Ligi kuu Tanzania bara itaeendelea tena leo ambapo mechi kubwa na ya kutazamwa ni kati ya Young Africans na Biashara united
Yanga wanaingia katika mchezo huu wakiwa wanaongoza ligi wakiwa na point 51 point 11 mbele ya biashara waliopo nafasi ya nne wakiwa na point 40
Ikumbukwe mara ya mwisho kukutana Yanga walitoka na ushindi wa 1 kwa sifuri goli lililofungwa na mshambuliaji hatari wa kigeni kutoka Ghana Michael Sarpong katika dk ya 68 ya mchezo huo uliopigwa 31/10/2020
Mechi tano za mwisho Yanga kashinda 1 kapoteza 1 na droo 3 wakati biashara kashinda 2 kadroo 2 na kupoteza 1.
Ni mechi muhim kwa Yanga ambao inabidi washinde ili wajikite kileleni kwan sare au kupoteza kutampa nafasi Mtani wake Simba ambaye anahitaji point 3 ili kwenda kileleni na ana mechi kesho dhidi ya mwadui,ikumbukwe simba anazihitaji point 3 za mwadui kwani toka msimu huu kuanza hajawahi kuongoza ligi.
Mchezo utapigwa saa moja kamili jioni
Kaa nami kuanzia sasa nikuletee uchambuzi wa kina na matangazo mubashara ya mchezo huu
NB; KILA LA KHERI WATANI WANGU WA JADI KWANI MKISHINDWA KUPATA POINT 3 LEO KESHO NAWAKIKISHIA TUTAMFUNGA MWADUI NA KUPOTEZA MATUMAINI YENU RASMI YA KUCHUKUA UBINGWA