Simba SC uwanja wa Samora mkoani Iringa

Mpira ni makali kwa gonga za hapa na pale

Lipuli wanakwenda lango la Simba.. Lakini wanapoteza kwa mabeki kukaa vizuri na kuokoa ile hatari

27' Kichuyaaa anapiga shuti lakini golikipa wa Lipuli anadaka

Wanakwenda hapa Lipuli kwake Adam salamba...

32 'Goooooaaal.... Goooooaaal Adam Salamba anaandika bao la kwanza baada ya kumzidi maarifa beki wa Simba SC

Lipuli FC 1-0 Simba SC

37' Lipuli wanashambulia lango la Simba na. Hakika leo wameamua kucheza vizuri

40' Simba wanapata kona ambayo haikuzaa matunda.. Bado dakika 5 kwenda mapumziko

Okwi anapiga shuti lakini golikipa anadaka bila wasiwasi.

45' Wakati wowote mpira utakuwa mapumziko .. Naam dakika 45+3 za kipindi cha kwanza uwanja wa Samora mkoani Iringa, kati ya Lipuli FC na Simba SC zimekamilika ambapo Simba wako nyuma ya goli moja dhidi ya Lipuli FC

Lipuli FC 1-0 Simba SC

kipindi cha pili cha mtanange wa VPL Lipuli FC Vs Simba SC kimeanza uwanja wa Samora

45' Naam mpira umeanza.. Simba wanafanya mabadiliko. Anatoka Jouko Murshid na nafasi yake inachukuliwa na Mavugo Laudt

47' Simba sasa wanakwenda, namna gani hapa wanapoteza mpira na kuokolewa na mabeki wa Lipuli FC

51' Salamba anakwenda Goo goo laaa, mpira unaokolewa.. Namna gani hapa anakosa bao la wazi. Ilikuwa nafasi mzuri kuandika bao

Mavugo anakwenda na Mpira kwake Kichuyaaa... Mpira unatoka nje na kuwa Goal Kick

Lipuli wanakwenda lango la Simba. Lakini wanapoteza umakini na kuokolewa na mabeki wa Simba SC

56' za mchezo wa VPL.. Lipuli FC 1-0 Simba SC

Mpira wa adhabu kuelekea lango la Lipuli, lakini Kichuya anapiga ndefu na kutoka nje

Kapombe anapiga pasi. Lakini wanapoteza kwao Lipuli sasa. Mpira ni makali kwa timu zote hapa uwanja wa Samora

Nicholas Gyan anang'ang'ana lakini mpira unatoka nje ni wa kurushwa kuelekea lango la Simba

61' mpira wa adhabu kuelekea lango la Simba. Lakini wanapoteza kwake Mavugo anatokea mchezaji wa Lipuli FC na kupiga nje.

Katikati ya uwanja kwake Laudt.. Kwake Asante Kwasi na beki wa Lipuli anatoa nje kuwa kona.. Ambayo inapigwa kuwa kona nyingine..

66' Goooooaaal Goooooaaal Goooooaaal.. Laudt Mavugo anaandika bao la kusawazisha kwa upande wa Simba SC, baada ya kona safi kumfikia.

Lipuli FC 1-1 Simba SC

Haya wanakwenda Lipuli wanapoteza mpira lakini mpira kwao Simba SC

Okwiiii anawekwa chini lakini mwamuzi akasema inuka Okwi

72' Mchezo wa VPL.. Mchezaji wa Lipuli FC Seif anatolewa nje baada ya kupata rabsha

Lipuli FC 1-1 Simba SC uwanja wa Samora mkoani Iringa

Mchezaji wa Lipuli FC yuko chini baada kupata rabsha.. Yamkini Lipuli wameanza kupokeza muda

Okwi kwake Asante Kwasi.. Kapombe anapiga shuti golikipa anapangua

Seif anaingia lango la Simba anapiga shuti.. Kutoka nje na kuwa Goal Kick

82' za mchezo wa VPL.. Lipuli FC 1-1 Simba SC uwanja wa Samora

84' mpira wa adhabu kuelekea lango Lipuli FC.. Okwiiii anapiga lakini golikipa anapangua na kuwa kona.

Wakati huo golikipa wa Lipuli yuko chini baada kupata rabsha. Lakini amenyanyuka

90+3
Za mchezo wa VPL.. Kuendelea kumalizika kwa kipindi cha pili

Lipuli FC 1-1 Simba SC uwanja wa Samora

Naam mpira umekwisha uwanja wa Samora mkoani Iringa patashika ya ligi kuu Tanzania bara VPL.
Ambapo timu zimetoshana nguvu kwa kila timu kupata sare ya goli moja kwa moja. Kwa matokea hayo Simba inaendelea kushika usukani kwa kufikisha alama 59 kwenye msimamo wa ligi.

Lipuli FC 1-1 Simba SC
 
Mashabiki wa soka wakiwa tayari kuingia uwanja wa Samora, Iringa kushuhudia mtanange Simba SC Vs Lipuli FC.
FB_IMG_1524314594982.jpg
FB_IMG_1524314601282.jpg
 
Mods tuwekee hizo picha kwenye thread huku inakataa.. Tafadhali
 
Okwi anapiga paleee lakini golikipa wa Lipuli anadaka
 
Back
Top Bottom