Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 49,759
- 118,798
Kwa hii post Sea nimekupa like tena ile yenye Makopa mawili. 😂😂😂Narudia tena. Miaka ya nyuma vilabu hivi vikubwa Simba na Yanga vilikua na kasumba ya kuchukua wachezaji kutola Afrika Magharibi. Nilikua naona wanakosea sana kwani mchezaji wa kiwango kutoka upande huo wa Afrika hawezi kuja Tz kucheza soka la hali ya juu. Ama atakwenda Ulaya au hata Asia au Afrika ya Kaskazini
Nikawa nashauri kua kuna wachezaji kutoka DRC na Burundi wana viwango vikubwa sana na ni cheap lakini ilichukua muda hadi miaka ya hivi karibuni ndio viongozi wa vilabu vyetu wamegundua hilo
Ujinga mwingine upo kwenye kuamini makocha wa kizungu kuwa wana viwango vizuri. Ni kweli lakini sio makocha wote hasa hawa wanaokuja kufundisha Tanzania.
Kama kuna kosa Simba walilifanya ni kumuondoa Masoud Djumaa. Nadhani ipo siku watakuja kugundua kosa lao na pengine yaweza kua too late
#mkifungwamnakaulitamukamasukari.