Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Weka namba ya tigo pesa hapa tukuchangie pesa ya wakili.., mi binafsi nakerwa sana na hawa wezi watakuja kuzoea. leo kwako kesho kwa mwingine.., pereka kotini hao mbwa..!!!
 
tayari watu washajitolea pesa ya wakili andaa nyaraka zote za ushahidi kabisa
 

wanajeuri sana. nahisi wamejisahau.
 
Voda badilikeni acheni ubabaishaji,hata mimi yalishanikuta laini yangu anatumia mtu mwingine
 
Voda voda voda
please you need to change
kila siku posts zenu tu
who the hell are you?!!
Mkiona hivi ujue mna tatizo kweli..!!
 
pia gharama zao za kupiga simu zimekuwa juu sana, jana nilipiga voda kwenda voda dakika 2 na nusu ikanigharimu shilingi 900!
 
...nimesha wasiliana na lawyer tunaenda kuandaa notification ya intention ya kwenda mahakamani endapo hawatakubali kuwajibika kwa uzembe huu, nitawapa mrejesho...
 
Cheka bombastick kila uchao wnapunguza dakika tu. Nimeiacha on kwa ajili ya kupokea tu, siku nikipata dharula na katika mazingira ambayo sina namna nyingine ya mawasiliano basi hukubali yaishe.
 

Hawa jamaa wajinga sana kama TRA! Yaani unajiunga hela nyingine inabaki kwenye akaunti kuu, unatumia unastukia jiunge imeisha bila kupata taarifa kwamba kifurushi chako kimeisha kucheki salio na kwenyewe wamelamba! Salio kule likiisha ndo wanakutumia meseji kifurushi chako cha Cheka kimekwisha! Shen.zy kabisa hawa! Hivi nani anaweza kutuanzishia mgomo Wa kuwasusia hawa wajinga!
 

wadau mimi nilikua natumia voda miaka 2 iliyopita kwa ajili ya intanet,nilikua natumia kifurush cha wiki,ikatokea mara 2 voda wananikata zile bunde napo sign in tu,hasa huwa na-browse,from there nakiri,nilivunja line.......
 
du! kumbe hadi tigo na airtel?

ila najua huwa baada inactivity ya miezi 3 system zao huwa zinairudisha line sokoni. ila inatakiwa kama kuna hela wazitunze
Warudishe basi documents ulizosajilia.Likitokea la kutokea,usitiwe hatiani kama mmiliki wa line husika.
 
Habari Gefu, endapo namba hii aliitumia kwa muda kisha akaacha kuitumia kwa zaidi ya miezi 3 namba hufutwa taarifa za awali na pesa yake inatunzwa akaunti maalum ambapo mteja atatakiwa kwenda Vodashop kujaza fomu na atapatiwa pesa kwenye namba mpya atakayokuwa ameijaza katika fomu.

Tunaomba namba ya simu kwa msaada zaidi tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
Mmekuja eeeh, safi sana sasa anzeni kujibu hizi shutuma.
 
Last edited by a moderator:

...nashukuru kwa mrejesho huu,namba hii si kwamba haitumiki,vinginevyo nisingelalamika na nisingepoteza fedha. Kilichotokea ni kuanza kupokea jina na taarifa za mtu ambaye hatumfahamu na yupo mwanza. Namba hii bado tunaitumia na ipo kwenye nyaraka zetu nyingi za muhimu. Nawatumia kwa pm namba na jina tulilosajili...
 
Last edited by a moderator:
mimi binafsi nishatoa post mbili kulalamika

KUHUSU VODA KIUKWELI mmejisahau sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…