Vodacom Premier League: Yanga yaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara

Vodacom Premier League: Yanga yaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara

Yaani wachezaji kama Mwamnyeto, Ditram Nchimbi na Sarpong, eti wanasugua benchi! Huku ni kutokujitambua kabisa kwa baadhi ya wachezaji!

Anyway, nawatakia ushindi. Ingawa sijafurahishwa na matokeo ya mechi chache zilizopita.
 
Kikosi cha biashara kinachoanza leo dhidi ya yanga
Screenshot_2021-04-17-19-00-38.jpeg
 
Utopolo waoga sana, mpira dakika 20 lakini hapa hawajitokezi kwenye Uzi

Hawajiamini
 
...goli lilifungwa na mshambuliaji hatari kutoka Ghana Michael Sarpong😊😊😊
Ligi kuu Tanzania bara itaeendelea tena leo ambapo mechi kubwa na ya kutazamwa ni kati ya Young Africans na Biashara united

Yanga wanaingia katika mchezo huu wakiwa wanaongoza ligi wakiwa na point 51 point 11 mbele ya biashara waliopo nafasi ya nne wakiwa na point 40

Ikumbukwe mara ya mwisho kukutana Yanga walitoka na ushindi wa 1 kwa sifuri goli lililofungwa na mshambuliaji hatari wa kigeni kutoka Ghana Michael Sarpong katika dk ya 68 ya mchezo huo uliopigwa 31/10/2020

Mechi tano za mwisho Yanga kashinda 1 kapoteza 1 na droo 3 wakati biashara kashinda 2 kadroo 2 na kupoteza 1


Ni mechi muhim kwa Yanga ambao inabidi washinde ili wajikite kileleni kwan sare au kupoteza kutampa nafasi Mtani wake Simba ambaye anahitaji point 3 ili kwenda kileleni na ana mechi kesho dhidi ya mwadui,ikumbukwe simba anazihitaji point 3 za mwadui kwani toka msimu huu kuanza hajawahi kuongoza ligi


Mchezo utapigwa saa moja kamili jioni

Kaa nami kuanzia sasa nikuletee uchambuzi wa kina na matangazo mubashara ya mchezo huu


NB; KILA LA KHERI WATANI WANGU WA JADI KWANI MKISHINDWA KUPATA POINT 3 LEO KESHO NAWAKIKISHIA TUTAMFUNGA MWADUI NA KUPOTEZA MATUMAINI YENU RASMI YA KUCHUKUA UBINGWA
M
 
Lamine Moro tatizo ni nini? Mechi ya pili sasa haonekani hata benchi
 
Dk ya 43 mambo bado magum kwa team zote mbili japo business wamepaki bus
 
Yanga toeni draw bas mtupe nafas nasie tuongoze ligi hatujaongoza toka inaanza na huu ni mzunguko wa 26
 
Back
Top Bottom