Tarehe 19/2/2015 nilifanya booking fast jet na kulipia kwa m pesa
booking ya kwanza ina refference fboh27 wakati nalipia ilionekana kuwa ime expire hivyo nilitakiwa kufanya booking upya, hata hivyo mrejesho huo ulifanyika baada ya kulipa fedha kwa mpesa, vivyo hivyo kwa booking ya pili fboif5 ambayo pia baada ya kulipia ilionyesha kuwa ime expire! Nikafanya booking ya tatu ambayo ilikubali hivyo kuacha kiasi cha shilingi 389,000 hewani. Baadaye siku hiyo hiyo usiku nilirejeshewa tshs 194,500/= ya booking ya kwanza, toka hapo chenji yangu nyingine imekuwa inachkua muda mrefu kurejeshwa mpaka hii leo 24/2 nimezungumza na agent anasema itarejeshwa ndani ya siku saba!!!! Hivi siku saba ninaishije mimi ukizingatia kuwa nililipia 583,500 ambazo hazikuwa kwenye plan yangu kutokana na mfumo wa siku hiyo wa fast jet (online booking) kuwa na shida kwa kue xpire ndani ya muda mfupi booking, hivyo nimeona nije hadharani hapa ili mnifanyie chap chap kurejesha pesa hiyo 194,500 manake kila unapoulizia salio mpesa zinakatwa tu!!!