Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Hata mimi ilitokea hivyo hivyo. Nilijiunga na kifurushi cha shiling 3500/= lakini baada ya kupiga simu dakika 2 tu simu ikakatika na nikapata ujumbe kuwa sina salio la kupiga simu. Vodacom ni wezi sana. TCRA inatakiwa kuwafungia wezi kama hawa wanaoibia wateja wake.
 
Nyie wezi msha2chukulia makoro na mtandao wenu voda watumie wazee kwangu me kijana xiwezi kutumia mme2ibia kwenye data kwa ma2mizi ya kijana mb 8 zitamuxaidia nn nawakati kitabu chetu kipo kwenye mtandao
 
Kwanini mnakomaa kubaki vodacom?
Kila siku mnalalama kuibiwa na gharama kupanda!!
Infact voda ni wezi wakubwa tu tena waepukeni hivi watauzaje 8mb kwa Tsh 1,000??

Ht mi nawashangaa
Chukueni hatua,hameni.
Mi line yao situmii sshv ni ya kupokea tu
 
Tatzo zio vodacom tatzo ni serikali yetu sik zote data na call ni vitu viwil tofaut nawashangaa nyie msiojua
 
Serikali yetu inayoona fursa kwa wanyonge na masikini ndio wa kukamuliwa, badala ya kupandiksha kodi kwenye madini na biashara zingine kubwa eti yenyew imeona simu ndio pa kukandamiza wanyonge wasiojatambua wengi wa tanzania
 
Tarehe 19/2/2015 nilifanya booking fast jet na kulipia kwa m pesa
booking ya kwanza ina refference fboh27 wakati nalipia ilionekana kuwa ime expire hivyo nilitakiwa kufanya booking upya, hata hivyo mrejesho huo ulifanyika baada ya kulipa fedha kwa mpesa, vivyo hivyo kwa booking ya pili fboif5 ambayo pia baada ya kulipia ilionyesha kuwa ime expire! Nikafanya booking ya tatu ambayo ilikubali hivyo kuacha kiasi cha shilingi 389,000 hewani. Baadaye siku hiyo hiyo usiku nilirejeshewa tshs 194,500/= ya booking ya kwanza, toka hapo chenji yangu nyingine imekuwa inachkua muda mrefu kurejeshwa mpaka hii leo 24/2 nimezungumza na agent anasema itarejeshwa ndani ya siku saba!!!! Hivi siku saba ninaishije mimi ukizingatia kuwa nililipia 583,500 ambazo hazikuwa kwenye plan yangu kutokana na mfumo wa siku hiyo wa fast jet (online booking) kuwa na shida kwa kue xpire ndani ya muda mfupi booking, hivyo nimeona nije hadharani hapa ili mnifanyie chap chap kurejesha pesa hiyo 194,500 manake kila unapoulizia salio mpesa zinakatwa tu!!!
 
Naomba jibu lenu Voda. Kwa nini mtu akinunua bundle kwa mfano MB 700, akitumia zikifika MB650 inaonyesha kuwa MB zimekwisha? Na huduma inakata?
 
Ninaomba Vodacom mnipe namna ya kujitoa kwenye huduma yenu ya Simutv kwani inanisumbua, inanimalizia salio na kibaya zaidi sikumbuki kama niliwahi kujiunga nikifahamu. Au yeyote humu anayefahamu namna ya kujitoa anielimishe kwani nimechoka na hizi updates za kila dakika za Azamtv.
Asante.
 
Hivi hizi million mia za January na James rugemalila. a.k.a Jay millions zipo kweli ? . mbona kama taarifa zimekuwa ndogo sana za washindi. Toka shindano limeanza hadi Leo hii .list inaweza kuwekwa hapa. Tuanze na mmoja wa 100m. , kumi wa 10m, na mia wa 1m. Maana siamini nahisi kama ni danganya toto
 
Mtandao wa Vodacom mara kadhaa umeniadhiri hususan wakati wa kununua Luku kupitia mtandao wao. Sijawahi kupata charge mapema kama mitandao mingine. Ni kero kutumia Vodacom kwani unaweza kukaa hata masaa 6 hujapata majibu na umeme umeshakata. Hii sio sawa marekebisho makubwa yanahitajika ili ku-gain customers confidence.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…